Kwanini Mungu yupo?

Kwanini Mungu yupo?

Pole pole TU ..nmeandika hasara nyingi mpaka Kupigwa Kuibiwa ila umeona ya kuulizia ni kusengenywa.

Sawa ..Sasa kusengenywa ni kubaya Kwa sababu Moja...Watu wakikusengenya wanakudharau, wakikudharau hawakupi nafasi, hawakusikilizi,hawakuamini,hawakusaidii ukiwa na shida,hawakukumbuki,.
Sasa kama wewe kwako hizo sio hasara basi wewe sio binadamu.

Na kama huoni shida ya kuishi na jamii inayokusengenya,inayokutukana,inayokudharau,isiyokuamini, isiyokulinda. (hata ukiumwa/ukifa haijali), isiyokujali, inayokunyanyapaa na kukutenga Basi utakuwa sahihi kusema hamna faida ya kuheshimiwa.

Na kama wewe huoni hasara ya kudharauliwa na mwanao na kufanyiwa yote hayo juu, Ntakushangaa siku nikikukuta unamlazimisha mwanao akuheshimu.
Hili la faida ya kuheshimiwa na mwanao huna maelezo ya maana...
 
NB: Huu mjadala sio wa kubishana kama mungu yupo au hayupo.
Hapa ninataka kuwauliza Kwa upole wale tunaoamini tayari kuwa Mungu yupo...Je, kwanini yupo?

Yaani siulizi mungu ametokea wapi/ametokanaje...
Hapa naulizia Kuna ulazima Gani wa yeye kuwepo? na kwanini yupo?

Mfano mtu akiuliza kwanini viti vya kukalia vipo, huwezi kujibu kwasababu mbao zikikatwa na kuchongwa vizuri zinatengeneza kiti, hapa utakuwa umejibu viti vinatokanaje....jibu zuri ni kwasababu vinatufanya binadamu tukae na kupumzika, hivyo tumevitengeneza...Inamaana bila kuwepo binadamu wenye shida ya kukaa basi viti visingekuwepo...

Kwahyo napouliza kwanini Mungu yupo? Siulizii chimbuko lake ametokana na Nini, ila naulizia ni sababu Gani iliyompelekea/iliyomlazimu yeye awepo.

Kuna wanaosema Mungu yupo ili auumbe ulimwengu, kwahyo function kubwa ya Mungu ni kuumba na kuendesha ulimwengu.

Hilo jibu kwangu halitoshelezi kwakuwa, Ningeuliza kwanini Huu ulimwengu upo?, Kwani Kuna ulazima ulimwengu uumbwe?

Kama Kuna ulazima wa ulimwengu kuwepo, basi Inamaana ulimwengu una thamani kuliko Mungu, kama binadamu tulivyo na thamani kuliko viti. Maana sisi ndo tumeleta viti, basi Ulimwengu umemleta Mungu.(yaani kama ni lazima ulimwengu uwepo, basi ulimwengu ndio umemlazimu Mungu awepo kama ambavyo Nyumba zinawalazimu mafundi ujenzi kuwepo,Simu zinawalazimu wauza simu kuwepo,Magari yanawalazimu madereva kuwepo, wahalifu wanalazimu polisi kuwepo nk.)

Lakini common sense inakataa.
Ingewezekana TU kusiwe na chochote, Hamna Dunia,hamna,Nyota,Hamna sayari, na Hakuna Mungu.

Sasa kwakuwa hivi vitu vipo, Je ni kwanini vipo?

Na kama ingewezekana kusiwepo kitu,Je ni Nini kililazimisha Mungu awepo?

Na kama mungu alikuwepo kabla ya Ulimwengu, na hakulazimishwa kuumba ulimwengu (angeamua angeacha na kubaki mwenyewe) Je yeye kwanini yupo? Nini kilipekea yeye kuwepo?

Kwanini Mungu yupo?
Kwasababu yupo. Alikuwako yupo na ataendelea kuwako. Hana mwanzo wala mwisho. Ndio sababu mungu yupo
 
Mungu ni baba, kwa maana rahisi ni mzazi, furaha yake ni watoto alioumba, ametuumba kwasababu anafurahia kuwa mzazi, hali kadhalika wewe kuna jambo au hali fulani unayofurahia pale unapoitwa baba ndio maana unatamani kuwa na watoto
 
Hili la faida ya kuheshimiwa na mwanao huna maelezo ya maana...
Kama hamna faida nayopata siwezi kutaka aniheshimu.
Lakini kama akiniheshimu hawezi kuniibia,Kunipiga,kunitukana,kunisingizia,kunisaliti nk ...Basi Nataka aniheshimu.

Na kama heshima haihusiani na hivyo vitu, yaani mtu anaweza kuniheshimu ila akaniibia,akanipiga,akanitukana,akanisengenya...Basi hiyo heshima Haina maana yoyote kwangu

Kipi usichoelewa hapo?
 
Kuna mambo yanafikirisha sana ngoja ni-mute nisije kufuru.
 
Mungu ni baba, kwa maana rahisi ni mzazi, furaha yake ni watoto alioumba, ametuumba kwasababu anafurahia kuwa mzazi, hali kadhalika wewe kuna jambo au hali fulani unayofurahia pale unapoitwa baba ndio maana unatamani kuwa na watoto
Mungu Akifurahi/asipofurahi kuwa watoto wake tupo na tunaendelea vizuri, Nini kinatokea?
Hiyo furaha Ina ulazima Gani kuwepo?

Ina maana lazima hiyo furaha iwepo ndio maana Mungu akawepo na binadamu tukawepo?

Siku Mungu akiamua kutofurahi uwepo wa binadamu, basi hiyo siku Mungu atakufa?
 
Sala na ibada zetu ni sawa na kutoa shukrani kwake kwa zawadi ya kuumbwa
Sasa Nimeelewa maana ya Sala na ibada ...asante sana.
Maana yake tunasali na kuabudu ili kumshukuru Kwa kutuumba....Sasa kwanini akatuumba lakini?
 
Nimeeleea maana ya Sala na ibada ...asante sana.
Maana yake tunasali na kuabudu kumshukuru Kwa kutuumba....Sasa kwanini akatuumba lakini?
Yale yote yanayokufanya wewe kutaka kuwa na watoto ndiyo hayo yaliyompendeza yeye na akatuumba
 
Mungu Akifurahi/asipofurahi kuwa watoto wake tupo na tunaendelea vizuri, Nini kinatokea?
Hiyo furaha Ina ulazima Gani kuwepo?
Ina maana lazima hiyo furaha iwepo ndio maana Mungu akawepo na binadamu tukawepo?

Siku Mungu akiamua kutofurahi uwepo wa binadamu, basi hiyo siku Mungu atakufa?
Asipofurahia basi anaweza kuangamiza na akaumba tena
 
Kwasababu yupo. Alikuwako yupo na ataendelea kuwako. Hana mwanzo wala mwisho. Ndio sababu mungu yupo
Nimeuliza kwanini Mungu yupo? Wewe unajibu kwasababu yupo.

Kwanini Kuna makarani wa sensa?? Kwasababu wapo.

Hiyo ni cyclical arguing.
 
Viashiria vya kuwepo nguvu kuu inayo ongoza au kuendesha dunia. Ukipenda hii nguvu iite mungu.
1. Structure ya Ulimwengu ( Universe). Universe siyo random. Imepangwa ikapangika...Sayari, nyota, hewa, jua etc. kila kitu mahali pake na kwa namna ya kipekee. Bila shaka hii haikutokea kwa bahati mbaya ila ilikuwa planned. Well planned. Kama ilikuwa planned nani ali i plan?

2. Viumbe. Viumbe vingi vimeumbwa kwa nanmna ya ajabu ili kuwezesha kuishi katika mazingira fulani. viko vya majini (Marine), nchi kavu, angani n.k. Kila kimoja kina structure ambayo binadamu hutumia miaka mingi kuvijua. Bila shaka havikutokea kwa bahati mbaya. Kuna kitu kiliviumba kwa ustadi mkubwa. Je ni kitu gani hicho?

3. Maisha yetu hapa dunia. Ukiangalia kila mtu duniani anapata riziki yake na maisha yanasonga kwa namna tofauti. Kuna wakati unakwama lakini ghafla unapata suluhu kwa namna ambayo hukuitarajia.

Religious poeple hasa hizi dini za kisasa ndo zinaharibu maana ya Mungu. Zinapotosha na kufanya watu kuwa watumwa badala ya kuwa huru kutumia nguvu hii. Lakini naturalist wanatambua nguvu inayoendesha dunia, na namna unavyoweza kuitumia ili uwe na heri dunia.
 
NB: Huu mjadala sio wa kubishana kama mungu yupo au hayupo.
Hapa ninataka kuwauliza Kwa upole wale tunaoamini tayari kuwa Mungu yupo...Je, kwanini yupo?

Yaani siulizi mungu ametokea wapi/ametokanaje...
Hapa naulizia Kuna ulazima Gani wa yeye kuwepo? na kwanini yupo?

Mfano mtu akiuliza kwanini viti vya kukalia vipo, huwezi kujibu kwasababu mbao zikikatwa na kuchongwa vizuri zinatengeneza kiti, hapa utakuwa umejibu viti vinatokanaje....jibu zuri ni kwasababu vinatufanya binadamu tukae na kupumzika, hivyo tumevitengeneza...Inamaana bila kuwepo binadamu wenye shida ya kukaa basi viti visingekuwepo...

Kwahyo napouliza kwanini Mungu yupo? Siulizii chimbuko lake ametokana na Nini, ila naulizia ni sababu Gani iliyompelekea/iliyomlazimu yeye awepo.

Kuna wanaosema Mungu yupo ili auumbe ulimwengu, kwahyo function kubwa ya Mungu ni kuumba na kuendesha ulimwengu.

Hilo jibu kwangu halitoshelezi kwakuwa, Ningeuliza kwanini Huu ulimwengu upo?, Kwani Kuna ulazima ulimwengu uumbwe?

Kama Kuna ulazima wa ulimwengu kuwepo, basi Inamaana ulimwengu una thamani kuliko Mungu, kama binadamu tulivyo na thamani kuliko viti. Maana sisi ndo tumeleta viti, basi Ulimwengu umemleta Mungu.(yaani kama ni lazima ulimwengu uwepo, basi ulimwengu ndio umemlazimu Mungu awepo kama ambavyo Nyumba zinawalazimu mafundi ujenzi kuwepo,Simu zinawalazimu wauza simu kuwepo,Magari yanawalazimu madereva kuwepo, wahalifu wanalazimu polisi kuwepo nk.)

Lakini common sense inakataa.
Ingewezekana TU kusiwe na chochote, Hamna Dunia,hamna,Nyota,Hamna sayari, na Hakuna Mungu.

Sasa kwakuwa hivi vitu vipo, Je ni kwanini vipo?

Na kama ingewezekana kusiwepo kitu,Je ni Nini kililazimisha Mungu awepo?

Na kama mungu alikuwepo kabla ya Ulimwengu, na hakulazimishwa kuumba ulimwengu (angeamua angeacha na kubaki mwenyewe) Je yeye kwanini yupo? Nini kilipekea yeye kuwepo?

Kwanini Mungu yupo?
Swali lako ni zuri, nahisi nimelielewa.

Kwa ufupi, Wanadamu huhisi kuwepo kwa Mungu—au kile wanachokiona kuwa ni uwezo wa juu zaidi—kwa silika safi, pamoja na au bila ufunuo wa kinabii wa kuwaongoza. Matamshi ya yabkwanini Mungu awepo hujibika bila mipaka wala maneno, hayo yameonekana katika tamaduni na dini kote ulimwenguni, licha ya kuwa yametenganishwa sana na wakati, jiografia na lugha.

Kwa maneno ya kiroho ya Kiislam, hii ni kwa sababu Mungu amempankila mtu (fitrah) ya kumtambua Muumba wao na uwepo wake.
 
Swali lako ni zuri, nahisi nimelielewa.

Kwa ufupi, Wanadamu huhisi kuwepo kwa Mungu—au kile wanachokiona kuwa ni uwezo wa juu zaidi—kwa silika safi, pamoja na au bila ufunuo wa kinabii wa kuwaongoza. Matamshi ya yabkwanini Mungu awepo hujibika bila mipaka wala maneno, hayo yameonekana katika tamaduni na dini kote ulimwenguni, licha ya kuwa yametenganishwa sana na wakati, jiografia na lugha. Kwa maneno ya kiroho ya Kiislam, hii ni kwa sababu Mungu amempankila mtu (fitrah) ya kumtambua Muumba wao na uwepo wake.
Jibu lako ni zuri lakini halijajibu swali langu lolote.
Lakini ngoja tuanze kujadili jibu lako kwanza
1.kila binadamu huhisi uwepo wa Mungu
-Hapana, Mila na dini ndio zinatuambia habari na mambo ya Mungu tukiwa wadogo, mtoto akianza kuambiwa hakuna Mungu tokea utotoni hawezi kuhisi huo uwepo wa Mungu .

2.Matamshi ya yabkwanini Mungu awepo hujibika bila mipaka wala maneno, hayo yameonekana katika tamaduni na dini kote ulimwengun
-Ninataka majibu Sasa ya hayo matamshi maana sijaona jibu lolote.
Uwepo wa Tamaduni na dini ulimwenguni ndio sababu ya Mungu kuwepo??

Turudi kwenye Maswali yangu;
Kwanini Mungu Mungu yupo?
Kwanini sisi binadamu tupo?
 
Back
Top Bottom