Kwanini mtu huogopa? Hasa kufa kwa nini?

Kwanini mtu huogopa? Hasa kufa kwa nini?

Kabla ya kuzaliwa nini kilifuata?

Kama hakuna.

Kwa nini unafikiri ukifa, kuna kinachofuata?

Ukifa hakuna kinachofuata kama ilivyokuwa kabla ya kuzaliwa. Hakuna kilichofuata.

Ukifa unaoza, Biashara imeisha.

This is what I was thinking, theres nothing to fear ni uongo kabisa..

You're just an accumulation of vibrational elements that shifts avatar bodies. Hakuna cha kuogopa kifo wala bibi yake na kifo.

So turudi square one, hii hofu tunawezaje kuifuta completely while we navigate this limited avatar
 
Nimeipata concept thanks for reminder..

So unataka kusema uncertainty is what causes it.. Periodt..? Na it's intentionally ingrained for survival?
Iko hivi Mkuu binadamu tuna uwezo wa kuwaza future, huu uwezo wa kuwaza ndio umetupa uwezo wa kujenga ustaarabu, lakini pia ndio uliotuletea huzuni ya kifo.

Hatujaijenga hii hofu kwa ajili ya ku-survive labda isipokuwa tumeijenga kwa sababu tumejipa uwezo mkubwa wa kufikiria sana, kadiri akili inavyokua, ndivyo hofu ya kifo inavyozidi kuwa kubwa pia.
 
Hofu ya kifo au kujilinda usife sio kwa binadamu pekee bali ni kwa viumbe vyote vilivyo hai.
Hali hii ya kujilinda ni msukumo wa nature ambao lengo ni ku maintain uhai wa hii dunia.
Mshana Jr ameelezea vizuri.
Watu wanaojiua kama kujinyonga na wao wanakuwa na hii hofu?

Nyuki dume akishamzalisha malkia anakufa, Je na yeye kama kiumbe anakuwa na hii hofu ya kifo?

Kuna wanyama wengi tu, kama Octopus 🐙 wanakufa baada ya sex, Je na wao wanakuwa na hofu na kifo?
 
Iko hivi Mkuu binadamu tuna uwezo wa kuwaza future, huu uwezo wa wa kuwaza ndio umetupa uwezo wa kujenga ustaarabu, lakini pia ndio uliotuletea huzuni ya kifo.

Hatujaijenga huu hofu kwa ajili ya ku-survive labda isipokuwa tumeijenga kwa sababu tumejipa uwezo mkubwa wa kufikiria sana, kadiri akili inavyokua, ndivyo hofu ya kifo inavyozidi kuwa kubwa pia.
No kidizain flani nakataa
Watu huongeza maarifa ili kutoa uncertainty and thus kupunguza hofu.

Ile point ya survival ina uzito kuzidi hii
 
This is what I was thinking, theres nothing to fear ni uongo kabisa..

You're just an accumulation of vibrational elements that shifts avatar bodies. Hakuna cha kuogopa kifo wala bibi yake na kifo.

So turudi square one, hii hofu tunawezaje kuifuta completely while we navigate this limited avatar
Kwanza wakati mtu unakufa wala huwezi kujua kwamba ndio unakufa.

Ni kama vile ukiwa unaishia usingizini wala huwezi kujua kwamba usingizi ndio unakupitia hivyo.

Wewe unashtukia tu, umeamka asubuhi lakini huwezi kujua ni muda gani exactly uliishia usingizini moja kwa moja.

Hofu kuhusu kifo sanasana imejengwa na hizi imani za kidini.

Masuala ya Jehanam ya moto ndio yanaleta hofu kwa watu.

Lakini wakati wa kufa wala hakuna anayejua kwamba hapa ndio nimekufa.
 
Kabla ya kuzaliwa nini kilifuata?

Kama hakuna.

Kwa nini unafikiri ukifa, kuna kinachofuata?

Ukifa hakuna kinachofuata kama ilivyokuwa kabla ya kuzaliwa. Hakuna kilichofuata.

Ukifa unaoza, Biashara imeisha.
Kwa wewe ni rahisi kuamini kuwa baada ya kifo hakuna kitu kinachofuata ili usihofie kile kisichojulikana ,yani unajaribu kufanya materialism kuwa dini yako mpya ili uiondoe existential anxiety uliyo nayo.
 
Ni mwanzo Tu lakini ikikufikia Hali Fulani kuwa ww ni wa kufa Tu huwezi kupona basi hofu hupotea...
 
Kwanza wakati mtu unakufa wala huwezi kujua kwamba ndio unakufa.

Ni kama vile ukiwa unaishia usingizini wala huwezi kujua kwamba usingizi ndio unakupitia hivyo.

Wewe unashtukia tu, umeamka asubuhi lakini huwezi kujua ni muda gani exactly uliishia usingizini moja kwa moja.

Hofu kuhusu kifo sanasana imejengwa na hizi imani za kidini.

Masuala ya Jehanam ya moto ndio yanaleta hofu kwa watu.

Lakini wakati wa kufa wala hakuna anayejua kwamba hapa ndio nimekufa.
usidanganye watu hakuna mtu aliehai anayejua mtu anahisi vipi wakati wa kufa ni kwasababu waliokufa hawawezi kurudi tena wakatuelezea
 
Kwanza wakati mtu unakufa wala huwezi kujua kwamba ndio unakufa.

Ni kama vile ukiwa unaishia usingizini wala huwezi kujua kwamba usingizi ndio unakupitia hivyo.

Wewe unashtukia tu, umeamka asubuhi lakini huwezi kujua ni muda gani exactly uliishia usingizini moja kwa moja.

Hofu kuhusu kifo sanasana imejengwa na hizi imani za kidini.

Masuala ya Jehanam ya moto ndio yanaleta hofu kwa watu.

Lakini wakati wa kufa wala hakuna anayejua kwamba hapa ndio nimekufa.
Unatumia analogy ya usingizi kuelezea kifo, yani umeshindwa kuona utofauti hapo?

Usingizi ni mchakato wa kibiolojia ndani ya mwili ulio hai, unapokuwa umelala, mwili wako bado unakuwa unafanya kazi, mapigo ya moyo yanaendelea kama kawaida, ubongo unaendelea na activity yake lakini kifo ni utengano wa mfumo mzima.

Ni makosa ya kifikra kulinganisha state of rest na cessation of existence, hauwezi kusema kifo ni kama usingizi kwa sababu kwenye usingizi kuna continuity ya maisha, wakati kwenye kifo, mtoa-ushuhuda ambaye ni wewe unatoweka kabisa.
 
Kwa wewe ni rahisi kuamini kuwa baada ya kifo hakuna kitu kinachofuata ili usihofie kile kisichojulikana ,
Kile kinachojulikana kipi?

Kithibitishe hapa.
yani unajaribu kufanya materialism kuwa dini yako mpya ili uiondoe existential anxiety uliyo nayo.
Moto ukizimika unaenda wapi?

Ukipuliza mshumaa🕯ukazima, moto unakuwa umezimika na kwenda wapi?

Maana unajiuliza mtu akifa anaenda wapi?

Kana kwamba binadamu ni "so special" anahitaji mahali pa kwenda akishakufa.
 
No kidizain flani nakataa
Watu huongeza maarifa ili kutoa uncertainty and thus kupunguza hofu.

Ile point ya survival ina uzito kuzidi hii
Kama unasema watu huongeza maarifa ili kutoa uncertainty basi hapa umekubali moja kwa moja kuwa uncertainty ndiyo chanzo cha hofu yenyewe.
 
Mimi naogopa tu yale maumivu ya kwenye mchakato wa kifo mfano ugonjwa wa maumivu makali ajali

Ila kama naweza kufa kwa amani mfano usingizini au nimekaa zangu sebuleni wala hakuna tabu 🥰
 
Kwa wewe ni rahisi kuamini kuwa baada ya kifo hakuna kitu kinachofuata ili usihofie kile kisichojulikana ,yani unajaribu kufanya materialism kuwa dini yako mpya ili uiondoe existential anxiety uliyo nayo.
Jamaa Ana point tena kubwa sana, yeye ame surpass the body and mind... Akadive into the metaphysical aspect kuwa before hajazaliwa hakuwepo na so akifa anarudi into That nothingness.. But hiyo hai negate existence ya hofu... Ambayo ni instinctual
 
Back
Top Bottom