Kwanini Marekani ameshindwa kuimaliza Iran haraka?

Muda huwa ni mwalimu mzuri sana.

Nakumbuka mabazazi na madunya wa humu ndani mnamo tarehe 24 February 2022 siku ambayo Urusi alivamia Ukraine walinitafuta na kunisimanga sana. Wengine walidiriki hadi kukashifu taaluma yangu. Walishangaa kwamba kwanini Urusi ameshindwa kuivamia Ukraine na kuimaliza kwa haraka ilhali anajiita taifa kubwa (Super-Power). Niliwaambia vijana wa humu ndani kwamba Urusi alifanya makosa kuvamia jirani yake na kuna mambo alikosea, lakini kusema kwamba NATO+EU wataiangusha ni jambo lisilowezekana. Mataifa makubwa huwa yanafanya makosa pia (Political Blunders)

Mpaka 2026, Urusi na Ukraine wanapigana, huku Ukraine wakiwa wameumizwa zaidi. Urusi anatumia fedha nyingi sana kwenye vita na usalama, jambo ambalo siku vita ikiisha litazua matatizo makubwa mno kwasababu watu wengi watakosa ajira ambazo wanazifanya sasa. Pia kuna mambo kadha wa kadha. Sasa huu ni utangulizi tu:

Naomba niwaulize ninyi vijana wa humu ndani, kwanini Marekani (The Only Global Super-Power) ameshindwa kulimaliza taifa la Iran ndani ya wiki kama alivyofanya Afghanistani au Venezuela ??? Fahamuni tu kwamba hivi vita hapigani Marekani peke yake bali anasaidiwa na Israeli na washirika wengine kama Australia ambao imejulikana hivi karibuni kwamba walisaidia kuzamisha manowari za Iran. Hapo kuna Saudi Arabia, Jordan, Qatar, Bahrain, UAE, Azerbaijan na Mgambo wa kikurdi (kurdish Militia).

Donald J Trump alisema ni siku nne tu baada ya Ayatollah kulambishwa mchanga basi, Iran ingekuwa kaputi. Ila sasa yametokea tofauti. Marekani kweli kawatandika Iran, lakini nao wamemtandika vibaya mno. Mara ya mwisho kambi za kijeshi za Marekani zimelipuliwa hivi ilikuwa ni mwaka 1941 kule Pearl Harbour ambapo Japan aliua zaidi ya wanajeshi 2000. Jambo la kushangaza kulikuwa na silaha za ulinzi za kisasa kabisa kwenye hizo kambi kama THAAD na PATRIOT ambazo zilikuwa na mfumo bora kabisa wa rada duniani ambao umelipuliwa.

Mahoteli ambayo walikuwa wanakaa MAJASUSI na WANAJESHI wa Marekani yamelipuliwa. Mpaka sasa maswali ni mawili tu: Aidha Iran alikuwa amejipanga sana AU kuna mtu anamsaidia maana siyo jambo rahisi kufanya haya ambayo Iran amekuwa akifanya hasa kwenye kufanya mashambulio ya ulengaji bila kukosea (Precision Attack) ambayo hutegemea kwa sehemu kubwa mifumo ya satellite. Israeli nako yamewakuta, sehemu muhimu za kiusalama zinalipuliwa. Utapinga, utanuna, utabisha na kuleta hasara ila hii ndiyo hali ilivyo.

SASA IRAN ANAPAMBANAJE: Mwaka 2018 nakumbuka kuna uzi wangu nilifurumushiwa matusi na mabazazi na madunya wa humu ndani, nilioandika kuhusu dhana ya ASYMETRIC WARFARE. Dhana hii inafanya kazi pale ambapo taifa dogo au kikundi kidogo kinapambana na taifa kubwa. Lengo siyo kutaka kupambana CONVENTIONAL WARFARE, ila ni kumsababishia maumivu makubwa yule aliye mkubwa kiasi cha kufanya akimbie. Mfano halisi, ni USSR vs Mujahedeen au USA vs Vietcong.

Iran hana AIRFORCE kama USA na ISRAEL. Iran hana NAVY kama USA na ISRAEL. Iran alichokiamua ni kutengeneza FORMIDABLE ROCKET AND DRONE FORCE, ambalo lina uwezo wa kisasa kabisa kushambulia taifa lolote lile hapa duniani. Jambo ambalo wengi hatulifahamu ni kwamba Iran mbali na udhaifu wao mwingi, walianza kupambana na Marekani tokea mwaka 1979, na wameshuhudia USA akishambulia wenzake kama Iraq, Afghanistan, Libya na Venezuela. Unadhani ni wajinga ???

MADHARA ENDAPO VITA HAITAISHA MAPEMA:

Mosi
, The Aura of American Invincibility has been shattered before the world. Zile propaganda za kusema hakuna wa kumgusa Marekani hazipo tena. Iran katuonesha kwamba Marekani na Israel wanagusika. Hebu sasa fikiria, endapo Uchina ataamua kuvamia Taiwani, nani anaamini kabisa kwamba kambi za Marekani zilizopo South-Korea, Philippines, Japan na Guam zitakuwa salama, kama tu kambi kubwa za Marekani barani Asia zimelipuliwa juzi na jana na Iran, taifa ambalo halina nguvu kama Uchina. Kiukweli, Marekani alizichanga karata vibaya na yanamtokea puani.

Pili, Urusi atapata nguvu kubwa kutokana na bei ya mafuta kupanda. Saudi Arabia, UAE, Oman, Qatar na Bahrain wanaogopa kupitisha mafuta Mfereji wa Hormuz, ambao kwa siku mapipa milioni 17 yanapita. Vita ikiendelea hivi na Iran akafanikiwa kufunga kabisa mfereji, basi mafuta ya Ulaya na Asia itabidi yapatikane Urusi ambako kuna vikwazo. Juzi Vladmir Putin kasema anafikiria kusitisha kabisa kuuza gesi Ulaya. Sasa USA na EU watabakiwa na maamuzi kama haya: Ondoa vikwazo ili tupate nishati kutoka Urusi. Bahati mbaya wakiondoa vikwazo Ukraine ndiyo kwaheri.

Tatu, Urusi atapenda kulipiza alichofanyiwa Ukraine. Hii ndiyo tabia kuu ya Urusi. Niguse-Ninuke. Marekani akitingwa kule Iran, basi lazima atapunguza kuangalia Ukraine. Sasa itabidi silaha zote zinazozalishwa zienda Persian Gulf (Ghuba ya Uajemi) siyo Ukraine. Urusi na Uchina wanaweza kuigeuza Iran, VIETNAM 2 endepo Marekani akiendelea hivi bila kuomba msamaha. Bahati mbaya sana kwa alichokifanya Donald Trump, Marekani ikirudi nyuma kama kipindi cha Twelve Days War mwaka 2024, basi ndiyo mwisho wa siasa za MAGA na Trump, na anaweza kufungwa kwasababu ameanzisha vita bila kibali cha Bunge.

Nne, mpaka sasa SECURITY DIPLOMACY ya Marekani imekufa. Ameingia makubaliano ya ulinzi na Saudi Arabia mwaka 1971, na mataifa kama UAE, Qatar na Bahrain kwamba wakitumia Dollar kuuza mafuta basi atawalinda. Bahati mbaya wanapigwa na Iran, wanaomba kuuziwa silaha na msaada wa kijeshi lakini bado hawajapata, kipaumbele chake ni Israel na kambi zake. Hii ndiyo vita kubwa ya kipropaganda ambayo Marekani hawezi kuishinda, endapo hatawalinda Saudi Arabia, UAE na Qatar dhidi ya Iran. Ujumbe utakuwa ni kwamba, kama Marekani ameshindwa kuwalinda UAE, Qatar na Saudi Arabia dhidi ya taifa dogo kama Iran, ataweza kweli kuwalinda Japan, South-Korea, Philippines na Australia dhidi ya taifa kubwa kama Uchina ???

Tano, THE COLLAPSE OF THE LAW OF NEUTRALITY. Katika sheria za kimataifa hasa wakati wa vita, The Law of Neutrality huyalinda mataifa ambayo hayapambani moja kwa moja, hata kama yanakuwa yanauza silaha kwa adui au kuwa na kambi za kijeshi ambazo hazitumiki kijeshi kushambulia adui. Kitendo cha Marekani kuvamia Iran bila sababu ni uvunjifu wa sheria za kimataifa. Hata Iran kuanza kuvamia Saudi-Arabia, UAE na Qatar ni uvunjifu wa sheria za kimataifa. Lakini Marekani hawezi kulalamika katika hili kwasababu yeye ndiye mvunjifu sugu wa sheria za kimataifa. Sheria za kimataifa ili zifuatwe na mataifa madogo, inategemea sana mataifa makubwa.

Hili lisipoangaliwa sana, tutaamka siku na kukuta Urusi kaanza kulipua Poland na Ujerumani kisa tu kuna kambi za jeshi za Marekani, hata kama hazitumiki kushambulia. Huku ndiko tunaelekea. Hivyo tukishafahamu haya, vitaifa masikini kama Tanzania vijiepushe na tabia za kupenda kujipendekeza kwa mataifa makubwa kama Uchina, Urusi na Marekani. Dunia inaelekea kubaya na kama tukitaka kuvuka itabidi kweli tusifungamane na upande wowote. Sasa wale wanopenda pesa za waarabu kisa ni wenzetu katika IMANI wakiendeleza tabia zao za kusajili manowari kule Zenji, wataliletea hili taifa matatizo makubwa mno. Tena kipindi hiki ukipigwa huna pakusemea maana kila mtu anapambana lwake.

==============================================================================

HALAFU KUNA MABAZAZI mengine yanasema INTERNATIONAL LAW IMEKUFA, haya nitayajibu baadaye.HAYANA AKILI

Its called bad planning
 
MALCOM LUMUMBA
Uko vizuri unashusha nondo huna ushabiki wala udini, unaandika uhalisia uliopo katika vita, asiyekuelewa kaamua kuchagua upande
Wasipo elewa basi tena 😎😎
Actually, I have a side: I side with the Victims of Imperialism.

I hate Fascism, I hate Imperialism and I can't stand Fanatical Nationalism.

If the evil things done by Americans were to be done by Tanzanians I would hate Tanzania as well.
 
Donald Trump hakimbii ila anacheza na masoko kwasababu ni mwanzo wa wiki.
Ndio maana anatoa kauli zenye utata '' Tumeua viongozi wa Iran wote, lakini kuna viongozi tuanongea nao''
Trump anasema ''nimeondoa vikwazo vya kuuza mafuta kwa Iran'' wakati huo huo anashambulia mitambo
Trump anacheza na masoko kwa bahati mbaya wanamuelewa, hakuna anayemchukua kauli zake seriously

Marekani huwa hafanyi vita mwanzoni wa mwiki bali mwishoni wakati masoko ya hisa yanapokuwa yametulia. Hapa anatafuta mbinu ya kukusanya vikosi vifanye uvamizi wa mguuni ili kukamata sehemu nyeti za Iran, jambo ambalo lina hatari kubwa sana sanaaa.
Kosa walilofanya vita ya siku 12 watalirudia. Katika vita hiyo Marekani/Israel walitumia kambi za Kuwait, Oman, Qatar, UAE ,Saud Aabiam Jordan na Iraq kumshambulia Iran na kuzuia makombora yasifike Irael
Mifumo ilipoanza kushindwa kwa makombora kufika Israel, wakasitisha vita. Iran ailikubali ili kujipanga

February 28 wakashambulia Iran tena! ilichukua masaa 2 Iran kujibu mapigo kwa mpangilio wa kuanza na Radar zote kubwa middle east na kambi za kijeshi zote! Anga la Israel limebaki wazi akombora yanaingia

Kupeleka askari wiki 3 baada ya shambulio ni kosa. Iran imepata nafasi ya kujipanga na wanajua hilo.
Marekani wataingia kwa nguvu lakini askari watakufa sana! Iran siyo Afghanistan wala Iraq

Vifo vya askari vinaongeza shinikizo USA. Kuna maandamano ya kumpinga Trump hayatangazwi na media.

Ndani ya Congress hakuna anayeelewa nini lengo, kwa mpango gani na mwisho wake ! kuna mgawanyiko

Uchumi wa Dunia unayumba lawama zikimwendea Trump! Ushawishi wa Marekani kijeshi unadhalilika.

Meli mbili kubwa zilizopelekwa kwa mbwembwe USS Lincoln na Ford zimeondolewa kwa kupigwa ili kuepusha aibu ya kazamishwa.

Ndege zao muhimu wanazojivunia zinapigwa. Yote haya yanaondoa ''ego'' za Trump na hataki kushindwa.

Kwasasa Trump anatafuta suluhu kwa udi na uvumba.Tatizo linalompata ni hili;

Israel inataka vita iendelee, Kwanza kuangusha utawala wa Iran. Pili,kuficha azma zao za vita ya kuchukua maeneo ya Lebanon, west bank na kweingineko na kufunika tatizo la Gaza linalowapa picha mbaya Duniani

Kwa upande wa nchi za Kiarabu zikiongozwa na Saud Arabia, wanasema vita inedelee '' huwezi kuchokonoa mzinga wa nyuki halafu utuachie msala''. Kwamba kumwacha Iran ni kumtangazia Ubabe wa middle east yote.
 
MALCOM LUMUMBA
Uko vizuri unashusha nondo huna ushabiki wala udini, unaandika uhalisia uliopo katika vita, asiyekuelewa kaamua kuchagua upande
Wasipo elewa basi tena 😎😎
Only in this thread kaonesha emotions kiasi.
 
Ndio maana anatoa kauli zenye utata '' Tumeua viongozi wa Iran wote, lakini kuna viongozi tuanongea nao''
Trump anasema ''nimeondoa vikwazo vya kuuza mafuta kwa Iran'' wakati huo huo anashambulia mitambo
Trump anacheza na masoko kwa bahati mbaya wanamuelewa, hakuna anayemchukua kauli zake seriously

Kosa walilofanya vita ya siku 12 watalirudia. Katika vita hiyo Marekani/Israel walitumia kambi za Kuwait, Oman, Qatar, UAE ,Saud Aabiam Jordan na Iraq kumshambulia Iran na kuzuia makombora yasifike Irael
Mifumo ilipoanza kushindwa kwa makombora kufika Israel, wakasitisha vita. Iran ailikubali ili kujipanga

February 28 wakashambulia Iran tena! ilichukua masaa 2 Iran kujibu mapigo kwa mpangilio wa kuanza na Radar zote kubwa middle east na kambi za kijeshi zote! Anga la Israel limebaki wazi akombora yanaingia

Kupeleka askari wiki 3 baada ya shambulio ni kosa. Iran imepata nafasi ya kujipanga na wanajua hilo.
Marekani wataingia kwa nguvu lakini askari watakufa sana! Iran siyo Afghanistan wala Iraq

Vifo vya askari vinaongeza shinikizo USA. Kuna maandamano ya kumpinga Trump hayatangazwi na media.

Ndani ya Congress hakuna anayeelewa nini lengo, kwa mpango gani na mwisho wake ! kuna mgawanyiko

Uchumi wa Dunia unayumba lawama zikimwendea Trump! Ushawishi wa Marekani kijeshi unadhalilika.

Meli mbili kubwa zilizopelekwa kwa mbwembwe USS Lincoln na Ford zimeondolewa kwa kupigwa ili kuepusha aibu ya kazamishwa.

Ndege zao muhimu wanazojivunia zinapigwa. Yote haya yanaondoa ''ego'' za Trump na hataki kushindwa.

Kwasasa Trump anatafuta suluhu kwa udi na uvumba.Tatizo linalompata ni hili;

Israel inataka vita iendelee, Kwanza kuangusha utawala wa Iran. Pili,kuficha azma zao za vita ya kuchukua maeneo ya Lebanon, west bank na kweingineko na kufunika tatizo la Gaza linalowapa picha mbaya Duniani

Kwa upande wa nchi za Kiarabu zikiongozwa na Saud Arabia, wanasema vita inedelee '' huwezi kuchokonoa mzinga wa nyuki halafu utuachie msala''. Kwamba kumwacha Iran ni kumtangazia Ubabe wa middle east yote.
Mkakati wa vita wa Iran umebadilika mno, na walijifunza somo gumu kwenye vita ya siku 12.

Mosi, waliacha kutumia mfumo wa Satelaiti za Marekani Global Positioning System (GPS) kuongoza mifumo yao ya makombora. Wengi walishangaa mno kwanini Iran bado anaendelea kutumia mifumo ya satelaiti za adui katika kushambulia maaduia zake. Kwenye vita ya siku 12 makombora na ndege zisizo na rubani zilifika lakini nyingi yalipata changamoto kwasababu za mfumo wa GPS ulikuwa unavurugwa kwa maksudi na Marekani hivyo wakawa wanashindwa kumshambulia adui.

Baada ya vita akahamia mfumo wa satelaiti wa Uchina BEIDOU ambao kwanza umeanza kutumika mwaka 2020, na unasafika kwa kuwa bora (Accurate) kuliko GPS. Hapa ndipi tatizo kwa Marekani na Israeli lilipoanzia.

Pili, Iran badala ya kushambulia Israel ameamua kushambulia miundombinu ya kijeshi (Military Infrastructure) inayofanya ndege na makombora ya Marekani na Marekani vifanya kazi. Analipua mifumo ya Rada na Ndege za Kijasusi ambavyo vimeunganishwa na satelaiti kusaidia kutoa taarifa mapema (Earl Warning Systems) ambazo ndiyo uti wa mgongo wa Airforce za Marekani na Israel.

Wataalamu wanasema, ndege kama F-15 na F-35, zinasaidiwa na mifumo ya mawasiliano mingine kama Radar & Satellite Tracking, ambapo Iran anailipua ili kuhakikisha adui anapata changamoto katika kushambulia. Ndiyo maana majuzi tu wameshambulia F-35 ndege tuliyoaminishwa kwamba haionekani kwenye Radar na bora dunia nzima.

Usiku wa kuamkia jana kalipuna ndege aina ya Boeing E-3 Sentry (AWACS) ambayo ndiyo nyenzo muhimu ya kuwinda makombora. Tena kaongezea na kulipua Tankers zinasofanya ndege za Marekani na Israel ziruke juu.Hapa kuna matatizo makubwa mawili ambayo yatamkuta Marekani: Kwanza kabisa, hizi ndege kama Boeing E-3 Sentry na Boeing KC-135 ni Cold War Relics, zimeanza kutengenezwa miaka ya 1955 na 1977, na mpaka leo hazina mbadala wake. Marekani hawezi kuzitengeneza ndani ya mwaka mmoja tu, itamchukua miaka mingi kufanikisha hili. Pili, itabidi aache kutumia kambi za Saudi Arabia, Bahrain, UAE au Qatar, na kuzipeleka ndege zake Jordan (Muwaffaq Salti Airbase) au Turkey (Incirlik Aibase), ambapo changamoto ni umbali.

Kutoka Muwaffaq Salti Airbase hadi Western-South Iran ni kilomita 700-900. Ndege kama F-15 na F-35 haziwezi kwenda umbali huu na kushambulia Iran bila kujazia mafuta walau nchini Iraq kupitia Tankers. Ndege za Marekani na Israel zikishajaza mafuta Iraq huwa zinachukua dakika 40 hadi 60 kuzunguka Iran (Western-South Iran (Loitering Time) na kushambulia, haziwezi kwenda ndani ya Iran (Central Iran hadi Eastern Iran) kwasababu hakuna Radar System ya kuziongoza na hakuna Tankers za kuwajazia mafuta endepo yataisha. Bahati mbaya Radar hazipo na AWACS hazipo jirani, unadhani watapona kirahisi ???

Iranian Attack.jpeg
\
(Hii picha ni maeneo ambayo ndege za Marekani na Israeli ziliweza kufika mwanzoni. Utagundua Central Iran na Eastern hakujaguswa sana na Iran kahamishia silaha kambi zake nyingi huko)

Tatu, Marekani huwa anatumia (Combined Arms) kupigana vita. Marines hawawezi kuingia kupambana na jeshi la mguu bila msaada wa jeshi la angani (Air Support). Haiwezekani, haiwezekani, na wakifanya hivyo yatawakuta kama yale ya Mogadishu 1993. Lakini pia, wanajeshi wa ardhini (Infantry) watahitaji Steady Supply Lines, kuhakikisha wanatumiwa silaha, madawa na chakula kwa wakati. Hivyo jambo kubwa ambalo watatiwa kulifanya ni kukamata Airport au Bandari ili kufanikiwa kutengeneza Steady Supply Lines. Hili halitakuwa jambo rahisi, maana kila manowari na kila ndege italipuliwa ikikaribia Iran.

Nne na Mwisho, Marekani anacheza kamari kama Napoleon Bonaparte. "If I catch Moscow, then Alexander and the Russians will surrender". Kumbe anajichanganya, Warusi wakaamua kuchoma moto Moscow yote na alipofika wakaanza kufa kwa baridi na njaa. Marekani anahisi akikamata kisiwa kama Kharga atawakomesha Iran kumbe anacheza kamali. Waajameni wanaweza kuanzisha Schorched Earth Policy kuhakikisha wanalipua na kuvichoma hivyo visiwa na Marekani asipate chochote. Mpaka sasa waajemi wameonesha uwezo wa hali ya juu kabisa kuvumilia maumivu kama wavietinamu.

Akiamua kuvamia Iran ndani kwa jeshi la miguu imekula kwake. Iran iko tofauti kabisa na Iraq ambako ni tambarare. Iran iko kama Afghanistan ambako ni milima tu. Hii ndiyo Relief Map ya Iran, inaonesha nchi nzima milima tu, sasa Marekani hapa atapeleka Abrams Tanks kweli ???
OIP.webp

Anacheza kamari mbaya mno....

Ila mimi nasubiri nione Super Power atafanyaje hapa...
Reference:https://defencesecurityasia.com/en/iran-abandons-us-gps-china-beidou-middle-east-security/
 
MALCOM LUMUMBA kama ulivyoanisha bandiko 305. Vita ya siku 12 iliwafunza sana Iran.Watu wengi wanalaumu Iran kusimamisha vita ile wakati ilishanza kuishambulia Israel kwa nguvu

Iran ilikabiliwa na vikwazo, kwanza, matumizi ya satellite za Marekani na pili nchi washirika wa Israel/ USA.Tatu , ilijifunza kudanganya taarifa za kijasusi kwa wapinzani wao. Nne walihitaji muda wa kufanya ujasusi wa kutosha katika nchi za Kiarabu. Iran hawakujua kina cha ushiriki wa nchi za Kiarabu

Kuhamia satellite za China (BEIDOU) kumedumamaliza ujasusi wa USA/Israel kwa kutoelewa mipango ya Iran.

Iran litambua Arab world wali play role kubwa kuzuia makombora kufika Israel. Vita walianza kufumua radar kubwa 2 nchi za Kiarabu kati ya 8 zilizopo dunianim wakafumua radar 2 Israel. Maana yake zimebaki radar 4 na moja ikiwa Korea. Nchi za Kiarabu zikabaki ''uchi', kambi za Marekani zikaanza kushambuliwa

Trump kasema Navy ya Iran imeharibiwa na haipo! Jana meli 3 za LCU (Landing craft utility) zinazobeba askari kwenye maji mafupi zimepigwa na 3 nyingine kutekekea kule Saud Arabia. 6 kati ya 32 zimefutika
Hiyo ni kazi ya Navy ya Iran baada ya kumhadaa Trump kwamba imefutika.

Marekani anakabiliwa na tatizo jingine, psychology. Kwamba ni mbabe hata akiguswa ni habari kubwa.

Marekani anamshambulia sana Iran lakini hiyo siyo news, news ni pale ndege zake za F-15 na F-35 na jana KC-135 na Sentry kuharibiwa. Hili linamuathiri sana Kisaikolojia na kumfanya awe defensive badala ya offesnisve.

Trump naye anachangia suala la saikolojia. Kitendo cha Trump kumdhalilisha MBS wa Saud Arabia, kimelipizwa kwa kuonyesha picha za uharibifu wa ndege za Marekani. Kwa kifupi ni kwamba Marekani imedhalilika kwa kichapo tena kwa ndege adimu wanazotumia.

Wakati huo huo Trump amezeiomba nchi za Egypt/ Pakistan n.k. kushawishi Iran ikubali kusitisha vita.
Israel inahujumu jitihada za Marekani kama vile kushambulia maeneo ya nishati na vyuo vikuu

Disadvantage kwa Marekani ni kuongezeka uwanda wa vita. Iraq , Hezbllah na Houth bila kujali uwezo wao wanaweza kusababisha madhara. Israel jana ilidai kuzuia makombora ya Houthi, kwa maana mifumo yao ya ulinzi inazidi kuelemewa! Iran inaendelea kupiga Israel bila kikwazo , Hezebollah ikileta tabu Lebanon

Tofauti ya Israel na Marekani ipo wazi, kwamba, Marekani anataka kumaliza vita kidiplomasia, Israel inamlazimisha abaki kwa kuhujumu jitihada. Marekani inapigana na Iran na imemsusia Israel kwa muda.

Kama kipigo kitaendelea kwa wiki 2 zaidi Israel inaweza kutumia Nuclear! huo ndio wasi wasi uliopo duniani
 
🤣
🤣
🤣
🤣
kuna vitu ili kussuport inabidi ujitoe akili,=uwe MPUMBAVU,watu wale wale wanaotaka SAMIA ashitakiwe ICC kwa mauaji ya October 29,ndio wanaomssuport Netanyau mwenye arrest warrant ya ICC kuua raia atakavyo sababu tu Israel ni Taifa teule
😁
😃
 
kuna vitu ili kussuport inabidi ujitoe akili,=uwe MPUMBAVU,watu wale wale wanaotaka SAMIA ashitakiwe ICC kwa mauaji ya October 29,ndio wanaomssuport Netanyau mwenye arrest warrant ya ICC kuua raia atakavyo sababu tu Israel ni Taifa teule🤣😁😃🐒🐒🐒
 
Likivuka hili wiki tu, wiki ijayo utatembea hapo Dar kwa mguu nakwambia. Mbaya zaidi hadi kule USA, Europe kutakuwa na hali mbaya maana Iran anashambulia Energy Infrastructure kuhakikisha kwamba Attack zake zinakuwa na The Multiplier Effect. Wamarekani wako mbali na Iran, lakini Iran has sent them A War Bill. Mfumuko wa bei utakaotokea Wamarekani watakuwa wa kwanza kuumia. Tena sanaaa.
Ndugu watanganyika, bado mnataka vita iendelee tu ???

AU bado mnaamini tu kwamba hii vita haiwahusu ninyi ???
 
Muda huwa ni mwalimu mzuri sana.

Nakumbuka mabazazi na madunya wa humu ndani mnamo tarehe 24 February 2022 siku ambayo Urusi alivamia Ukraine walinitafuta na kunisimanga sana. Wengine walidiriki hadi kukashifu taaluma yangu. Walishangaa kwamba kwanini Urusi ameshindwa kuivamia Ukraine na kuimaliza kwa haraka ilhali anajiita taifa kubwa (Super-Power). Niliwaambia vijana wa humu ndani kwamba Urusi alifanya makosa kuvamia jirani yake na kuna mambo alikosea, lakini kusema kwamba NATO+EU wataiangusha ni jambo lisilowezekana. Mataifa makubwa huwa yanafanya makosa pia (Political Blunders)

Mpaka 2026, Urusi na Ukraine wanapigana, huku Ukraine wakiwa wameumizwa zaidi. Urusi anatumia fedha nyingi sana kwenye vita na usalama, jambo ambalo siku vita ikiisha litazua matatizo makubwa mno kwasababu watu wengi watakosa ajira ambazo wanazifanya sasa. Pia kuna mambo kadha wa kadha. Sasa huu ni utangulizi tu:

Naomba niwaulize ninyi vijana wa humu ndani, kwanini Marekani (The Only Global Super-Power) ameshindwa kulimaliza taifa la Iran ndani ya wiki kama alivyofanya Afghanistani au Venezuela ??? Fahamuni tu kwamba hivi vita hapigani Marekani peke yake bali anasaidiwa na Israeli na washirika wengine kama Australia ambao imejulikana hivi karibuni kwamba walisaidia kuzamisha manowari za Iran. Hapo kuna Saudi Arabia, Jordan, Qatar, Bahrain, UAE, Azerbaijan na Mgambo wa kikurdi (kurdish Militia).

Donald J Trump alisema ni siku nne tu baada ya Ayatollah kulambishwa mchanga basi, Iran ingekuwa kaputi. Ila sasa yametokea tofauti. Marekani kweli kawatandika Iran, lakini nao wamemtandika vibaya mno. Mara ya mwisho kambi za kijeshi za Marekani zimelipuliwa hivi ilikuwa ni mwaka 1941 kule Pearl Harbour ambapo Japan aliua zaidi ya wanajeshi 2000. Jambo la kushangaza kulikuwa na silaha za ulinzi za kisasa kabisa kwenye hizo kambi kama THAAD na PATRIOT ambazo zilikuwa na mfumo bora kabisa wa rada duniani ambao umelipuliwa.

Mahoteli ambayo walikuwa wanakaa MAJASUSI na WANAJESHI wa Marekani yamelipuliwa. Mpaka sasa maswali ni mawili tu: Aidha Iran alikuwa amejipanga sana AU kuna mtu anamsaidia maana siyo jambo rahisi kufanya haya ambayo Iran amekuwa akifanya hasa kwenye kufanya mashambulio ya ulengaji bila kukosea (Precision Attack) ambayo hutegemea kwa sehemu kubwa mifumo ya satellite. Israeli nako yamewakuta, sehemu muhimu za kiusalama zinalipuliwa. Utapinga, utanuna, utabisha na kuleta hasara ila hii ndiyo hali ilivyo.

SASA IRAN ANAPAMBANAJE: Mwaka 2018 nakumbuka kuna uzi wangu nilifurumushiwa matusi na mabazazi na madunya wa humu ndani, nilioandika kuhusu dhana ya ASYMETRIC WARFARE. Dhana hii inafanya kazi pale ambapo taifa dogo au kikundi kidogo kinapambana na taifa kubwa. Lengo siyo kutaka kupambana CONVENTIONAL WARFARE, ila ni kumsababishia maumivu makubwa yule aliye mkubwa kiasi cha kufanya akimbie. Mfano halisi, ni USSR vs Mujahedeen au USA vs Vietcong.

Iran hana AIRFORCE kama USA na ISRAEL. Iran hana NAVY kama USA na ISRAEL. Iran alichokiamua ni kutengeneza FORMIDABLE ROCKET AND DRONE FORCE, ambalo lina uwezo wa kisasa kabisa kushambulia taifa lolote lile hapa duniani. Jambo ambalo wengi hatulifahamu ni kwamba Iran mbali na udhaifu wao mwingi, walianza kupambana na Marekani tokea mwaka 1979, na wameshuhudia USA akishambulia wenzake kama Iraq, Afghanistan, Libya na Venezuela. Unadhani ni wajinga ???

MADHARA ENDAPO VITA HAITAISHA MAPEMA:

Mosi
, The Aura of American Invincibility has been shattered before the world. Zile propaganda za kusema hakuna wa kumgusa Marekani hazipo tena. Iran katuonesha kwamba Marekani na Israel wanagusika. Hebu sasa fikiria, endapo Uchina ataamua kuvamia Taiwani, nani anaamini kabisa kwamba kambi za Marekani zilizopo South-Korea, Philippines, Japan na Guam zitakuwa salama, kama tu kambi kubwa za Marekani barani Asia zimelipuliwa juzi na jana na Iran, taifa ambalo halina nguvu kama Uchina. Kiukweli, Marekani alizichanga karata vibaya na yanamtokea puani.

Pili, Urusi atapata nguvu kubwa kutokana na bei ya mafuta kupanda. Saudi Arabia, UAE, Oman, Qatar na Bahrain wanaogopa kupitisha mafuta Mfereji wa Hormuz, ambao kwa siku mapipa milioni 17 yanapita. Vita ikiendelea hivi na Iran akafanikiwa kufunga kabisa mfereji, basi mafuta ya Ulaya na Asia itabidi yapatikane Urusi ambako kuna vikwazo. Juzi Vladmir Putin kasema anafikiria kusitisha kabisa kuuza gesi Ulaya. Sasa USA na EU watabakiwa na maamuzi kama haya: Ondoa vikwazo ili tupate nishati kutoka Urusi. Bahati mbaya wakiondoa vikwazo Ukraine ndiyo kwaheri.

Tatu, Urusi atapenda kulipiza alichofanyiwa Ukraine. Hii ndiyo tabia kuu ya Urusi. Niguse-Ninuke. Marekani akitingwa kule Iran, basi lazima atapunguza kuangalia Ukraine. Sasa itabidi silaha zote zinazozalishwa zienda Persian Gulf (Ghuba ya Uajemi) siyo Ukraine. Urusi na Uchina wanaweza kuigeuza Iran, VIETNAM 2 endepo Marekani akiendelea hivi bila kuomba msamaha. Bahati mbaya sana kwa alichokifanya Donald Trump, Marekani ikirudi nyuma kama kipindi cha Twelve Days War mwaka 2024, basi ndiyo mwisho wa siasa za MAGA na Trump, na anaweza kufungwa kwasababu ameanzisha vita bila kibali cha Bunge.

Nne, mpaka sasa SECURITY DIPLOMACY ya Marekani imekufa. Ameingia makubaliano ya ulinzi na Saudi Arabia mwaka 1971, na mataifa kama UAE, Qatar na Bahrain kwamba wakitumia Dollar kuuza mafuta basi atawalinda. Bahati mbaya wanapigwa na Iran, wanaomba kuuziwa silaha na msaada wa kijeshi lakini bado hawajapata, kipaumbele chake ni Israel na kambi zake. Hii ndiyo vita kubwa ya kipropaganda ambayo Marekani hawezi kuishinda, endapo hatawalinda Saudi Arabia, UAE na Qatar dhidi ya Iran. Ujumbe utakuwa ni kwamba, kama Marekani ameshindwa kuwalinda UAE, Qatar na Saudi Arabia dhidi ya taifa dogo kama Iran, ataweza kweli kuwalinda Japan, South-Korea, Philippines na Australia dhidi ya taifa kubwa kama Uchina ???

Tano, THE COLLAPSE OF THE LAW OF NEUTRALITY. Katika sheria za kimataifa hasa wakati wa vita, The Law of Neutrality huyalinda mataifa ambayo hayapambani moja kwa moja, hata kama yanakuwa yanauza silaha kwa adui au kuwa na kambi za kijeshi ambazo hazitumiki kijeshi kushambulia adui. Kitendo cha Marekani kuvamia Iran bila sababu ni uvunjifu wa sheria za kimataifa. Hata Iran kuanza kuvamia Saudi-Arabia, UAE na Qatar ni uvunjifu wa sheria za kimataifa. Lakini Marekani hawezi kulalamika katika hili kwasababu yeye ndiye mvunjifu sugu wa sheria za kimataifa. Sheria za kimataifa ili zifuatwe na mataifa madogo, inategemea sana mataifa makubwa.

Hili lisipoangaliwa sana, tutaamka siku na kukuta Urusi kaanza kulipua Poland na Ujerumani kisa tu kuna kambi za jeshi za Marekani, hata kama hazitumiki kushambulia. Huku ndiko tunaelekea. Hivyo tukishafahamu haya, vitaifa masikini kama Tanzania vijiepushe na tabia za kupenda kujipendekeza kwa mataifa makubwa kama Uchina, Urusi na Marekani. Dunia inaelekea kubaya na kama tukitaka kuvuka itabidi kweli tusifungamane na upande wowote. Sasa wale wanopenda pesa za waarabu kisa ni wenzetu katika IMANI wakiendeleza tabia zao za kusajili manowari kule Zenji, wataliletea hili taifa matatizo makubwa mno. Tena kipindi hiki ukipigwa huna pakusemea maana kila mtu anapambana lwake.

==============================================================================

HALAFU KUNA MABAZAZI mengine yanasema INTERNATIONAL LAW IMEKUFA, haya nitayajibu baadaye.HAYANA AKILI

Hii ndiyo jf Sasa. Umechambua vizuri sana
Unarikiwe
 
Wakati huo US na Israel wamekula vichwa zaidi ya 40 ya vingunge wa Iran, wewe endelea na propaganda zako mfu na uchambuzi uchwara ukiwa banda la uani kwa shemeji Mbezi Madale..
 
Hayo ndiyo malengo yao au ?
Kwahiyo wamefanikiwa kutimiza si ndiyo ?
Mbona bado wana endelea kupiga madaraja huko ?
 
Bado nashindwa kujua ni Propaganda au ni kweli.
Habari zimesambaa katika social media kua ndege 40 aina ya F-35 zimepigwa zikiwa katika pango la Siri katika Kambi ya ndege hizo ya Nevetim huko Isarel.
 
Wakati huo US na Israel wamekula vichwa zaidi ya 40 ya vingunge wa Iran, wewe endelea na propaganda zako mfu na uchambuzi uchwara ukiwa banda la uani kwa shemeji Mbezi Madale..
Wewe kenge kula vichwa sio kufikiwa malengo haya nambie baada ya kula vichwa kimebadilika??Majirani wote wamekula kipigo mlango bahari umefungwa Iran regime bado ipo madarakani haya nambie kula vichwa kumesaidia nini??
 
Bado nashindwa kujua ni Propaganda au ni kweli.
Habari zimesambaa katika social media kua ndege 40 aina ya F-35 zimepigwa zikiwa katika pango la Siri katika Kambi ya ndege hizo ya Nevetim huko Isarel.
Inawezekana ni kweli au uongo ila hata ikiwa kweli hawa wanaficha taarifa za madhaifu yao
 
Back
Top Bottom