Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 21,339
- 51,876
Kwema Wakuu!
Kuna watu watabisha Kwa ubishi wao tuu lakini kimsingi na kitaalumuna unapozungumzia mapishi Kwa nchi yetu basi hapo utakuwa unazungumzia ukanda wa Pwani.
Kama unaishi maisha ya kawaida Kurudi ufukara na hujawahi kuishi Maeneo ya Pwani na hapa nazungumzia DAR es salaam, Pwani yenyewe, Tanga, Lindi, Mtwara, na Zanzibar basi kaa ukijua hujawahi Kula chakula kitamu.
Na Kama Mwanamke hajawahi fika na kuishi Pwani basi ni hakika hajui Kupika chakula kitamu.
Wanawake WA Pwani moja ya silaha zao nzito za Masafa mafupi na marefu mbali na kukata mauno pia Upishi WA chakula kitamu wameshindikana.
Kuanzia Chai, Andazi, chapati, wali, pilau, biriani, Makande, Makange, Ndizo, maharage, kunde, mtori, n.k. vyakula hivyo Kama hujawahi kupikiwa na Mwanamke wa Pwani basi jua hujui utamu wake.
Ukiona mtu yeyote anajua Kupika chakula Kwa nchi hii ya TANZANIA, jua Ujuzi huo ameupatia baada ya kuishi aidha ni DAR es salaam, au Pwani, au Tanga.
Kupika Kwa wanawake WA Pwani ni Sanaa, ni ufahari, ni Jadi Yao. Vikorombwezo bila ya bezo, wakiimba Kwa Dezo na michezo ya Ngoma chakula chenyewe kinageuka chocolate.
Mwanamke wa Pwani hahitaji kwenda kujifunza Hotelia ATI ili awe MPISHI mzuri, mapishi matamu kwao ni silaha.
Wengine chakula kitamu ni mpaka siku ya Harusi au sikukuu hasa huko Mikoani.
Ila ukanda wa Pwani kila siku chakula kitamu bila kujali bajeti ni ndogo kiasi gani.
Taikon Leo nipo kwenye Migahawa ya Waswahili huku, kuna watu wanapika bhana, utamu mpaka unafumba macho.
Ooh! Kalogwa! Sijui limbwata! Hivi chakula kitamu unafikiri mchezo!
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam