KWELI Kufanya mapenzi wakati wa ujauzito Kunaweza kuongeza kwa kiasi kidogo kichocheo cha kuanzisha uchungu ikiwa siku za kujifungua zimefika

Taarifa hii imethibitika kuwa ya kweli baada ya kufanya tathmini ya kina
Wakuu wa mambo tunaomba msaada hapa, huku mtaani kwetu kumekuwa na maneno mengi juu ya Kufanya mapenzi Wakati Ujauzito Kunasaidia Kupunguza maumivu, njia kufunguka kwa haraka wakati wa kujifungua na mtoto kushuka haraka wakati wa kujifungua, je kuna ukweli katika Hili?

1708860793881.jpeg

 
Tunachokijua
Ujauzito ni hali ya mtu mwanamke kubeba kiumbe (mtoto) kwenye tumbo la uzazi hali hiyo hutokea baada ya yai la mwanamke(ovari) na mbegu za kiume kukutana na kufanyika urutubishaji uliopelekea kutungwa kwa ujauzito(mimba)

Hali hiyo kwa kawaida inadumu kwa wiki 38 (miezi tisa) ambapo nadi ya iezi 9 hukua na kukomaa ndani ya tumbo la uzazi la mama hadi wakati wa kujifungua.
375px-PregnantWoman.jpg

Kufanya mapenzi(ngono) ni tendo la kujamiiana kati ya mwanamke na mwanaume.

images
Mama mjamzito anaweza kuendelea kujamiiana na mwenza wake katika kipindi chote cha ujauzito ikiwa hali yake ya kiafya inamruhusu kufanya hivyo(Hana tatizo la kiafya linalomzuia kufanya hivyo kama kutoka damu ukeni nk)

Hata hivyo kumekuwa na dhana kwamba kufanya mapenzi wakati wa ujauzito hasa zile siku za mwishoni humsaidia mama mjamzito kutokuchukua muda mrefu anapojifungua, akipata uchungu ajifungue ndani ya muda mfupi.

Baada ya mdau wa Jamiicheck kuuliza swali kama kufanya mapenzi kwa mjamzito humfanya mama mjamzito ajifungue kwa haraka akipata uchungu, Jamiicheck imezungumza na Mtaalam wa Afya kuhusu suala hili ambaye ameeleza kuwa:

Wakati Mama Mjamzito anakaribia kwenda kujifungua, zikiwa zimebaki siku chache au muda mchache Mama mjamzito akifanya mapenzi au kuhusiana na mwenza wake na mwanaume huyo akaweka mbegu zake, basi kuna uwezekano wa kuchagiza au kuchochea kwa kiasi fulani au kidogo hali ya kuanza kwa uchungu.

Uchagizo huo unatokana na kwamba mbegu za kiume zina kichocheo kiitwacho Prostaglandin ambacho kinafanana na kile ambacho huchochea kuanza uchungu au tunamwekea mama kumuanzishia uchungu kwa hiyo hicho kichocheo wakati anaweka mbegu, mbegu zikiingia kwa kiwango kidogo sana kinaweza kuchangiza kwa kiasi fulani.

Hivyo ni kweli kufanya mapenzi kunaweza kuchangiza au kuchochea kwa kiasi fulani au kidogo sana kwa sababu mbegu za kiume zina hicho kichocheo ambacho kinafafana kwa kiasi fulani na kichocheo ambacho huwa mama anawekewa ili kuanzishiwa uchungu.

Pia huweza kusaidia kwa kiasi fulani au kidogo njia kufunguka kwa urahisi kutokana na kichocheo cha Prostaglandin kuwepo kwenye mbegu za kiume ambacho hufanana na kichocheo ambacho mama mjamzito huwa anawekewa ili kuanzishiwa uchungu(Uchungu kuanza maana yake kuanza kufunguka kwa njia)

images
Lakini kuwepo kwa kichocheo hicho hakumaanishi kwamba kutamsaidia mama, mtoto kushuka wakati wa kujifungua, hakuna mahusiano kati ya mtoto kushuka na uwepo wa kichecheo cha Prostaglandin kwenye begu za kiume. Hivyo Hukufanyi mtu kujifungua kirahisi, yaani akipush mtoto anatoke kirahisi.

Pia haimaanishi kutamsaidia ama kupunguza maumivu ya uchungu, hakuna uhusiano wowote kati ya maumivu ya uchungu na kufanya mapenzi kwani uwepo wa kichocheo hicho hakuhusiani kwa chochote na maumivu ya uchungu.

Tendo hilo halina uhusiano wa aina yoyote na Mama mjamzito kujifungua salama.


Zipo faida mbalimbali za kufanya mapenzi kwa mama mjamzito ikiwemo ya kumuondolea msongo wa mawazo mama Mjamzito, hivyo mbali na kupata hicho kichocheo ambacho kinaweza kuchagiza kwa kiasi kidogo kufunguka kwa njia anaweza kupata faida nyingine, na kuendelea kufurahia maisha yake akiwa katika hali hiyo ya ujauzito.

Kutokana na majibu ya mtaalam wa Afya, Jamiicheck imejiridhisha kuwa ni kweli kufanya mapenzi wakati wa ujazito hasa siku za mwishoni huweza kuchochea kwa kiasi fulani kuanza kwa ujauzito, na kwamba tendo hilo halihusiki kupunguza maumivu ya uchungu wala mtoto kushuka kwa urahisi.
Kichwa cha habari umeuliza kuhusu kujifungua salama, ila mbele umeongelea kuhusu maumivu.

Uchungu upo pale pale hata ukisanzuka mpaka siku ya mwisho.

Kama hutaki kujisikia uchungu nenda Agakhan wakupige epidural.Utamaliza pesa yako yote.
 
Japo sina experience ila kwa uelewa nafahamu kufanya mapenzi wakati wa ujauzito inasaidia kupanua sehemu ya uke wa mwanamke hii inaweka urahisi zaidi wakati wa kujifungua pia inaepusha kujifungua kwa njia ya upasuaji kwa mwanamke mwenye uzazi wa kwanza.
 
Wakuu wa mambo tunaomba msaada hapa, huku mtaani kwetu kumekuwa na maneno mengi juu ya Kufanya mapenzi Wakati Ujauzito Kunasaidia Kupunguza maumivu wakati wa kujifungua, je kuna ukweli katika Hili?

Hizi ndio mada zenu

Bora tatizo la umeme lisiishe

Mmbaki gizani
Na sukari izidi kupanda bei
 
Japo sina experience ila kwa uelewa nafahamu kufanya mapenzi wakati wa ujauzito inasaidia kupanua sehemu ya uke wa mwanamke hii inaweka urahisi zaidi wakati wa kujifungua pia inaepusha kujifungua kwa njia ya upasuaji kwa mwanamke mwenye uzazi wa kwanza.

Tuna danganyana sana na upuuzi mwingi,muda wa kuzaa ukifika mishipa yote ya utelasi na uke inatanuka kwaajili ya kupitisha mtoto,sasa mwili wa mtoto na hicho kiuboo kipi kinatanua k to the maximum?
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom