Kwanini Migahawa ya Wakristo Tanzania haina chakula kizuri?

Njoo bukoba Baba upate chakula pale ELCT Hotel au Tea room nisijue mikoa mingine lkn ata uko bukoba kuna kolping hotel kashura hapo kuna chakula kizuri sana
 
Kuna ki restaurant hapa arusha kinaitwa mwambao kinamilikiwa na wazenji kuna pilau mbuzi haijawahi kutokea, hapa kesho Christmas nina mpango wa ku lunch pale
Ni pilau inayosifika zaidi hapa arusha
Watu wa pwani wanajua kupika sababu maeneo yao kuna spices nyingi na wamekuwa nazo wanafahamu kuzitumia vizuri
Hahahaha...pale "Mwambao" ndio mahali napoendaga kula Pilau Mbuzi

Ni wakali wa mapishi kwakweli.
 
Mimi ni Mkristo!

Katika kusafiri safiri kwangu mikoani, nimegundua migahawa mingi iliyopo kanda ambazo zina wakristo wengi kama Mwanza, Arusha, Mbeya, Kilimanjaro, Iringa n.k. huwa na chakula kibaya sana. Migahawa inayofanya vizuri mara nyingi huwa inamilikiwa na Mama Zena, Hamisa, Hadija, Aisha, Mpemba, n.k. Majina ambayo huwa yana uhusiano na dini ya Kiislamu. Mke wangu ni mpishi mzuri sana, labda kwa sasa alibadiri dini; lakini nasikia wanawake wa kikristo mapishi kwao ni taabu!

Kuna tatizo gani la upishi katika Jamii ya Kikristo Tanzania?
Kama unazungumzia vyakula vya kiswahili kama chai, pilao, biriani uko sawa ila kama unazungumzia vyakula kama nyama choma, michemsho, mitori nk umekosea sana.
Jielimishe zaidi maana usiangalie wahudumu kwani hujui jikoni yuko nani !!
 
Me nafikiri ni interest ya mtu dhidi ya kupika na malezi.
Kwa binti wa kiislamu mara nyingi huwa wanafundishwa kupika pindi wanapokuwa nyumbani na hata kama yupo bize na shule lazima hata wikiend asaidie kupika hata kama kuna msaidizi wa kaz tofauti na hao wengine
Then kama mtu ana interest ya kupika atajifunza tu regardless ni dini ipi
Sasa mara nyingi wakristo hawalelewi hivyo na wala kujifunza hawataki na interest hawana
Hii comment ni too general na sijui ulifanyia wapi hiyo research. Nakubaliana na aliye comment kwa habari ya ukanda na sio udini. Hayo malezi ulosema wanafanya wote na wote pia hawafanyi.
 
Mkuu ni malezi tuu sio elimu wala kukosa muda, kama huamini chukua binti wa kikristo mwenye degree na binti wa kiislam mwenye degree waambie wakupikie chakula au wape pesa kiasi sawa kwa matumizi ya home au kujipendezesha alafu urudi uniambie nani fundi.
Aisha au Zulfa atapika vizuri kuliko Janet au Scholar
 
Umekosea sana kuiweka ktk uislam na ukristo ingekaa kiukanda kungekuwa na mantiki, we mchukue mwanamke muislam wa shinyanga na mwanamke muislam wa tanga hlf wakupikie ndo utajua ishu sio dini ni eneo na tamaduni ya eneo husika
Na hata huo uzuri au sijui ktk chakula hutamkwa ubora ni kulingana na tamaduni za mtu husika, mfano kwa aliyekulia Pwani ugali wa kisukuma ni mbaya kwake na kinyume chake msukuma ndo hali na akila ni kwa shida sana ugali wa kipwani. Kwahyo uzuri au ubaya wa mapishi ni kutokana na yale uliyoyazoea wewe, mmasai ugali anaweka chumvi na ndo mzuri kwake.
 
Nakujibu kama ifuatavyo:
Mimi ni Mkristo!
Mkristo wapi-acha unafiki

Katika kusafiri safiri kwangu mikoani, nimegundua migahawa mingi iliyopo kanda ambazo zina wakristo wengi kama Mwanza, Arusha, Mbeya, Kilimanjaro, Iringa n.k. huwa na chakula kibaya sana.
Nchini mwetu hatuna maeneo ya wakristo wengi au waislamu wengi, huo upuuzi peleka Nigeria, Kenya au India. Isitoshe uliwahesabu ukajua idadi zao katika kila mkoa?

Migahawa inayofanya vizuri mara nyingi huwa inamilikiwa na Mama Zena, Hamisa, Hadija, Aisha, Mpemba, n.k. Majina ambayo huwa yana uhusiano na dini ya Kiislamu. Mke wangu ni mpishi mzuri sana, labda kwa sasa alibadiri dini; lakini nasikia wanawake wa kikristo mapishi kwao ni taabu!
Poor reasoning-yaani wamiliki wa mgahawa-tena unao kutana nao wewe kuitwa Zena, Hamisi, Hadija, Aisha, Mpemba tayari usha generalize waislamu ni bora kwenye mapishi kuliko wakristo.
-pia ni kuulize anaye pika ni mmliki (yani bosi) au vijakazi ambao ndani yake kuna mixture ya dini mbali mbali wakiwemo hao waislamu na akina Recho, Mary, Jack, Angel, Jennifer, Annet.
-na unaposema mapishi be specific ni mapishi ya chakula gani, kuna aina chungu nzima ya vyakula, kuna vyenye asili ya india, uarabuni, uchagani, usukumani, kwa wahaya, ulaya na marekani.

Huna lolote zaidi ya kutaka mpambano wa kidini, stupid.
 
Mke wangu alikuwa christian, alipobadili dini tu na kumwoa anapika Chakula kitamu hadi bac, hata mm najiuliza cjui Kwa nn sasa anajua kupika kuliko alipokuwa christian
 
Vipi mtori bomba pia unapatina hapo mwambao? Vipi na mchembe wao ukoje?
Mtori bomba sijawahi kuuona pale.

Pale watu wengi wakienda wanaagiza pilau mbuzi, pia bites zao na juice halisi ni nzuri sana.
 
Hakuna suala la udini hapa, ni utamaduni zaidi wa eneo na eneo....na wengi wanaotoka mikoa ya Pwani ni/wanatumia majina yanayoshabihiana na ya kiarabu au kiislamu kama unavyosema wewe hapo juu...ndio maana unagundua haraka umiliki wa Mgahawa husika.

Mapishi yanayotumia viungo viungo ni utamaduni wa Kihindi/kiarabu na ndio wameuambukiza maeneo ya mwambao.

Wewe hujasikia hata stori za eti kuwa Tanga hata maji ya kuoga hutiwa iliki?

Utarajie nini kutoka kwa Mama Manka anayeshindia ndizi mshare au ndizi ng'ombe Januari to December.....au Mama yeyoo ambae mumewe wanashindia nyama januari to December.

Sasa umpelekee Mama Swai binzari, iliki, mdalasini, tangawizi, swaumu, atie kwenye nini...kibulu? au kitalolo?
 
Mtori bomba sijawahi kuuona pale.

Pale watu wengi wakienda wanaagiza pilau mbuzi, pia bites zao na juice halisi ni nzuri sana.
Vyakula vya kimwambao hivyo msukuma lazima aende shule hapo, ila wakiweka ligi ya kupika michembe na magugulu then mteja akiwa ni msukuma hiyo Hotel ya mwambao na uzanzibari wao watatoka nduki.
 
Mboga mboga na maviungo ya kukarangiza watu pwan si.haba

But kuna wachaga hawa watu wanapika kitimoto moja flan amazing,wanachanganya na.mchicha na.ndizi inakuwa balaa

Kitimoto bora na supu ya mbuzi bora tz inapatikana kilimanjaro

Kuna wasukuma bwana,supu ya samaki wakuchanganyie karanga na ndizi ebhana eeeh..vila park kesho mwanza kinahappan

Kuna wanyakyusa.kongoro na ndizi na mbalaga lazima ujilambe

Ila watu wapwan ni balaaa,idara zao waweza kunywa mboga debe,wali wakuchanganyie,nyegere,karoti nk

Kudadek njaa imeniuma gaflaaa
 
Bila shaka mumeo unamlisha notes zinazonukia harufu nzuuuuuri ya wino.

Kusoma kwako kukusaidie kujitambua ili kuyamudu mazingira ya sasa na yajayo.
Mazingira yajayo ni kujua kuwa ipo siku utakuwa mke, na huna budi kutimiza majukumu yako ikiwa ni pamoja na kumpikia mumeo. Vipo vitu vingi vinavyoongeza upendo, hata hili pia lina mantiki.
Hujachelewa, chukua hatua.
Wakati unaandika ujinga huu, kesho usiwe wa kwanza kusema 'oooh mbona nafasi wanapewa Edith na Rachel tu, kwani kina Mwantumu na Zena sio wanawake'?

Maisha ni maandalizi. Mtu akiniambia wanawake wa Kikristo hawajui kupika labda nitamuuliza chakula gani. Kitu kama biriani na vitumbua si asili ya watu wa bara na hata mimi ukinipikia biriani utamichefua. Nikiwa na akili zangu timamu, too much spices ni uchafuzi wa tumbo langu. Mke wangu anajua kupika, kuliko hao mama ntilie walioorodheshwa hapa.

Kitimoto mnaturostiaga nyie?

Labda huko uswahilini mnakoishi waweza kuona jambo, wacha nikusaidie. Wakati mama Flora anamhimiza binti yake aende shule maneno yake hayatafanana na ya mama Aisha akimhimiza Aisha asugue sufuria 'ling'ae'.

Mama Flora: Hivi wewe, ukishafeli utaishi maisha gani hapa mjini kama sio kutegemea wanaume wakulishe wewe? Nani anataka golikipa siku hizi?

Mama Aisha: Wewe endeleaga hivyo hivyo na mkichwa wako mzito, tui la kwanza linakuwaga hivyo...we hata humalizi mwaka mumeo atakuolea mke mwingine, hebu niondokee hapa

MAISHA NI VIPAUMBELE.
 
Wakati unaandika ujinga huu, kesho usiwe wa kwanza kusema 'oooh mbona nafasi wanapewa Edith na Rachel tu, kwani kina Mwantumu na Zena sio wanawake'?

Maisha ni maandalizi. Mtu akiniambia wanawake wa Kikristo hawajui kupika labda nitamuuliza chakula gani. Kitu kama biriani na vitumbua si asili ya watu wa bara na hata mimi ukinipikia biriani utamichefua. Nikiwa na akili zangu timamu, too much spices ni uchafuzi wa tumbo langu. Mke wangu anajua kupika, kuliko hao mama ntilie walioorodheshwa hapa.

Kitimoto mnaturostiaga nyie?

Labda huko uswahilini mnakoishi waweza kuona jambo, wacha nikusaidie. Wakati mama Flora anamhimiza binti yake aende shule maneno yake hayatafanana na ya mama Aisha akimhimiza Aisha asugue sufuria 'ling'ae'.

Mama Flora: Hivi wewe, ukishafeli utaishi maisha gani hapa mjini kama sio kutegemea wanaume wakulishe wewe? Nani anataka golikipa siku hizi?

Mama Aisha: Wewe endeleaga hivyo hivyo na mkichwa wako mzito, tui la kwanza linakuwaga hivyo...we hata humalizi mwaka mumeo atakuolea mke mwingine, hebu niondokee hapa

MAISHA NI VIPAUMBELE.

Ok
 
Kila watu wana asili yao kwenye mapishi.Kuna wanaokaangiza sana na kujua namna ya kutumia viungo na Kuna wanochemsha zaidi kuliko kukaangiza.Dini isihushwe hapo kwakua italeta shida.
 
hiyo pilau itakuwa mandi hiyo.. bismat rice hatariiiii

kuna mgahawa unaitwa almaida pale lumumba karibu na ccm ni hatari...

dr ramadhan dau lilikuwa chimbo lake pale anapiga mandi mbuzi... sahani 8000 ila unaona kabisa hujaibiwa jinsi pilau lilivyo tamu



Kuna ki restaurant hapa arusha kinaitwa mwambao kinamilikiwa na wazenji kuna pilau mbuzi haijawahi kutokea, hapa kesho Christmas nina mpango wa ku lunch pale
Ni pilau inayosifika zaidi hapa arusha
Watu wa pwani wanajua kupika sababu maeneo yao kuna spices nyingi na wamekuwa nazo wanafahamu kuzitumia vizuri
 
Back
Top Bottom