Kwanini Mukama alipigwa chini ukatibu mkuu CCM?

Kwanini Mukama alipigwa chini ukatibu mkuu CCM?

Mimi naona sababu kubwa ni Katibu wake wa Itikadi na Uenezi Nape Nauye kujitwalia madaraka ya kusema kila kitu mpaka akavuka mipaka na kuonekana wazi Mzee Mukama hana kazi anayofanya.

Kosa hilo hilo ndilo limeanza tena sasa ambapo kwa makusudi Nape amekuwa akimfunika Mzee Kinana kwa kuongea kila kitu hovyo hovyo.Ama anafanya kwa makusudi au kutokujua lakini hii imeshaanza kuonekana Mzee Kinana hana kazi anayofanya kwa sababu kila kitu anarukia Nape.

Pia Nape kwa kuwatumia waandishi wa habari wa hapo Lumumba kila anachofanya yeye harakaharaka kinapostiwa kwenye blogs zote nchini na picha mbalimbali.Lakini ni nadra kukuta habari za Kinana zimepostiwa kwenye blogs..

Je huu ni mkakati wa kummaliza Kinana kama ilivyokuwa kwa Mukama? Muda tu ndiyo utakaoamua.
 
RIP mukama.Msiba wake ulianzia pale Mbowe alipomtoa ukware ktk hotuba.Mukama kama wana CCM wengine wajinga alikuwa affected na uongo wa CCM kuliko mtu mwingine yoyote.Kaamini uongo aliokusudia kumuaharibu mtu miwngine.

Hao ndio magamba ndege wa aina moja wanaruka pamoja.Wanadanganyiak kirahisi sana, siku hizi wameamua jidanganya wao wenyewe.
 
Aliwaingiza chaka kuwaambia JF ndiyo iliyowanyima ushindi wa kishindo na wakaingia gharama kujaza misukule yao hapa jamvini,baada ya kugundua kuwa ule ulkuwa ushauri feki na umewagharimu mabilioni kuilipa hiyo misukule kwa kazi isiyo kuwa na tija ndiyo wakammwaga. Na sababu nyingine alikuwa akiwalowesha mate wenzie kwenye vikao.
 
Alishindwa kurudisha mikono mwa CCM jimbo la Arumeru Mashariki.
 
You cant teach an old dog new tricks jamaa alileta mambo yake ya USSR bila kujua kuwa kwa sasa kuna Urusi tuu ile USSR ishakufa so ata strategy zimekufa yeye akawa anakomaa kuzi Adopt bila mafanikion
Chukua experience kwa Mangula juu na namna ya kuwa mkulima bora uko kwenu Mh Mukama
 
*Huu ni wakati wa Mangulla na Kinana kutumiwa kama Condom!![/QUOTE]

Kwa maneno mengine ni kwamba jamaa ameamua kubadili aina ya kondomu!
 
Tofauti kubwa ya Mkama na Jk ilikuwa kuwatosa mafisadi kitu ambacho Kikwete hakuwa tayari kukitekeleza matokeo yake akawa anamfanya kama Mkama anatoa maamuzi binafsi badala ya maamuzi ya chama na hata sekretarieti aliyomuundia ilikuwa inahisha makundi yaliyotakiwa yafutwe
 
Nakumbuka alipoteuliwa alianza kazi kwa mbwembwe nyingi, akikomalia propaganda ya kujivua gamba lkn kadiri Siku zilivyoyoyoma akawa kimyaaaaaaaaaa!!! Akimwacha Nape anahangaika vyake.

Nasikia pia yeye ndo alifanya utafiti na kumpelekea JK taarifa ya page nyingi yenye material yaliyopelekea JK kuja na single ya kujivua gamba nimelinganisha na kutofautisha mchango kati yake na Kinana nikaona angalau Mukama alifanya Kitu kuliko Kinana naleo nimemsikia kinana akisema baada ya uteuzi watu wanaisifia sekeetarieti iko safi.

Ebu nisaidieni sababu ya kuachwa Mukama ni nini?

Ni kwa sababu kakataa kusilimu!
 
Tofauti kubwa ya Mkama na Jk ilikuwa kuwatosa mafisadi kitu ambacho Kikwete hakuwa tayari kukitekeleza matokeo yake akawa anamfanya kama Mkama anatoa maamuzi binafsi badala ya maamuzi ya chama na hata sekretarieti aliyomuundia ilikuwa inahisha makundi yaliyotakiwa yafutwe
 
Back
Top Bottom