Kwanini Marais wengi Afrika Magharibi wanaoa wanawake wazungu?

donga

JF-Expert Member
Sep 13, 2017
2,475
4,926
Kwa nyakati mbalimbali nimekuwa nikiona masekeseke mengi nchi za umoja wa ECOWAS ila kinachonichanganya kwanini? Ma-first lady wengi wa kizungu

Mfano mwaka jana kulitokea mapinduzi ya kijeshi ya NIGER baada ya kufuatilia niligundua Rais alikuwa na mke mzungu aliyesadikika ni mfaransa

Juzi tena wakati IVORY COST wanatwaa ubingwa pale jukwaani nikaona Rais akiwavisha medali wachezaji pia firstlady alikuwa ni mzungu.

Je ni kukosa uzalendo? Au ndio mapenzi ni upofu.

Na hii vipi kwenye usalama wa nchi hasa zile sensitive information.
 
Ni kweli. West Africa na hasa nchi zilizotawaliwa na Mfaransa zina marais wanaopenda sana kuoa Wazungu. Senegal wamewahi kuwa na marais 4 na wawili kati yao walikuwa na wake wazungu. Inawezekana ni mitego ya Wafaransa ili kuwatawala zaidi hawa jamaa zetu wa Francophone
 
Ni kweli. West Africa na hasa nchi zilizotawaliwa na Mfaransa zina marais wanaopenda sana kuoa Wazungu. Senegal wamewahi kuwa na marais 4 na wawili kati yao walikuwa na wake wazungu. Inawezekana ni mitego ya Wafaransa ili kuwatawala zaidi hawa jamaa zetu wa Francophone
MI nawasiwasi wale ni moles pandikizi wanammonitor rais akianza kwenda kinyume na maslahi wanamsabotage rais
 
Uzalendo hadi kwenye mapenzi?

Swali la kujiuliza wanawaoa wakiwa washakuwa marais?
SIjajua lakini ndio iwe accidentally kwa nchi tofauti tofauti?

Lakini pia mara nyingi marais wengi kabla ya kuwa rais hushika nyazifa za juu sana za kiuongozi km uwaziri, ukuu wa majeshi au ukuu wa taasisi

Hivyo ni rahisi mtu kupredict na kujipenyeza kabla muhusika hajawa rais
 
Afrika ya Magharibi wengi wamefuata ile dini ya mnyaanzi ambayo mwanamke anatunzwa ndani no school sasa unapokuwa raisi unahitaji mke msomi mwenye exposure ya kimataifa
Inaweza kuwa kweli but inamaana nchini hakuna wasomi au mabalozi, wakuu wa mashirika km WHO,FAO, UNICEF wenye exposure?

KWamm naweza amini rais akiwa na mke mzungu possibility ya kuwa kibaraka wa west ni kubwa sana
 
But muingereza ndio hatari alikotawala kote bado anamkono mpaka kwa super power bado hata middle east machafuko gaza ni mkono wa uingereza
Huyu ndiye Joka Kuu. Mbali ya yote, Muingereza au watu wa Ulaya ndio walioishika dunia, piga ua.

Vinasaba vyote vinarudi kwa wafalme na washirika wao kuanzia karne ya 17,18,19... Basi tu, watu huwa wanajiondoa ufahamu kwa makususdi au hawajui historia.

Utawasikia, oh Usicheze na wa Australia! kumbe ni off shoot ya Uingereza.

Oh usicheze na Marekani, huko ndio kabisa, matabaka yanayopambana ni shirika la tembo na punda.

Fuatilia vizuri tembo huyo katokea wapi! Hawa ni off shoot ya Uingereza ikujumlishwa na Ufaransa na Waholanzi na wengine waliofuata ni mashirika yaliyoanishwa na Wafalme wa Ulaya huko n.k

Huko middle east walisha chafua kitambo enzi za Umalaya.
 
Hao marais ni malimbukeni tu kuoa wazungu, bora hao wazungu wangekuwa ni raia wa kuzaliwa wa nchi zao. Pengine hao marais wana uraia pacha ndio maana wameoa huko kwenye mataifa yao mengine walio na uraia wake. Pia kikinuka wanakimbilia kwa wake zao walikowaolea
 
Ajabu, kihistoria, watu wa Afrika Magharibi walikuwa wanaongoza kwa kuwachukia Wazungu.

Kuna muasisi wa taifa fulani la Afrika Magharibi (sikumbuki nchi na jina) alioa Mzungu ilihali hakuwapenda.

Jibu lake ni kwamba alitaka kujua ubaya wa Wazungu hadi kwenye uchi wao namna walivyo.
 
Back
Top Bottom