Kwanini Marekani ameshindwa kuimaliza Iran haraka?

Kwakweli Iran imeonesha uwezo mkubwa ambao hata mimi shabiki wake sikuwa nategemea.

Tumwimbie Trump kidogo...

Mbaraka Mwinshehe - Jogoo la Shamba

🔹🔹🔹🔹🔹🔹🔹🔹🔹

*Hilo oooh
Ulijidai wewe mbabe sana
Leo umepigwa na kijana mdogo
Aibu imekupata
Kiko wapi sasa
Ulichokua ukujidai nacho?
Leo ungepambana na mimi kaka
Kilema ungekipata
🔹🔹🔹🔹🔹🔹🔹🔹🔹*

*Utampiga nani we?
Kwanza utoto bado haujakutoka
Wewe uliona wapi jogoo la shamba
Linawika mjini?
Utampiga nani we?
Kwanza ukini bado haujakutoka
Wewe uliona wapi jogoo la shamba
Linawika mjini?
🔹🔹🔹🔹🔹🔹🔹🔹🔹*

Ewe ngebe na majivuno yako

*Yamekwisha sasa heshima iko wapi?
Ulipotoka shamba kuingia mjini*

*Mimi nimekuona huwezi kunitisha
Ukiingia mikogo na kudharau wenzio*

Leo umefundishwa adabu na heshima

Ewe ngebe na majivuno yako


*Yamekwisha sasa heshima iko wapi?
Ulipotoka shamba kuingia mjini*

*Mimi nimekuona huwezi kunitisha
Ukiingia mikogo na kudharau wenzio*

*Leo umefundishwa adabu na heshima
🔹🔹🔹🔹🔹🔹🔹🔹🔹*

Ewe ngebe na majivuno yako

Yamekwisha sasa heshima iko wapi?
 
Haya mabazazi yapoyapo kama vile yamekatwa vichwa
 
Mkuu mosad na CIA ni binadamu kama ww nao wanaweza kufanya makosa,kwani Marekani alipo enda kuivamia Vietnam wakashindwa vibaya sana hiyo CIA haikuwepo.
Walipo fanya operation nchini Somalia ikafeli ikaishia wanajeshi wa Marekani kuuliwa na kuburuzwa barabarani na walio nusulika kukimbia CIA haikuwepo?
 
Mkuu samahani naomba unisaidie kujua ni wapi huko ambako Australia kasaidia kuzamisha manowari za marekani?
Richard Meirdhurst, a British Investigative Journalist juzi usiku kasema manowari ya Marekani iliyosaidia katika kulipua manowari ya Iran iliyotokea India ilikuwa na wanajeshi wa Australia. Do you understand the magnitude of these allegations???​
 
The same Delta-Force that took-out Maduro failed to even establish a foothold in Mogadishu.

War is fickle my friend...
​
 
Richard Meirdhurst, a British Investigative Journalist juzi usiku kasema manowari ya Marekani iliyosaidia katika kulipua manowari ya Iran iliyotokea India ilikuwa na wanajeshi wa Australia. Do you understand the magnitude of these allegations???​
Mkuu sio kwa ubaya Ila hiki umeandika ni uongo. Lakini tupeane benefit of doubt. Naomba uweke hiyo taarifa ya huyo Richard meirdhurst
 
Mkuu pro US & Israel ni ngumu kuelewa ndo maana hata Iran kukitokea hata natural disasters kama earthquake nk bado watakuambia imefanywa na majajusi wa Israel na US
 
Iran ingekuwa karibu na Marekani maana yake ungekuwepo urahisi wa Marekani kuishambulia. Huo urahisi haupo ndio maana Marekani inasafiri maelfu ya kilomita, ila Iran inashindwa kuifuata Marekani kwenye ardhi yake.

Drones na makombora kadhaa vingepiga miji ya Marekani ila Iran ingeshindwa. Kupiga chenga mbili tatu hakuzuii wewe kufungwa.

Marekani imeenda na Israel ndio, Iran nayo itafute kwa kwenda nae haijakatazwa. Hezbollah, Houthi, Hamas, Syria, Russia waiunge mkono ilikuwa nao bega kwa bega.
 
Usichokijua UK na USA walishawahi kumsandia IRQ kwa nguvu zote aweze kuangusha utawala wa IRAN ujua nini kilitokea IRAN ndo super power wa Middle East hiyo itabaki kua ivyo na hii vita USA hatachomoa soon na kuomba kukaa meza moja ni IRAN
 
Josif Broz Tito hakuungwa mkono na US, ila aliachwa na mambo yake bila kuingiliwa. Ikumbukwe kuwa Tito alikuwa na form yake mwenyewe ya communism ambayo iliitwa Titoism, ilikuwa haifungamani na upande wowote (hata Communists wenzake) bali ilikuwa ya kitaifa tu kwa ajili ya Yugoslavia.

Ndio maana Tito alikuwa kwenye Non Aligned Movement kama kiongozi, na alikuwa na ugomvi mkubwa sana na Stalin ila waliheshimiana kwa kuogopana.
Tito hakuwa na tabia ya kulisha Titoism kwa nchi nyingine hivyo domino effect haikumhusu.
 
Lakini pia hilo wenda lingeipa urahisi pia Iran kuwadhuru wamarekani tofauti na sasa ambapo wako mbali.
Nadhani unataka kuja na hoja ya kwamba Marekani ingekuwa imepakana na Iran mashambulizi yake dhidi ya Iran yangekuwa rahisi lakini kumbuka kuwa hata sasa kambi zote za Marekani zilizo izunguka Iran zote amezikimbia amerazimika kushambulia kutoka mbali.
 
Kalamu Nguruvi3 zitto junior nk njoo mteme madini vijana wenu tupate elimu
Ahsante kwa mwaliko, mkuu 'Kinkunti El Pendedo', kwenye mjadala makini kama huu, lakini naomba kutoa udhuru, juu ya ushiriki wangu kwa sababu nizijuazo mwenyewe.

Kwa uchache tu ni hivi:
Jamaa wakishapata silaha mpya, au mbinu za kivita mpya, wanatafuta sehemu ya kufanyia majaribio. Kwa haraka haraka hilo ndilo ninaloweza kueleza kuhusu vita hii.

Pili: ikitokea kwamba mtafaruku huu utatusaidia waTanzania kushughulika na balaa letu tulilonalo hapa sisi wenyewe, huo utakuwa msaada mkubwa sana kwetu.

Matumaini yangu makubwa juu ya vita hiyo ni kuwa itatusaidia kupambana na hawa mashetani wetu hapa.

Hayo ndiyo machache kati ya mengi sana niliyo nayo kwa sasa ninayoweza kuyaweka wazi hapa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…