CCM imekuwa ikianguka kila inajaribu kuinuka

karama kaila

Senior Member
Jan 30, 2015
122
60
Nakumbuka wakati wa Katibu Mkuu Yussuf Makamba CCM walipata shida sana kwenye kura za maoni.

Mchakato wa kura za maoni uligubikwa na hila nyingi tena zikiratibiwa kutoka ofisi ya Katibu Mkuu wa chama.

Ni kipindi ambacho CCM ilitengeneza wahanga wengi wa kura za maoni.

CCM iligundua kosa lake ikaamua kuinuka kutoka kwenye anguko lile na kumkabidhi ukatibu Mkuu Mzee Mukama.

Hapa ndiyo walipoanguka zaidi baada Mukama kuja na falsafa ya kujivua gamba safari hii wahanga wakawa ni wanamtandao waliomuingiza Mwenyekiti wa CCM Taifa madarakani hapa hali ilikuwa mbaya zaidi vita ya makundi ikashamiri zaidi.

Ili kuweka hali sawa CCM ikabidi imkabidhi ukatibu Mkuu Kanali wa jeshi mstaafu Abdulrahman Kinana.

Naye bila kusita akaanza ziara kama ile ya kujivua gamba Lakini kwa wakati huu ikiwa na sura tofauti na kuwa ziara ya kuivua nguo serikali.

Ofisi ya katibu Mkuu ilishindwa kuangalia athari za makundi yaliyomea ndani ya chama baada ya Operesheni vua gamba.

Hapa CCM ilijiweka uchi nakiri kusema matokea ya leo wapinzani Kuwa na wabunge wengi ni Operesheni hii, na matokea ya nguvu ya lowasa kwenye uchaguzi Mkuu uliopita ni Operesheni vua gamba.

CCM wanaenda kuanguka tena kwa kuweka Katibu Mkuu mpya,mwenezi mpya na Mwenyekiti mpya.

Anguko la Safari hii litaiondoa CCM madarakani 2020.

CCM inaenda kuweka Mwenyekiti asiyekuwa na rekodi ya uongozi ndani ya chama inaenda kuweka Makamu Mwenyekiti,Katibu Mkuu na Mwenezi ambao sifa yao kuu NDIYO MZEE.

Huu ni wakati wa wapinzani kujiandaa kuchukua Ikulu 2020.
 

Tunasema tena :
Ukombozi wa Taifa hili hauto patikana chini ya hawa watu.

Ukombozi kamili unakuja mwaka 2020. Hata TB Joshua alikuja hapa kumpa taarifa hiyo Mh Lowassa.
 
Hata chama chao Kinawashinda kukiimarisha, wanang'ang'ania Madaraka ya Nchi miaka 50+ hakuna hata cha Kujivunia nchi hii.
 
Mkuu, unataka kutuambia kama chama hicho kimekufa ni kweli yule mbunge aliyesema nchi inaongozwa na mizuka atakuwa mkweli?
 
Back
Top Bottom