Mhaya
JF-Expert Member
- Aug 20, 2023
- 1,658
- 4,866
Nimebahatika kufika Bagamoyo safi na salama kabisa, shukran za dhati ziende kwa Mungu Mkuu.
Mji wa Bagamoyo ni mji mzuri sana kimandhari, ukitizama mji wenyewe huko kando kando ya bahari ya Hindi. Nimefika Bagamoyo kwanza ni mji umepoa sana, sio mji wenye harakati kwa sisi wachakarikaji, nahisi hata mzunguko wa pesa ni mdogo sana, na maduka ni ya kuhesabu hesabu kwenye mitaa niliyobahatika kupita.
Kwenye upande wa chakula wanajitahidi sana, nimekula wali wenye bei ndogo na radha nzuri tofauti na wali wa usukumani. Watu wa Bagamoyo hawasemi Wali, bali wanasema ni Ubwabwa. Kila mtu utasikia nipate Ubwabwa, mimi wa kanda ya ziwa nimezoea neno wali.
Ubaya wa Bagamoyo, mziki unaanzia kwenye barabara za mitaani, barabara nyingi mtaani ni za vumbi zenye mabonde mabonde, mvua ikinyesha barabara zote zinajaa madimbwi ya maji. Yaani hakuna Water Drainage Systems mabararani.
Maeneo mengi hayana nyumba za kupangisha za maana zinazoendana na kodi. Nyumba nyingi ni za wakazi, na za kupangisha utakuta unakaa na mwenye nyumba hapo hapo. Kwa sisi tusiopenda kukaa na wenye nyumba kidogo ni mtihani.
Mji ni mzuri, japo waswahili kibao, ukitembea hatua chache kila baada ya nyumba unakuta watu wamekaa nje. Vijana wengi ni bodaboda, wazee wengi ni wakukaaa majumbani tu. Tofauti na mikoa kama mwanza unakuta mzee nae anachakalika.
Kwa kifupi mara ya mwisho kuja bagamoyo ilikuwa 2016, sasa nimerejea 2023 lakini sijaona mabadiliko yoyote ya kimaendeleo, kwa kifupi mji haukui. Stendi ya daladala iko vile vile. Miji mingi iko vilevile. Kwa sababu ni mji unaopakana na Dar es Salaam nilitegemea kuona maendeleo kwa sababu ni rahisi kuagiza bidhaa za ujenzi na mambo mengine ya kimaendeleo na mji ukakua.
Sijui hawa jamaa wanafeli wapi kwenye maendeleo, huu ni miongoni mwa miji mikongwe sana hapa Tanzania (Tanganyika) ila wilaya hii haina maendeleo na inazidiwa maendeleo na Wilaya za juzi juzi tu kama Chato, na wilaya nyingine zinazofanya vizuri kiuchumi.
Unaweza kuongezea experience yako kuhusiana na mji huu mkongwe, na pia unawashauri nini wageni wanaoingia mji huu ni kipi cha kuzingatia na kipi cha kukaa nacho chonjo, kipi cha kufanya na kipi cha kuacha kufanya ndani ya mji huu mkongwe toka enzi za utumwa.