Malezi ni sifuri, hatufundishwi kuwajibika Angali wadogo. Kuwajibika kwetu ni msamiati Tu usio na maana...Malezi ndiyo Kila kitu, ukiangalia huo mfano wa Rwanda, wanyarwanda ambao nawafahamu mm ni wasafi halafu vitu viko kwenye mpangilio wenye unafuu kuliko Sisi, yaani kwenye standard za usafi wametuacha hata Kwa level ya mtu mmoja mmoja.
Hata upite na bunduki mtaani kutishia watupa taka bado Tu kuna watu watatupa.
nakumbuka miaka Fulani kule Tanga walikuwa na kampeni ya usafi inaitwa Kalembo day, yaani Hadi hiyo siku ifike ndo watu wanakimbizana kwenye usafi wakati ni Jambo linalotakiwa kufanywa Kwa Kila siku, njoo kwenye nyumba zetu ndo utajua Sisi ni mapimbi wenye miguu miwili nyumba ziko hovyo hovyo, mtu akiamka shuka hatandiki vizuri, shuka chafu, chumba hakifagiliwi, bukta na chupi zipo dirishani, vitana na mafuta yako uvunguni yaani Kila kitu hakipo mahali pale, nenda vyooni sasa hizo harufu na uchafu kwenye masink, sasa watu wa Aina hii watakuelewa kweli unapowaambia masuala ya usafi na mpangilio, tena mijini watu hutoa pesa za usafi lakini wapi watendaji wanakula buyu Tu wanapita kushoto.
Kuna jamii Hapa TZ ukiingia nyumba zao zinapendeza hata kama uchumi si mkubwa mfano Mabohora, hawa Jamaa Kila kitu huwa kinakaa sehemu Yake sasa ukiwa na jamii kama hii ni rahisi Sana kukuta mazingira safi, ww Angalia maeneo mengi tuliyojazana sisi waafrika weusi pako hovyo hovyo Tu, Malezi ni muhimu Sana.
Mtu kanunua bidhaa anakula anatupa Ganda au plastiki barabarani au unakuta anatupa dirishani wala hajali, mtu anakamua kamasi anajifutia na nguo Yake. Umaskini si Tatizo pekee Bali Malezi yetu mabovu, tunazaliwa ili kujaza dunia Tu.