Kwanini Migahawa ya Wakristo Tanzania haina chakula kizuri?

Aisee chakula cha Mwambao ni kitamu balaa sijui wanapika wakiwa uchi? Au pale Cafe la Aziz. Unaweza ukaondoa ratiba ya kula nyumbani.
fundisheni weke zenu kupika mimi mama hawezi kunilisha matap tap maana mimi ni fundi kwenye kupika viungo unafaidi mautam.
 
Inategemea na aina ya chakula.

Wewe kama wa pwani umezoea biriani pilau wali chai yenye hiliki nk. Ni mapishi yenye vionjo vya mila za kiarabu. Pwani hawajui kupika Ugali wala samaki wa kuchemsha.

Bukoba ni wataalamu wa ndizi maharage na samaki.

Moshi nyama na ndizi. Arusha nyama choma.

Mbeya ndizi wali maharage. Mwanza na mara ni ugali samaki na nyama.

Hivylo mapishi yanaendana na makuzi au mila za mahala husika.

Huwezi kuta mkurya anajua kupika ndizi au wali kuliko mzaramo.

Pia kuna aina ya viungo kama nazi karanga mafuta na maziwa vinatumika katika mikoa tofauti kuunga kitoweo.

Mnyamwezi atakuungia karanga kwenye tembele. Pwani wataweka nazi. Mkurya ataweka maziwa. Kigoma mawese nk.

Hivyo wewe kama mkeo ni wa nazi lazima ukisafiri uone tofauti.

Kama kuna mashindano ya upishi basi wanyamwezi wanaongoza
 
Kuna ki restaurant hapa arusha kinaitwa mwambao kinamilikiwa na wazenji kuna pilau mbuzi haijawahi kutokea, hapa kesho Christmas nina mpango wa ku lunch pale
Ni pilau inayosifika zaidi hapa arusha
Watu wa pwani wanajua kupika sababu maeneo yao kuna spices nyingi na wamekuwa nazo wanafahamu kuzitumia vizuri
Mnaposifia mtu kujua kipika taja na aina ya chakula anachopika.

Waamnie hao wapemba wako wakupikie ugali sato mchemsho kama watawafikia wakerewe.
 
Pale, Turiani Morogoro kuna Mangi mmoja wanamuita Masawe, aisee jamaa kwa kupika Supu ya mbuzi kali ni balaa... Sijui anaweka nini hiyo Supu yake maana ni so delicious...
Wanaoshabikia mapishi ya pwani watuambie ni mapishi ya kitu gani.

Samaki choma mzuri nenda mwanza

Nyama choma nenda Arusha

Kitimoto nenda Moshi

Supu ya mbuzi muone mchaga. Ya samaki mwone mkerewe siyo mmasai.
 
Bila shaka mumeo unamlisha notes zinazonukia harufu nzuuuuuri ya wino.

Kusoma kwako kukusaidie kujitambua ili kuyamudu mazingira ya sasa na yajayo.
Mazingira yajayo ni kujua kuwa ipo siku utakuwa mke, na huna budi kutimiza majukumu yako ikiwa ni pamoja na kumpikia mumeo. Vipo vitu vingi vinavyoongeza upendo, hata hili pia lina mantiki.
Hujachelewa, chukua hatua.
Hakuna, kuzalishwa zalishwa je?
Labda ukinizalisha wewe
 
fundisheni weke zenu kupika mimi mama hawezi kunilisha matap tap maana mimi ni fundi kwenye kupika viungo unafaidi mautam.
Wake zetu wanafahamu kupika aina ya vyakula vya kwetu. Kwenye mapishi ya mlenda nani hodari kati ya mnyamwezi na mpemba?

Acheni kudharau watu wengine


Mleta mada unapenda udini na ukanda hadi kwenye mapishi. Umeleta taarifa za uongo.

Uzuri wa mapishi inategemea na asili ya anayepika na anayekula. Mzoea nazi samli haiwezi
 
Mimi ni Mkristo!

Katika kusafiri safiri kwangu mikoani, nimegundua migahawa mingi iliyopo kanda ambazo zina wakristo wengi kama Mwanza, Arusha, Mbeya, Kilimanjaro, Iringa n.k. huwa na chakula kibaya sana. Migahawa inayofanya vizuri mara nyingi huwa inamilikiwa na Mama Zena, Hamisa, Hadija, Aisha, Mpemba, n.k. Majina ambayo huwa yana uhusiano na dini ya Kiislamu. Mke wangu ni mpishi mzuri sana, labda kwa sasa alibadiri dini; lakini nasikia wanawake wa kikristo mapishi kwao ni taabu!

Kuna tatizo gani la upishi katika Jamii ya Kikristo Tanzania?
Kwa kuwa hatujasoma kazi za ofisi tunawaachia nyie sisi tunapika
FaizaFoxy Ritz
 
Mimi ni Mkristo!

Katika kusafiri safiri kwangu mikoani, nimegundua migahawa mingi iliyopo kanda ambazo zina wakristo wengi kama Mwanza, Arusha, Mbeya, Kilimanjaro, Iringa n.k. huwa na chakula kibaya sana. Migahawa inayofanya vizuri mara nyingi huwa inamilikiwa na Mama Zena, Hamisa, Hadija, Aisha, Mpemba, n.k. Majina ambayo huwa yana uhusiano na dini ya Kiislamu. Mke wangu ni mpishi mzuri sana, labda kwa sasa alibadiri dini; lakini nasikia wanawake wa kikristo mapishi kwao ni taabu!

Kuna tatizo gani la upishi katika Jamii ya Kikristo Tanzania?
Sio kila mmiliki mgahawa muislam anajua kupika ila Kuna jamii ya kutokea mahali Fulani, Ni mafundi hata mkristo akikulia mazingira Yao anakua mkali wa mahanjumati. Upishi pamoja Na kuwa ni utamaduni lakini pia ni elimu Kama elimu nyingine hivyo huweza kufundishika katika jamii nyingine yoyote
 
Hatuwezi kulingana kila kitu,ndiomaana ukitaka kujua mapishi kwenu huko ila elimu nzuri kwa WAKRISTO, wakati mnafundishana kupika wenzenu wako darasani wakiingiza vitu vichwani
 
29 Reactions
Reply
Back
Top Bottom