Kwanini Mbunge asijitolee diwani akalipwa mshahara? Kama chakula kidogo anaachiwa mdogo

Azizi Mussa

Verified Member
May 9, 2012
8,789
2,000
Hivi ni kigezo gani kilitumika kuamua Mbunge alipwe maslahi ya uhakika halafu diwani afanye kazi kwa kujitolea?

Kama hoja ni kwamba uwezo ni mdogo 'chakula', kwa mila za kitanzania chakula kikiwa kidogo, wakubwa huachia wadogo. Sasa mbona kama kwenye hili liko kinyume nyume?

Kama hoja ni kuhudumia wanyonge, nadhani diwani ni mnyonge kuliko mbunge. Lakini pia diwani yuko karibu zaidi na wanyonge kuliko mbunge? au vipi?

Kama uzito wa kazi, diwani anafanya kazi muhimu sawa na mbunge tu,lakini pengine kwenye mazingira magumu kuliko mbunge au sivyo?

Ushauri wangu,

Kwa kuwa kama taifa tunataka kujenga jamii yenye haki na usawa 'Fair and just society';-

1. Maslahi ya wabunge yapunguzwe na fedha inayookolewa madiwani walipwe mishahara kiasi flani. Kwa kufanya hivyo kutakuwa na fairness ya hali ya juu. Pia watu hawatakimbilia ubunge kibiashara bali kiutumishi.

2. Iruhusiwe kwamba kwa mtu mwenye vyanzo vingine vya mapato na yuko tayari kufanya kazi ya ubunge kwa kujitolea bila kulipwa anaruhusiwa pia mradi aainishe kwamba yeye ni mbunge wa kujitolea na hatadai gharama yoyote kutoka kwa yoyote (kama madiwani wanaweza kujitolea kwa nini ishindikane wabunge kujitolea angalau hata wachache?). Hii itasaidia kupata wawakilishi wazalendo ambao 'motive' yao ni kuishirikisha jamii kupiga hatua na sio kutafuta maslahi binafsi.

Mwisho, wazo hili linaweza lisiwe 'popular' ila ni la kweli, muhimu na likifanyiwa kazi litasaidia kutatua changamoto nyingi n kuleta manufaaa mtambuka.
 
Nowonmai

JF-Expert Member
Jan 15, 2019
605
1,000
Wote wasilipwe mshahara.

Walipwe tu posho ya vikao.

Wawakilishi wa wananchi hawapaswi kuwa makupe.

Lakini hata makupe wengine kama malaya wanalipwa tu pale wanapotoa huduma.

Tupige vita ukupe na unyonyaji wa aina zote.

Naunga mkono hoja.
 
denooJ

JF-Expert Member
Mar 31, 2020
5,650
2,000
Hilo wazo lingepelekwa bungeni likafanyiwe kazi, ni ajabu sana kuona watu wanaofanya kazi kwenye mazingira magumu tena bila ya vitendea kazi vya uhakika (usafiri) mwisho wa miaka yao mitano ya utumishi hawalipwi chochote, huku wale wanaopata viyoyozi kwenye V8 muda wote huo wakiondoka na milioni 200, tena haraka bila kusubiri!.

Hii nchi ina maajabu mengi sana.
 
Samcezar

JF-Expert Member
May 18, 2014
8,573

Ni milioni 360+ sio 200
 
Kashaulo

JF-Expert Member
Jun 14, 2019
2,772
2,000
Hilo wazo lingepelekwa bungeni likafanyiwe kazi, ni ajabu sana kuona watu wanaofanya kazi kwenye mazingira magumu tena bila ya vitendea kazi vya uhakika (usafiri) mwisho wa miaka yao mitano ya utumishi hawalipwi chochote, huku wale wanaopata viyoyozi kwenye V8 muda wote huo wakiondoka na milioni 200, tena haraka bila kusubiri!.

Hii nchi ina maajabu mengi sana.

Huko bungeni si ndo walipo wabunge!
 
Wise E

JF-Expert Member
May 10, 2019
760
1,000
wewe uwajui wabunge wa nchi hii wapo kwa ajili ya matumbo yao hawana mapenzi na sisi watu wanaangalia ugali wa familia zao hakuna mbunge anaetetea maslahi yako kwa dhati watu wanafuata utajili tu huko
 
Lupweko

JF-Expert Member
Mar 26, 2009
14,584
2,000
Hivi ni kigezo gani kilitumika kuamua Mbunge alipwe maslahi ya uhakika halafu diwani afanye kazi kwa kujitolea?
Mbunge anatunga sheria, diwani hatungi chochote. Mbunge yupo kwenye mhimili mmojawapo, diwani yupo yupo tu
 
Kim Jong Jr

JF-Expert Member
Mar 15, 2014
9,456

Sheria inatungwa na wizara ya sheria bunge ni kwenda kupitisha tu acha uongo ...

Unazijua By laws za halmashauri zinatungwa na Nani ?

Hujui Baraza la madiwani linafanya kazi sawa na bunge na hata muundo ni sawa
 
Babati

JF-Expert Member
Aug 7, 2014
44,574
2,000
Hivi ni kigezo gani kilitumika kuamua Mbunge alipwe maslahi ya uhakika halafu diwani afanye kazi kwa kujitolea?

Kama hoja ni kwamba uwezo ni mdogo 'chakula', kwa mila za kitanzania chakula kikiwa kidogo, wakubwa huachia wadogo. Sasa mbona kama kwenye hili liko kinyume nyume?

Kama hoja ni kuhudumia wanyonge, nadhani diwani ni mnyonge kuliko mbunge. Lakini pia diwani yuko karibu zaidi na wanyonge kuliko mbunge? au vipi?

Kama uzito wa kazi, diwani anafanya kazi muhimu sawa na mbunge tu,lakini pengine kwenye mazingira magumu kuliko mbunge au sivyo?

Ushauri wangu,

Kwa kuwa kama taifa tunataka kujenga jamii yenye haki na usawa 'Fair and just society';-

1. Maslahi ya wabunge yapunguzwe na fedha inayookolewa madiwani walipwe mishahara kiasi flani. Kwa kufanya hivyo kutakuwa na fairness ya hali ya juu. Pia watu hawatakimbilia ubunge kibiashara bali kiutumishi.

2. Iruhusiwe kwamba kwa mtu mwenye vyanzo vingine vya mapato na yuko tayari kufanya kazi ya ubunge kwa kujitolea bila kulipwa anaruhusiwa pia mradi aainishe kwamba yeye ni mbunge wa kujitolea na hatadai gharama yoyote kutoka kwa yoyote (kama madiwani wanaweza kujitolea kwa nini ishindikane wabunge kujitolea angalau hata wachache?). Hii itasaidia kupata wawakilishi wazalendo ambao 'motive' yao ni kuishirikisha jamii kupiga hatua na sio kutafuta maslahi binafsi.

Mwisho, wazo hili linaweza lisiwe 'popular' ila ni la kweli, muhimu na likifanyiwa kazi litasaidia kutatua changamoto nyingi n kuleta manufaaa mtambuka.
Hao wabunge lazima walipwe vzr sababu ndiyo anategemea wabadili katiba wampe kutawala zaidi/vipindi vingi
 
Lupweko

JF-Expert Member
Mar 26, 2009
14,584
2,000
Sheria inatungwa na wizara ya sheria bunge ni kwenda kupitisha tu acha uongo ...
Mimi darasani nilifundishwa kuwa mojawapo ya kazi za Bunge ni kutunga sheria (sio kupitisha sheria). Kuhusu Wizara, labda unachanganya kati ya muswada na sheria. Lakini napokea kama maoni kutoka kwako kwamba sheria huwa inatungwa na wizara, ila nachanganya na za kwangu
 
Kim Jong Jr

JF-Expert Member
Mar 15, 2014
9,456
2,000
Mimi darasani nilifundishwa kuwa mojawapo ya kazi za Bunge ni kutunga sheria (sio kupitisha sheria). Kuhusu Wizara, labda unachanganya kati ya muswada na sheria. Lakini napokea kama maoni kutoka kwako kwamba sheria huwa inatungwa na wizara, ila nachanganya na za kwangu
Unaelewa maana ya kutunga ??? Haya tuseme wizara inapeleka muswaada Bungeni , huko Bungeni wanaitungaje sheria ? ... Unajua Bill inakuaje ili iwe law ...

Acha kukariri madesa yako ya Nyambari Nyangwine Sheria hutungwa na Wizara ya sheria hayo unayoelezwa shuleni ni utopolo tu.
 
Kim Jong Jr

JF-Expert Member
Mar 15, 2014
9,456
2,000
Mbunge anatunga sheria, diwani hatungi chochote. Mbunge yupo kwenye mhimili mmojawapo, diwani yupo yupo tu
Wewe ulisoma shule ya kata , Hakuna mtumishi asiekuwa chini ya muhimili wowote. Unaposema madiwani Hawana muhimili naona jinsi gani elimu ya uraia (civics) imevyokupita kushoto.
 
denooJ

JF-Expert Member
Mar 31, 2020
5,650
2,000
Huko bungeni si ndo walipo wabunge!
Yes, na kwasababu ya kujali matumbo yao hawawezi kukubali hilo jambo litokee, mpaka yule anayewapa hizo pesa atakapoamua kuwapunguzia, japo sidhani kama hilo litatokea.
 
AGITATOR

JF-Expert Member
Apr 7, 2019
1,693
2,000
wewe uwajui wabunge wa nchi hii wapo kwa ajili ya matumbo yao hawana mapenzi na sisi watu wanaangalia ugali wa familia zao hakuna mbunge anaetetea maslahi yako kwa dhati watu wanafuata utajili tu huko
Ukweli mchungu huu.
 
AGITATOR

JF-Expert Member
Apr 7, 2019
1,693
2,000
Ha
Hivi ni kigezo gani kilitumika kuamua Mbunge alipwe maslahi ya uhakika halafu diwani afanye kazi kwa kujitolea?

Kama hoja ni kwamba uwezo ni mdogo 'chakula', kwa mila za kitanzania chakula kikiwa kidogo, wakubwa huachia wadogo. Sasa mbona kama kwenye hili liko kinyume nyume?

Kama hoja ni kuhudumia wanyonge, nadhani diwani ni mnyonge kuliko mbunge. Lakini pia diwani yuko karibu zaidi na wanyonge kuliko mbunge? au vipi?

Kama uzito wa kazi, diwani anafanya kazi muhimu sawa na mbunge tu,lakini pengine kwenye mazingira magumu kuliko mbunge au sivyo?

Ushauri wangu,

Kwa kuwa kama taifa tunataka kujenga jamii yenye haki na usawa 'Fair and just society';-

1. Maslahi ya wabunge yapunguzwe na fedha inayookolewa madiwani walipwe mishahara kiasi flani. Kwa kufanya hivyo kutakuwa na fairness ya hali ya juu. Pia watu hawatakimbilia ubunge kibiashara bali kiutumishi.

2. Iruhusiwe kwamba kwa mtu mwenye vyanzo vingine vya mapato na yuko tayari kufanya kazi ya ubunge kwa kujitolea bila kulipwa anaruhusiwa pia mradi aainishe kwamba yeye ni mbunge wa kujitolea na hatadai gharama yoyote kutoka kwa yoyote (kama madiwani wanaweza kujitolea kwa nini ishindikane wabunge kujitolea angalau hata wachache?). Hii itasaidia kupata wawakilishi wazalendo ambao 'motive' yao ni kuishirikisha jamii kupiga hatua na sio kutafuta maslahi binafsi.

Mwisho, wazo hili linaweza lisiwe 'popular' ila ni la kweli, muhimu na likifanyiwa kazi litasaidia kutatua changamoto nyingi n kuleta manufaaa mtambuka.
Ha ha mkuu taratibu, unataka watia nia warudishe makabrasha nini??
 
Lupweko

JF-Expert Member
Mar 26, 2009
14,584
2,000
Wewe ulisoma shule ya kata , Hakuna mtumishi asiekuwa chini ya muhimili wowote. Unaposema madiwani Hawana muhimili naona jinsi gani elimu ya uraia (civics) imevyokupita kushoto.
Taja mhimili diwani anaofanyia kazi za siku kwa siku
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom