Azizi Mussa
JF-Expert Member
- May 9, 2012
- 9,172
- 7,428
Hivi ni kigezo gani kilitumika kuamua Mbunge alipwe maslahi ya uhakika halafu diwani afanye kazi kwa kujitolea?
Kama hoja ni kwamba uwezo ni mdogo 'chakula', kwa mila za kitanzania chakula kikiwa kidogo, wakubwa huachia wadogo. Sasa mbona kama kwenye hili liko kinyume nyume?
Kama hoja ni kuhudumia wanyonge, nadhani diwani ni mnyonge kuliko mbunge. Lakini pia diwani yuko karibu zaidi na wanyonge kuliko mbunge? au vipi?
Kama uzito wa kazi, diwani anafanya kazi muhimu sawa na mbunge tu,lakini pengine kwenye mazingira magumu kuliko mbunge au sivyo?
Ushauri wangu,
Kwa kuwa kama taifa tunataka kujenga jamii yenye haki na usawa 'Fair and just society';-
1. Maslahi ya wabunge yapunguzwe na fedha inayookolewa madiwani walipwe mishahara kiasi flani. Kwa kufanya hivyo kutakuwa na fairness ya hali ya juu. Pia watu hawatakimbilia ubunge kibiashara bali kiutumishi.
2. Iruhusiwe kwamba kwa mtu mwenye vyanzo vingine vya mapato na yuko tayari kufanya kazi ya ubunge kwa kujitolea bila kulipwa anaruhusiwa pia mradi aainishe kwamba yeye ni mbunge wa kujitolea na hatadai gharama yoyote kutoka kwa yoyote (kama madiwani wanaweza kujitolea kwa nini ishindikane wabunge kujitolea angalau hata wachache?). Hii itasaidia kupata wawakilishi wazalendo ambao 'motive' yao ni kuishirikisha jamii kupiga hatua na sio kutafuta maslahi binafsi.
Mwisho, wazo hili linaweza lisiwe 'popular' ila ni la kweli, muhimu na likifanyiwa kazi litasaidia kutatua changamoto nyingi n kuleta manufaaa mtambuka.