Kwanini Mbeya ni jiji? My Detailed Explanation

Kwanini Mbeya ni jiji? My Detailed Explanation

Mh. Magufuli (Hayati) ndiye aliyeongoza maamuzi hayo. Nyaraka zipo. Pia utekekezaji wake unaweza kuona ktk taarifa mbalimbali e.g matokeo ya mtihani inayotolewa Kwa mfumo wa Halmashauri na masuala mengine ya kiutawala. Awali kabla ya March 2021 Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam ilijumuisha Manispaa zote za Dar.
 
Screenshot_20260630-195827_1.jpg
 
View attachment 3599442Moja ya maswali ambayo watu wengi wanauliza mara kwa mara hapa jukwaani ni kwa nini Mbeya ni jiji. Wengine wanasema kuwa hata miji kama Iringa, Moshi na Morogoro ingefaa kuitwa jiji kuliko Mbeya.
View attachment 3599465 Ukiangalia sababu kubwa inayofanya watu kuleta comparison kama hizi utagundua wengi wao wanaangalia maghorofa kuliko factors za kufanya sehemu kuwa jiji. Leo hii akitokea tajiri akajenga maghorofa kumi na tano katika mji wa Lindi na kuwapa masikini waishi bure, baadhi ya watu wakiangalia picha za maghorofa hayo wataanza kudai Lindi inafaa kuwa jiji. Wanasahau kuwa jiji ni combination ya factors nyingi.
View attachment 3599443
Wengine wanatoa sababu kama nyumba za matope, slums, barabara mbovu, mpangilio mbovu wa mji na vumbi kama sababu halisi za kunyima Mbeya hadhi ya kuwa jiji. Lakini madai haya kwa asilimia kubwa yanapuuzia sababu halisi zinazofanya Mbeya iwe na hadhi ya jiji. Ukiniuliza mimi, nitakuambia ni kweli Mbeya ina barabara mbovu na mpangilio wa hovyo sana. Lakini je, hizi ni sababu za kufanya Mbeya lisiwe jiji? Hapana, sababu hizi zinafanya Mbeya kuwa jiji lenye barabara mbovu, au jiji lenye mpangilio wa hovyo na si kuondoa hadhi ya jiji moja kwa moja.
View attachment 3599444
Nini maana ya jiji?
“Jiji ni mji mkubwa sana ulioendelea kiviwanda, kiuchumi na kijamii wenye idadi kubwa ya watu na hadhi maalumu kisheria au kiutawala. Mara nyingi linakuwa kitovu cha utawala kama vile kuwa makao makuu ya mkoa au nchi”
Hakuna vigezo vya dunia nzima vinavyotumika kuclassify majiji, mara nyingi hutegemea vigezo vya nchi husika, na hapa ndio confusion kubwa inatokea. Hata hivyo kuna sifa za msingi ambavyo majiji huwa navyo in common ambavyo kwa asilimia kubwa Mbeya ina sifa hizi zote.

Hapa nitataja sifa mbalimbali zinatofautisha Mbeya na miji ya kawaida kama Morogoro, Moshi na Iringa.

1.Mbeya ina mapato makubwa sana na biashara nyingi
View attachment 3599445
Jiji la Mbeya ndio makao makuu ya mkoa wa Mbeya lakini pia ni sehemu inayokusanya mapato makubwa sana. Jiji la Mbeya always lipo top 5 ya miji yenye mapato makubwa zaidi Tanzania. Maana yake ni jiji linalojitosheleza sana kimapato kuliko miji mingi Tanzania kwa hiyo haiwezi kufanana na Iringa au Moshi. Jiji la Mbeya lina very big magnetic effect, watu kutoka maeneo kama Songwe, Makambako, Sumbawanga, Iringa, Njombe nk wanafanya movements kubwa sana za kuingia na kutoka ndani ya jiji la Mbeya kwa ajili ya biashara.
View attachment 3599446
Jiji la Mbeya ni centre ya biashara kwa ukanda huu. Pia ni gateway ya kuingilia nchi jirani ya Zambia, kitu kilichofanya Mbeya kuwa very busy hadi barabara ya TANZAM imeharibika kutokana na shughuli hizi na bado inaonekana haitoshi, kwa sasa inapanuliwa kuwa njia nne (Japo kwa speed ya konokono)

2. Mbeya ina idadi kubwa sana ya watu
View attachment 3599449
Jiji la Mbeya lina idadi kubwa sana ya watu, takribani watu laki 6 kwa eneo la jiji pekee. Hii inarudi moja kwa moja kwenye maana ya jiji. Siku zote sifa ya jiji lolote lile ni kuwa na watu wengi na kwa Tanzania watu alaki 6 katika mji mmoja ni wengi sana. Ndio sababu Mbeya always iko busy na biashara nyingi, ina population kubwa

3. Jiji la Mbeya ni kubwa sana kieneo
View attachment 3599447
Moja ya sifa inayotofautisha Mbeya na miji kama Iringa au Mtwara sio tu population bali size ya mji pia. Jiji la Mbeya lina ukubwa wa takribani 250km2 . Size hii ni moja ya tatu ya jiji la Nairobi, meaning makazi ya watu yamesambaa kwa eneo kubwa sana. Eneo hili tayari ni kubwa sana kutosha sehemu kuwa jiji. Fun fact, watu wengi wanaishi Mbeya miaka na miaka bila kukanyaga maeneo mengine ya jiji hilo au bila hata kujua kama yanaexist. Mfano, ninajua wakazi wengi wa Uyole hawapajui Maziwa au St Marcus ambako ni 20km kutoka wanapoishi lakini ni ndani ya jiji moja.


4. Jiji la Mbeya limeendelea sana kwenye huduma nyingi za kijamii
View attachment 3599452
Jiji la Mbeya liko mbali sana kwenye huduma nyingi za kijamii, kitu ambacho wengi wanakiouuzia wanapoanza kui judge Mbeya kuwa ni jiji au la.

Kwanza tukianza na shule. Jiji la Mbeya lina shule nyingi na zimezagaa karibia kila kona ya jiji kuanzia shule za serikali hadi za private, shule za primary hadi high school, za day hadi za bweni ikiwemo shule famous ya wasichana “St Francis Secondary School” na shule kongwe kama “Iyunga Technical Secondary School”
View attachment 3599448
Kama shule si big deal basi angazia vyuo vinavyopatikana ndani ya jiji la Mbeya, kuanzia vya kati hadi vikuu ngazi ya Diploma hadi PHD. Mbeya ndio jiji la pili kwa kuwa na vyuo vingi nchini Tanzania, inazidiwa na Dar es Salaam pekee. Mfano wa vyuo vinavyopatikana Mbeya ni
  • Mbeya University of Science and Technology (MUST)
  • University of Dar es Salaam, Mbeya branch (MCHAS)
  • Catholic University of Mbeya (CuoM)
  • College of Business and Education, Mbeya branch (CBE)
  • Tanzania Institute of Accountancy, Mbeya branch (TIA)
  • Mzumbe University, Mbeya branch (MU)
  • Teofilo Kisanji University (TEKU)
  • Southern Highlands College of Health and Allied Sciences
  • Agricultural Research Institute, Uyole
  • Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania
  • St John College of Health Science
  • K’s Royal College of Health and Allied Sciences
  • Mbeya Polytechnic College nk

Hivi vuo vyote zaidi ya 10 vipo ndani ya jiji la Mbeya na vyuo kama MUST na MCHAS ni among the best in Tanzania. Ukitazama kwa makini utagundua Mbeya ina vyuo vya kila aina kuanzia Uhandisi, biashara, Afya, Kilimo, sanaa nk

Tukija kwenye hospitali, kuanzia za serikali mpaka za private zimezagaa kila sehemu hapa Mbeya. Mfano wa hospitali za Mbeya ni
  • Meta Maternity Hospital, (Biggest maternity hospital in Tanzania)
  • K’s Hospital Mbeya
  • Maranatha Hospital
  • Mbeya Surgical Clinic
  • Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mbeya
  • UWATA HOSPITAL, IVUMWE MBEYA
  • UHAI Health Care nk
View attachment 3599437View attachment 3599438View attachment 3599441

Mbeya kuna masoko mengi ikiwemo soko kubwa la Mwanjelwa, Kuna stendi za mabasi mbili, Nanenane na Stendi Kuu na pia stendi mpya inajengwa pale Old Airport.
View attachment 3599457
Umeme na maji Mbeya uko available muda mwingi kuliko miji mingi Tanzania. Tena kwa sekta hii Mbeya ipo vizuri kuliko hata Dar. Ni nadra sana kusikia umeme umekatika Mbeya. Wanakata umeme lakini si mara nyingi na hawakawii kurudisha.

5. Mbeya ina viwanda vingi
Moja ya sifa inayotofautisha Mbeya na miji mingi ya kawaida Tanzania ni pamoja na viwanda vingi au makao makuu ya baadhi ya viwanda. Jiji la Mbeya lina hadi eneo lililotengwa kwa ajili ya viwanda “Iyunga Industrial Area” kuna viwanda vya Pepsi na Mirinda, Cocacola, TBL, tiles, magodoro, kuprocess kahawa, kiwanda cha madawa msd na vingine vingi
Mbeya iko busy sana kiuchumi, inaingiza na kutoa mizigo mingi sana kwenda mikoa mingine na nchi jirani. Isitoshe Mbeya ina hadi Bandari Kavu kutokana na shughuli za kiuchumi zilivyo nyingi

Now sisemi kuwa changamoto za Mbeya si za kweli. Changamoto zipo nyingi na asilimia kubwa ni kwa sababu ya uzembe wa serikali na hazifanyi Mbeya kutokuwa jiji. Barabara nyingi za Mbeya ni mbovu, bado zina mashimo, hakuna streetlights, mpangomji ni hovyo kabisa, vumbi kali pembezoni mwa barabara ya TANZAM kutokana na kuchelewa kupanua barabara hiyo, bado kuna uhaba wa mitaro na iliyokuwepo mingi imejaa mchanga na slums ni nyingi sana.
Licha ya serikali kuiacha Mbeya nyuma kwa miaka mingi kwa kutoipa miradi mingi inayostahili Mbeya bado imebaki kuwa kitovu cha uchumi Nyanda za Juu Kusini na watu hawajastop kujenge jiji lao. Mbeya inakua kwa kasi sana. Kila siku neighbourhoods mpya zinaibuka, watu wanafungua biashara, wanajenga nyumba nzuri, mji unakua. Ni miundombinu na mpangomji ndio vinaangusha jiji la Mbeya
View attachment 3599453View attachment 3599455View attachment 3599456
Kutokana na Mbeya kuwa na nguvu kubwa sana kiuchumi, solution ya matatizo yake cha kwanza ni kuunda serikali za majimbo. Hii itawezesha mapato makubwa ya Mbeya kuweza kuboresha hali ya jiji la Mbeya na sio miji mingine na Mbeya itakuwa mbali sana kimiundombinu
Kwa sasa serikali inaona Mbeya kama tu just another town in Tanzania. Hawaichukulii serious enough ukilinganisha na potential ya jiji hili lakini siku Mbeya ikiweza kujitawala kama jimbo itafika mbali sana.
View attachment 3599458View attachment 3599459View attachment 3599460View attachment 3599461View attachment 3599462View attachment 3599463View attachment 3599464
View attachment 3599451View attachment 3599454
Aiseee picha zote hizo umenikumbusha sehemu niliyosoma O level... Mitaa ya Mbeya day..... Kabla sijaondoka bongo ..... Daaah Ubarikiwe sana
 
Sawa, ila musijisifie mbeya ni kubaya sana munafosi Kulinganisha kijiji chenu na Tanga, Arusha, mwanza.

Tanga ya bandari na miradi mikubwa ya mafuta na Saruji kaeni kwa kutulia nyie ndio washika mkia
 
Sawa, ila musijisifie mbeya ni kubaya sana munafosi Kulinganisha kijiji chenu na Tanga, Arusha, mwanza.

Tanga ya bandari na miradi mikubwa ya mafuta na Saruji kaeni kwa kutulia nyie ndio washika mkia
Mtu wa Tanga unapata ujasiri wa kulinganisha Mbeya na Tanga
Inachekesha sana
 
Mtu wa Tanga unapata ujasiri wa kulinganisha Mbeya na Tanga
Inachekesha sana
Unayechekesha ni wewe Me nakusahauri njoo tanga, kuna michongo endelea na ubishi wako sasa. Tanga ya bandari, Miradi ya mafuta. Ipo mbali sana fanya safari ya kwenda tanga nakushauri kisha uje ulete mrejesho tanga ilikuwa imelala sikatai ila kwa huu muda mfupi imenyanyuka vibaya mno
 
Sawa, ila musijisifie mbeya ni kubaya sana munafosi Kulinganisha kijiji chenu na Tanga, Arusha, mwanza.

Tanga ya bandari na miradi mikubwa ya mafuta na Saruji kaeni kwa kutulia nyie ndio washika mkia
Hii ni nje ya mada. Umeona nani akisifia kuwa Mbeya ni kuzuri kuliko Tanga? Kama kuna mtu umebishana naye amekukera nenda kamalizane nae huko sio unaleta makasiriko kwenye mada za watu wengine. Haya maneno yako hakuna mahali nimeyataja kwenye thread kijana
 
Hii ni nje ya mada. Umeona nani akisifia kuwa Mbeya ni kuzuri kuliko Tanga? Kama kuna mtu umebishana naye amekukera nenda kamalizane nae huko sio unaleta makasiriko kwenye mada za watu wengine. Haya maneno yako hakuna mahali nimeyataja kwenye thread kijana
Nawewe nenda kapeleke kero kwa madiwani wako kama hutaki tuchangie
 
Nawewe nenda kapeleke kero kwa madiwani wako kama hutaki tuchangie
Halafu wakazi wengi wa Mbeya wanajua jiji lao lina changamoto nyingi ndio maana unaona hata kwenye mitandao ya kijamii wanaandaa content za vumbi, au jinsi uswazi ulivyotapakaa. Kama kuna watu wanafananisha Mbeya na Tanga basi ni wachache sana na mmojawapo (sijui ni nani) ndio huyo aliyekukera, aidha umebishana na chawa wa CCM au blind patriot wa Mbeya ambaye ameridhika na hali duni ya jiji sasahivi. But honestly wakazi wengi wa Mbeya wanajua kuhusu changamoto za Mbeya na jinsi jiji lilivyo nyuma kimiundombinu na kimpangilio, mara ngapi umeona thread humu wakazi wa Mbeya wakilalamika ukifananisha na idadi ya thread za kulinganisha Mbeya na Tanga? Thread za malalamiko dhidi ya Mbeya ni nyingi kuliko thread za kufananisha Mbeya na Tanga
 
Unayechekesha ni wewe Me nakusahauri njoo tanga, kuna michongo endelea na ubishi wako sasa. Tanga ya bandari, Miradi ya mafuta. Ipo mbali sana fanya safari ya kwenda tanga nakushauri kisha uje ulete mrejesho tanga ilikuwa imelala sikatai ila kwa huu muda mfupi imenyanyuka vibaya mno
Imenyanyuka sehemu gani Mimi nilikuwa Tanga juzi
 
Imenyanyuka sehemu gani Mimi nilikuwa Tanga juzi
Bandari, reli vyote vinafanya kazi hukuliona hilo, kwa majuzi hapa walitoa taarifa bandari ya tanga na kupitia TRA walikusanya billion 443 nadhani mwaka huu, Mradi wa Chongoleani Eacop umeibadilisha sana tanga na sahivi mradi unaelekea ukingoni ajira nyingi sana zimepatikana kwa wazawa na watanzania. Hayo machache tu nitakuletea mafanikio ya jumla ya bandari uone utoafauti
 
Imenyanyuka sehemu gani Mimi nilikuwa Tanga juzi
Bandari kavu zimeongezeka idadi ya magari yanayoingia tanga city ni mengi yakija kwa shughuli za bandari hawa wote wanalala Wanatumia wanakunywa, wanapata huduma nyengine wanachangia mzunguko wa hela, Rwanda sasa hivi rasmi inachukua mafuta kupitia bandari ya Tanga, yapo makampuni mengi ya forodha yamefika 400 yanajishusisha na shughuli za bandari hawa wote wanamaofisi Wamepangisha wanalipa kodi, Wameajiri
 
Bandari, reli vyote vinafanya kazi hukuliona hilo, kwa majuzi hapa walitoa taarifa bandari ya tanga na kupitia TRA walikusanya billion 443 nadhani mwaka huu, Mradi wa Chongoleani Eacop umeibadilisha sana tanga na sahivi mradi unaelekea ukingoni ajira nyingi sana zimepatikana kwa wazawa na watanzania. Hayo machache tu nitakuletea mafanikio ya jumla ya bandari uone utoafauti
Tunafurahi kuona Tanga inaendelea kwa kasi. Kama Tanga inakua kwa kasi ipasavyo then tunataka mikoa yote Tanzania including Mbeya iwe kama Tanga. Kila mkoa unapaswa kuendelea kwa kasi Tanzania na kama Tanga imefanikiwa hilo basi ni jambo la heri
 
Tunafurahi kuona Tanga inaendelea kwa kasi. Kama Tanga inakua kwa kasi ipasavyo then tunataka mikoa yote Tanzania including Mbeya iwe kama Tanga. Kila mkoa unapaswa kuendelea kwa kasi Tanzania na kama Tanga imefanikiwa hilo basi ni jambo la heri
Kwa takwimu rasmi za hivi karibuni, Bandari ya Tanga imefikia takribani wafanyakazi 17,000 wa kutwa (casual workers) kwa mwezi.

Kabla ya maboresho: takribani 6,000 wafanyakazi wa kutwa.
Baada ya maboresho: wameongezeka hadi 17,000 kwa mwezi.

Ajira za kudumu zimeongezeka kutoka karibu 200 hadi 344.

Taarifa nyingine ya TPA imetaja takribani 17,871 ajira za wenyeji zilizotokana na shughuli za bandari.


Muhimu: ongezeko la mizigo, magari, mafuta na upanuzi wa magati 3, idadi hii inaweza kuongezeka zaidi. TPA yenyewe inasema miradi ya maendeleo ya bandari itazalisha ajira mpya.
 
Kwa mtazamo wangu huu ndio mtiririko wa ma jiji tanzania

Dar Es Salaam
Mwanza
Arusha
Dodoma
Tanga
Mbeya
 
Ccm wanaihujumu sana mbeya sijui mliwakosea nin jiji kama kijiji miundo mbinu mibovu
 
Umejitahidi sana mkuu, umeandika kwa facts pamoja na weakness zake hasa katika miundombinu.

-serikali ijenge barabara za mitaani kiwango cha rami.
-mitaro ya maji taka ijengwe .
. Ila mbeya kuna vumbi balaha linatimuka kama jiji lipo jangwa la sahara 😃😃😃
 
Kichaka cha GDP asee, ila hata Kijiji kikubwa kikubwa lazima kichangie pato kubwa 🤣
 
Back
Top Bottom