Bagamoyo Real Estate Workshop Namba 1

Aliko Musa

Senior Member
Aug 25, 2018
156
240
Bagamoyo Real Estate Workshop Namba 1

Utangulizi wa programu.

Programu hii ya FURSA ZA ARDHI/MAJENGO (Real Estate Workshop) zimelenga kwenye mambo makuu matatu (3). Mambo yenyewe ni:

✓ Moja; kujenga uwezo kwa mwekezaji kutafuta taarifa, koneksheni, maarifa na uzoefu wa sehemu anapowekeza kabla ya kufanya maamuzi kuhusu uwekezaji wake.

✓ Mbili; kujenga uwezo wa kutathmini masoko ya ardhi na majengo. Hii ni baada ya kujenga ubobevu katika wilaya moja kwa miaka fulani wakati wa uwekezaji wake.

✓ Tatu; kutambua umuhimu wa kujenga timu bora ya wilaya unapowekeza.

Njia ya kujenga uwezo wa kutathmini soko la ardhi na majengo ni kufanya yafuatayo:

✓ Moja; kuwekeza katika wilaya moja kwa miaka fulani kwa kutumia njia moja au mbili tu bila kupoteza fokasi.

✓ Mbili; kutumia timu yako kujipatia taarifa, koneksheni na maarifa ipasavyo. Hii inatakiwa ifanyike bila kujali kiwango cha mafanikio uliyofikia kwenye uwekezaji wa ardhi na majengo.

Karibu tuangalie kwa ufupi kuhusu FURSA ZA ARDHI/MAJENGO wilayani Bagamoyo. Ninaamini mimi na wewe tunaweza kubadilishana taarifa/maarifa kwa ajili ya manufaa yetu sote. Karibu sana rafiki.

Historia ya wilaya ya Bagamoyo.

Wilaya ya Bagamoyo ni moja ya wilaya kongwe hapa Tanzania bara. Idadi ya wakazi wilayani Bayamoyo ni ya kawaida ukilinganisha na wilaya za Geita na Kahama.

Kutokana na utafiti uliofanyika na programu ya Umoja Na Mataifa Ya Makazi Ya Binadamu (United Nations Human Settlement Programme (UN HABITAT), Bagamoyo ilikuwa ni mji wa heshima katika historia ya nchi ya Tangayika miaka ya 1889 hadi 1891. Mwaka 1929 mji wa Bagamoyo ulichaguliwa hadhi ya kuwa mji. Mji ulipata nguvu zaidi ya hiyo kutokana na kukua kwa biashara ya utumwa na meno/bidhaa za mnyama Tembo.

Taasisi hiyo ilibainisha kwenye kitini chake kiitwacho Tanzania; Bagamoyo Urban Sector Profile cha mwaka 2009 kuwa Morogoro (karibu na mlima uluguru), Dar Es Salaam na Bagamoyo ni mji iliyochaguliwa kufanyika kwa programu yenye jina la D kwa D (Decentralization by devolution programme).

Hii ni programu ya kuhamisha baadhi ya nguvu za kiutawala, kazi, wajibu, na majukumu ya kisiasa kutoka serikali kuu kwenda serikali za mitaa.

Programu inashindwa kufikia ufanisi mkubwa kutokana na serikali kukosa mitaji fedha na baadhi ya viongozi kuweka udhibiti mkubwa kwenye serikali za mitaa.

Kitini kinaendelea kutushirikisha kuwa zaidi ya 65% ya wakazi wa wilaya ya Bagamoyo wanaishi kwenye makazi ambayo hayajapangiliwa (Unplanned settlements). Makazi ambayo hayajapangiliwa na mipango miji na vijiji kwa lugha nyingine tunaita mitaa ya changanyikeni.

Hii ina maana kuwa ni 35% ya wakazi wa wilaya ya Bagamoyo wanaoishi kwenye mitaa iliyopangiliwa. Hivyo nguvu ya mpangilio wa miundombinu na mali isiyohamishika ina athari ndogo kwenye mji huu wa Bagamoyo.

Kuzaliwa, Kukua, Kukomaa Na Kufa Kwa Miji.

Kama ambavyo nilikushirikisha hapo awali kuwa miji huzaliwa, hukua, hukomaa na kufa, mji wa Bagamoyo ulikuwa na nguvu sana kiutawala na kiuchumi. Baada ya kufa kwa biashara ya bidhaa za ndovu na biashara za utumwa, taratibu mji ukaanza kupoteza nguvu yake.

Hivyo kupelekea mji kukosa nguvu ya ukuaji wa thamani za ardhi/majengo katika wilaya ya Bagamoyo kwa kipindi hicho. Hebu nikukumbushe tena kwamba kuna nguvu 4 nne zinazoathiri mienendo ya thamani/bei ya ardhi na majengo.

Nguvu hizo ni:

✓ Nguvu ya kisiasa (political forces).

✓ Nguvu ya mpangilio wa miundombinu na mali zisizohamishika (Physical forces).

✓ Nguvu ya wakazi (idadi, kipato chako, tabia zao, na tamaduni zao).

✓ Nguvu ya kiuchumi (ukuaji wa biashara na uwekezaji).

Nguvu ambazo zitakupa matokeo chanya kwa miaka mingi zaidi bila kutegemea mabadiliko ya hali dunia ni mbili tu:

✓ Moja; Nguvu ya mpangilio wa miundombinu na mali zisizohamishika.

✓ Mbili; Nguvu ya wakazi wa eneo husika.

Ukichunguza vyema, utagundua mji wa Bagamoyo uliathiriwa zaidi na nguvu mbili; moja ni nguvu ya kiuchumi na ile ya kisiasa au kimamlaka kwa miaka hiyo. Idadi ya watu ilikuwa ni sababu iliyoleta matokeo chanya, lakini kwa sababu ilikuwa inachangiwa na wapitaji (watumwa, wachuuzi wa watumwa na wakoloni wenyewe) haikuweza kuleta matokeo ya muendelezo.

Hivyo basi, nguvu ya idadi ya watu isingeweza kuleta matokeo chanya kwa muendelezo kama ambavyo tunategemea. Hii ni kwa sababu ya aina ya waingiaji (immigrants) kutokea maeneo tofauti tofauti ya Tanganyika.

Hii tunaiona pia katika mkoa wa Kigoma, ambao umekuwa na historia ya kuwa na wageni kutoka Burundi. Wageni hao wanaweza kuwa na matokeo chanya ya muda mfupi tu na kuleta matokeo hasi endapo makazi yao yaliyopo Kigoma yataathiriwa.

Ni jambo muhimu sana kuangalia wahamiaji wana tabia gani na kua uwekezano kwa wao kuishi miaka mingapi na kipato chao kitakuwa shilingi ngapi. Pia, uzao wao utakuwa mkubwa au mdogo. Haya yatakusaidia sana kufanya aina ya uwekezaji wa ardhi na majengo kwenye eneo fulani.

Itaendelea...

Rafiki yako,

Aliko Musa.

Whatsapp; +255 752 413 711
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom