Tutulie kwanza....
Uislam maana yake ni TOTAL SUBMISSION TO THE WILL OF ALMIGHTY GOD.....
Ukisema uislam wa kushushwa Quran ulikuwepo kabla ya mtume SAW hapo utakuwa ni uongo wa kitoto....kwani kabla ya kuwa mtume SAW ,dunia haikuwa na QURAN.....
Ila.....
Manabii wote waliotoka kwa mwenyezi Mungu walihubiri NENO moja tu....
"Mwenyezi Mungu muumba mbingu na nchi ni mmoja na yeye pekee ndiye apasaye kuabudiwa kwa haki...."
Hiki kiko ndani ya TAURATI...
Hiki kiko ndani ya INJILI ya YESU...
Hitimisho:
Binafsi ninaamini wayahudi ,waislamu na wakristo wanaamini katika Mwenyezi Mungu mmoja aliyeumba MBINGU ,ARDHI NA VIUMBE WOTE....
YEYE hana mwanzo ,YEYE hana MWISHO....
Mengine ni MBWEMBWE tu za ubishani wa WABISHI KOKO ha ha ha ha
Hili swala halipaswi kujibiwa kwa hisia bali elimu iliyothabiti yakuweza kuchambua hiki ni sio na hiki ni kweli (sahihi) na hiki sio sahihi (uzushi).
Mimi pia sio mjuzi wa haya ila kwenye uislam wetu kuna shida moja bayana kuchanganywa na uongo, mbaya zaidi watu wa uongo wamekua na nguvu sana na wajuao ukweli wamekua wanyonge kusema ukwel kutoka na mambo mbali mbali, ntatoa mifano michache ya vichache navyo vifahamu vnavychangia uislam kulega na kuonekana una ubatilifu ndani yake tofauti na mtume wetu alvyotufundisha kutoka ndani ya Quran.
1. Siasa za aina zote; hii imepelekea kutokea kwa vita wanazodai ni jihad wakati kitabu na hadithi znaeleza wazi kuhusu ipi jihadi ya kweli na huku tukiambiwa imebaki jihadi ya sisi na nafsi zetu, ila unakuta kikundi cha watu fulan dhehebu fulan ndan ya dini fulan kwa faida zao fulani na kutokana na uwezo wao wanaanzsha chokochoko mpka vita ila infact binafsi hakuna jihadi ni siasa tu na hata ukija kwenye sheria za jihadi hakuna inayofatwa dini yakiislamu hairuhusu kabsa mtu kujitoa uhai (kudhulumu nafsi) kwa namna yoyote ile, sasa je anaejifunga bomu nakujilpua nakulipua wanawake, watoto, wafanyabiashara n.k hyo jihad kajfunza kwa mtume yupi na ni kipi umefanyiwa mpaka kuingia kwnye jihad? umekatazwa kuswali ama vip? Kuna vtu vinafanywa kufurahisha viongoz wa mataifa hii sana ipo afrika ata kama hcho ktu kinapngana na Allah na kikubwa hapa ni njaa ukipewa chochote kitu aanh basi kwisha unatafuta kahadith flan dhaifu kakuliptsha jambo lako, ama kasherehe flan hv kakupgia dili kuptia kivuli cha assalam alyekum ni huzuni
2. Watu kujarbu kupindisha nini quran na hadithi inasema na kutaka kuendana na utandawazi ili kupunguza ukali wa sheria; mfano mavazi wanawake wana namna wamelekezwa ila sahv kuna namna wanavaa inaleta picha hyo kama uislam unavyotaka ila infact hawako sawa unakuta mwanamke kapga kiushungi chake kipande, gauni ya body fit inayomchora body yake na make up ama mapambo mengi na manukato hadharan hyo haipo ila aslam alyekum nyng mashekhe wenyedhaman yakusikika wengu hawasemi hii haifai na haipo kwenye uislam wanabaki kusema afadhali, swala la equality uislam haupo hvyo ni kuna equity (degree of fairness) na hii athari yake n mbaya sana kwa watoto wakiume miaka ijayo maana tutatafuta haki zao nao kam miaka hii tunavyotafta za mtoto wa kike.
3. Matumizi mabaya ya vivuli vya dini; sahv kuna kitu watu wanaita masheikh sheik ananisomea sheikh anatoa majin sheikh hv na vile je ukija kwnye uislam kuna sehemu mtume alikua ana weka watu foleni kuwafanyia visomo? Kuwaandikia madude? Kuchoma udi? Kugawa majini? Kusafisha nyota?Hakuna ila mtu mwenye elimu kusimam kusema hzi n shirki n ngumu sana kwasababu anaogopa atipgwa ktu kzto na hii inachafua uislam mpka kufikia kuitwa dini ya wafuga majini , waganga wakienyeji infact hakuna kitu kama hcho ila tunaogopa kusemezana tu sasa inabid upgane jihadd yakuumia moyoni tu, sahiv kuna misikti wanasimama masheikh wanauza dawa za utajir sijui nn na nn, hao watu wachache wanaokuja kwa kasi wachafua sana, Allah atusamehe.
4. Waislamu weng kutoisoma dini vizur na kubak kuwa watu wa amini, inshaallah, takbir , naam nk bila ata kuelewa ni sahihi ama si sahihi; binafs swala la mtu kuoa anapga chini asilimia kubwa ya talka hzfat sharia ya dini kabsaaa kma dhumuni la talaka hii inachafua uislam nakuitwa watu wakuoa nakuacha kwasbabu mtu kasikia tu uktaka kumuacha mwanamke n talaka lkn hajui lengo na utaratbu sahihi wa talaka, kingne watoto wetu wakiislam kuonekana elimu ya dunia sio kipaumbele hasa kwa vijijin na mijini kuongoza kwa vijna wakiume na wakike wenye majina ya kiislam kuwa na tabia mbaya wizi, vigodoro, kutostaarabik nk lkn dini ina ukwel wake na maelekezo yake juu ya malezi kwnye kila ktu.
Kuna maswala mengi ila naona kama nachanganya mengne ntafafanua kwenye comment mtu analotaka kulijua kwa nlipowezeshwa.
Sujaweka uzito wa hadithi wala aya kwasabubu n jamii changamano hapa kuna ambao hatutaelewana ila kuna wajuzi zaidi wanaweza kazia kwa aya na adithi.
Rai yangu tuishi kwa mipaka ya kila mtu na anachokiabudu maana hizi mada hupelekea kuchfua amani kuna wakati sio jambo zuri kuzileta humu.
Samahani kwa yeyote andiko langu litakua mimemletea makwazo.