Kwanini Mungu yupo?

Kwanini Mungu yupo?

Kama hamna faida nayopata siwezi kutaka aniheshimu.
Lakini kama akiniheshimu hawezi kuniibia,Kunipiga,kunitukana,kunisingizia,kunisaliti nk ...Basi Nataka aniheshimu.

Na kama heshima haihusiani na hivyo vitu, yaani mtu anaweza kuniheshimu ila akaniibia,akanipiga,akanitukana,akanisengenya...Basi hiyo heshima Haina maana yoyote kwangu

Kipi usichoelewa hapo?
Kwani mtu kukuibia ni kukudharau!?...
 
Kwani mtu kukuibia ni kukudharau!?...
Huwezi ukaniheshimu halafu ukaniibia.
Maana ya kuniibia ni kwamba umeona Mimi sifai kumiliki hiyo Mali, lakini kwakuwa wewe ni Bora zaidi, hiyo Mali inakufaa wewe, ndiyo maana umeamua kuninyang'anya Kwa kuniibia.

Huwezi kumuheshimu Mzazi halafu ukamdhulumu au kumuibia.
(Kuna watoto wanaibia mpaka wazazi wao)
 
Mungu anao uwezo wa kufanya kile anataka bila kulazimika kuelezea chochote.
 
Kitendo cha kuishi katika ardhi umeagizwa utunze ardhi hiyo ili ikupe chakula
Safi sana, we are going somewhere.
Kwahyo kazi kubwa ya sisi binadamu ni kuitunza hii Dunia ili itupe chakula.
Sasa hii ardhi tukiitunza Mungu anapata faida Gani? Nayeye anaitumia au?

Halafu mbona naona kama hii Dunia ingekuwa sehemu Bora zaidi bila binadamu?? Sisi binadamu ndio tunaleta maswala ya pollution,global warming, climate change,nk. Yaani binadamu mpaka imefikia hatua tunatupa mabomu ya nuclear baharini,kuua viumbe, na kuyatupa nchi kavu na kuiharibu nchi.
Tunaongoza Kwa kukata miti, Tunaongoza Kwa kuchafua mazingira.

Na hata kama tuassume ni kweli tumeumbwa ili kuitunza hii Dunia...Inamaana hii Dunia ni ya muhimu kwa Mungu kuliko sisi....ndomaana ametuumba vijakazi vya kuitunza Dunia yake.
Na kama anaithamini hivyo Dunia, inampa yeye faida Gani? Anaila Dunia?.
Kwanini aliiumba Dunia?
 
Mungu anao uwezo wa kufanya kile anataka bila kulazimika kuelezea chochote.
Ndio, nafahamu Hilo..
Ndiomaana sijamuuliza Mungu, nimeuliza Wanadamu tuliopo huku jf.
Ina maana sisi wanadamu hatujui kwanini tupo hapa duniani?Hatujui kwanini tunamuabudu Mungu? Hatujui kwanini Mungu yupo?
Na tunalazimishwa kumuabudu huyu Mungu ambae hatuelezei hata umuhimu wa hizi ibaada kwake?

Mbona huyu Mungu ni kama dikteta, na anataka atuendeshe kama maroboti TU, Yani sisi ni kufuata order zake bila kuwaza hata kwanini tunafata hizo order .

Mimi sidhani sisi ni maroboti ya kufanya vitu kama mazezeta bila kufikiria.
Ndiomaana nikahoji, Kwanini Mungu yupo?
 
Ni fumbo, hakuna mtu atakuja kuelewa
 
Mbona huyu Mungu ni kama dikteta, na anataka atuendeshe kama maroboti TU, Yani sisi ni kufuata order zake bila kuwaza hata kwanini tunafata hizo order .
Angekuwa anakuendesha kama roboti usingeweza kutoa maoni yako hapa kinyume naye.
 
Naona wengi mnamlaumu mtoa mada kwanza mujue kabisa hajakufuru kwa imani yangu ya kiislamu yeye anataka kujua ,kingine anatoa swali litakapojibiwa Inakuwa elimu ....wengi tunafeli sana katika kuelimisha vichache tulivyo navyo mtoa mada amefanya reasoning na wachangia watoe evidence hakuna mahali mtoa mada kakejeli yeye kauliza na katoa assumptions zake
 
Tuendelee kuelimishana jamani, maamuma tupo tunafuatilia na mada kama hizi mi huwa silali mpaka watu wamalize kujadili.
 
Mimi binafsi ntatoa evidences na assumptions zangu kwa kidgo nilichojaaliwa kutokana na vitabu vya dini sema nitabase sana kweny sayari ya uumbaji na "kwa nn mungu yupo" kwa machache ntakayotoa sikuwa na quotes sana Aya coz ntabase kweny maoni zaidi kwa kutumia elimu niliyo nayo ili mkristo na muislamu tuwe pamoja.

Swali: kwa nn mungu yupo?

Naona ni swa na kusema je mungu yupo au sio wajameni.

jibu:Mungu yupo kutokana na sayansi ya uumbaji ulimwengu na uendeshaji wa Maisha ya viumbe vyote duniani na yote yanayotokea dunia kama ifuatavyo,

Asili ya kifo na mwanzo wa Maisha ya viumbe. Hapa duniani tunajua Kuna Maisha ya viumbe hai na visivyo hai basi Nan anataratibu msingi mzima wa Maisha hayo ni kwamba kiumbe hai chochote like dunia kina mwanzo na mwisho wake Inakuwa ni cycle hyo kwamba mtu atazaliwa lakini atakuja kufa hata iweje ni je kipi kinaratabu mzunguko huu basi hapo ni mungu pekeee ,ukitaka kujua hilo wanasayansi washafanya mambo kibao dunia ila waneshindwa kugundua nini asili ya kifo maana vifo vipo kibao unaweza sema magonjwa ila ni sababu sio asili ya kifo Kuna mtu hana ugonjwa ila aneweza kufa ghafla


Utoaji wa rizki na mzunguko katika kutegemeana kwa viumbe hai ili kusurvive(ecosystem). Kama tunavyojua duniani ili tuweze kuishi Kuna vitu kama riziki mfano kula chakula na kujushughulia sasa je ? kama binadamu ana uwezo mkubwa wa kulima na kupanda mazao pamoja na kutumia rasilimali ila kujipatia chakula na kuishi Maisha yake ya kila siku vip kuhusu ndege baadhi wanaotegemea mazao ya binadamu ,vip kuhusu wanyama wanaokula nyama ili waweze kuishi kama sehemu ya mlo wao ,je Nan anaratibu hii ecosystem ya viumbe hai ambayo miaka nenda na rudi ipo ivyo ni kwamba binadamu atalima kweny ardhi ambayo hajui chanzo chake ni nn,mvua itanyesha ,mazao yatkuwa ndege atakuja atakula au binadamu atakula lakini akija kufa na viumbe kama funza akizikwa watakuja kula mwili wa binadamu au ndege na hao funza ndo itakuwa rizki yao.na wao pia wakuja kuliwa hata nguruwe anakula funza nae nguruwe atakuja kuliwa.

Watu kutofautiana na Wanyama. Kwamba watu na Wanyama au viumbe wengine ni vitu tofauti na hapo utakuja gundua kwamba binadamu alipewa akili nyingi ili kuja kucontrol viumbe hai ndo maana hata mitume wa mungu tunaomini dini zote wamekuja katika hali ya binadamu.je ni nan alipanga hii khilafa ya binadamu duniani kama sio mungu katika uumbaji wa ulimwengu ili pawe na kiongozi ulimwengu.Ndo maana binadamu ana power sana hata kama wapo wanyama wakina Godzilla wakubwa ila binadamu anaweza kuwa control. Msukuma mmoja kijitoto anaweza kutumia akili tu akawa anasweka ng'ombe hata hamsini na wakamtii je hii power imetoka wapi .


Uwepo wa nyota, kuzama na kuchomoza kwa jua,majira mbalimbali ya mwaka,kupwa na kujaa kwa maji .Hivi zote na mengine mengi ambayo yanatokea katika dunia yetu ya sasa kama kawaida je who control them? Kwamba kwa nn kila siku jua linachomoza mashariki na kuzama magharibi je nana anafanya ivyo basi ni mungu .Ntakupa mfano hapa dunia vitu vingi sana utajua Kuna kitu kinaendesha hata gari yako Kuna mechanism ambazo zinafanya iwake na liweke kutembea binadamu unakaa tu pale unawasha au kuzima yaani hata kama gari Haina dereva basi Kuna drive force na kitu kinacontrol the same na mambo yote yanayotokea dunia mungu ana ratibu hakuna kiumbe kinaweza hata wajenge jua fake basi itabdi waliendeshe yaani walicontrol. So hili jua la asili ,mvua na mambo mengi je ni nan ana control basi ni Mungu.


Watu kutofautiana lugha ,makabila,rangi ,mataifa ,asili, uwezo wa kufikiria & akili, kuwepo kwa walemavu ,kutofautiana kipato(maskini &matajiri). Hii ni sababu kwa nn mungu yupo je kwa nn watu wengine weupe ,wengine weusi,wengin Wana akili sana ,wengine hawana ,kuwepo kwa maskini na matajiri ,kuwepo kwa walemavu (vipofu viwete, albino,) ni kwamba hayo yote hakuna kiumbe kinaweza kuzuia ,Mfano wewe unaweza kujitkuta automatic umezaliwa Tanzania ila utamanni kuishi ulaya if would be your will ,would rather to choose to be born in USA Than Tanzania, Mungu ndo kapanga huyu awe ivi yule awe ivi hata akili Kuna mtu bogus hata azaliwa na asomeshww vip na inawezekana kabisa wazazi na ukoo wao ukawa wako vizuri kiakili lakini mtoto akaja kuwa bogus hii haipo ndani ya control ya binadamu zaidi ya mungu ndo ana ratibu ivyo, umaskin na utajiri kwa nn wengin Wana kipato kikubwa wengine hawana ?je nan ameweka hili gap ?

HYO BAADHI YA ELIMU SEMA KATIKA UWASILISHAJI KUNA SEHEMU NAWEZA KUWA NIMEKOSEA ILA IVYO VYOTE NILISOMA KATIKA MAARIFA YA UISLAMU KITADO CHA TATU ZIPO SABABU LUKUKI NYINGI SANA SEMA JINSI YA KUZIPANGILIA NA HAPA NATUMIA SIMU NAWEZA KUWA NIKO HURRY SANA NIMEKOSEA LABDA SPELLING ILA NIKO TAYAR KUKOSOLEWA NA KUJIFUNZA
 
Wafia dini hapo ndipo mnapofeli.
Mtu kauliza maswali yake,
Badala ya kutoa majibu unaanza kusema eti ana mapepo.
Huoni kuwa wewe ndiye mwenye mapepo?
Yaani watu kama nyie ndiyo mnafanya watu wazidi kuamini Mungu hayupo.

Mtu akiuliza swali, toa majibu.
Sina dini.

meditation ime tuaribia vijana.

+Chakra+Kundalini+yoga aya Mambo ni uchawi mtupu, na ndio chanzo cha aya .
 
Huwezi ukaniheshimu halafu ukaniibia.
Maana ya kuniibia ni kwamba umeona Mimi sifai kumiliki hiyo Mali, lakini kwakuwa wewe ni Bora zaidi, hiyo Mali inakufaa wewe, ndiyo maana umeamua kuninyang'anya Kwa kuniibia.

Huwezi kumuheshimu Mzazi halafu ukamdhulumu au kumuibia.
(Kuna watoto wanaibia mpaka wazazi wao)
Porojo na blah blah nyingi mjomba
 
Angekuwa anakuendesha kama roboti usingeweza kutoa maoni yako hapa kinyume naye.
Kwasababu nmeshtuka.. mi sio roboti la kufuata maagizo TU bila kujua hata kwann nayafanya.
Ila mabilioni ya waumini it seems wanafata TU bila kujua...Sasa kama wapo wanaojua ndo Nataka namimi wanielimishe kupitia Huu Uzi.
 
na kwanini yupo?
Kwa nini JUA lipo? Kwa nini linatokeza Mashariki na kuzama Magharibi na si Kaskazini au Kusini?

Huwezi ukahoji uwepo wa nature au maumbile yake namna ilivyo. Nature inakuwepo tu pasipo ridhaa yako na baada ya hapo unachotakiwa kuhoji ni SABABU ZA UWEPO WAKE na si kwa nini ipo

Kwa mfano, huwezi ukahoji kwa nini wewe umezaliwa mwanamme au mwanamke ila unaweza ukahoji sababu za wewe kuzaliwa mwanamme au mwanamke.

SI KILA SWALI ULILONALO KICHWANI KWAKO, LINA MAJIBU AMBAYO YANAWEZA KUTOLEWA NA MWANADMU
 
Hakukuwa na error isipokuwa amevipa viumbe free will na ujuzi wa kutambua baya na jema lakini wanatakiwa na anawataka wafanye mema na yule mwenye kushinda huo mtihani atazawadiwa na aliyeshindwa ataadhibiwa.
kama kuna adhabu hiyo haitakuwa free will tena
 
NB: Huu mjadala sio wa kubishana kama mungu yupo au hayupo.
Hapa ninataka kuwauliza Kwa upole wale tunaoamini tayari kuwa Mungu yupo...Je, kwanini yupo?

Yaani siulizi mungu ametokea wapi/ametokanaje...
Hapa naulizia Kuna ulazima Gani wa yeye kuwepo? na kwanini yupo?

Mfano mtu akiuliza kwanini viti vya kukalia vipo, huwezi kujibu kwasababu mbao zikikatwa na kuchongwa vizuri zinatengeneza kiti, hapa utakuwa umejibu viti vinatokanaje....jibu zuri ni kwasababu vinatufanya binadamu tukae na kupumzika, hivyo tumevitengeneza...Inamaana bila kuwepo binadamu wenye shida ya kukaa basi viti visingekuwepo...

Kwahyo napouliza kwanini Mungu yupo? Siulizii chimbuko lake ametokana na Nini, ila naulizia ni sababu Gani iliyompelekea/iliyomlazimu yeye awepo.

Kuna wanaosema Mungu yupo ili auumbe ulimwengu, kwahyo function kubwa ya Mungu ni kuumba na kuendesha ulimwengu.

Hilo jibu kwangu halitoshelezi kwakuwa, Ningeuliza kwanini Huu ulimwengu upo?, Kwani Kuna ulazima ulimwengu uumbwe?

Kama Kuna ulazima wa ulimwengu kuwepo, basi Inamaana ulimwengu una thamani kuliko Mungu, kama binadamu tulivyo na thamani kuliko viti. Maana sisi ndo tumeleta viti, basi Ulimwengu umemleta Mungu.(yaani kama ni lazima ulimwengu uwepo, basi ulimwengu ndio umemlazimu Mungu awepo kama ambavyo Nyumba zinawalazimu mafundi ujenzi kuwepo,Simu zinawalazimu wauza simu kuwepo,Magari yanawalazimu madereva kuwepo, wahalifu wanalazimu polisi kuwepo nk.)

Lakini common sense inakataa.
Ingewezekana TU kusiwe na chochote, Hamna Dunia,hamna,Nyota,Hamna sayari, na Hakuna Mungu.

Sasa kwakuwa hivi vitu vipo, Je ni kwanini vipo?

Na kama ingewezekana kusiwepo kitu,Je ni Nini kililazimisha Mungu awepo?

Na kama mungu alikuwepo kabla ya Ulimwengu, na hakulazimishwa kuumba ulimwengu (angeamua angeacha na kubaki mwenyewe) Je yeye kwanini yupo? Nini kilipekea yeye kuwepo?

Kwanini Mungu yupo?
Kulingana na imani za dini, Mungu alikuwepo, yupo na ataendelea kuwepo (haitaji sababu ya nje ili awepo)

Kama hilo jibu halijitoshelezi kwako, basi inabidi uipinge hiyo imani na kukataa kabisa uwepo wa Mungu.
 
Back
Top Bottom