Kwanini mapolisi wanakufa sana siku hizi?

Miguel255

Member
Joined
May 13, 2020
Posts
35
Reaction score
111
Hivi karibuni matukio ya mapolisi kufariki yamekuwa mengi sana tanzania. Sijui kama na nyie mmegundua au nimeona peke yangu tu.

Yaani ukiingia mtandao wowote ule iwe instagram, x zamani twitter au hata facebook ndani ya dakika mbili lazima ukutane na post ya msiba wa aliyekuwa askari polisi au mwanajeshi japo wanajeshi sio sana.

Sasa nikawa najiuliza je ni algorithm kwenye akaunti yangu ndo inaniletea taarifa za misiba ya polisi? Jibu likawa hapana kwasbabu nimeuliza watu kadhaa wenye interest tofauti na mimi na wao wameniambia hivyo hivyo kuwa wanakutana nazo.

Pengine tukio la tarehe 29 na siku zilizofuata zimefanya watu kuwafaitilia zaidi askari na hivyo kupelekea taarifa zinawahusu kusambaa kwa haraka. Pengine rate ya vifo vyao ipo vile vile ila tasnia ya habari kwa upande huo umekuwa mkubwa ndo maana tunaona ripoti nyingi za misiba yao. Hili bado sijalipatia jibu kamili.

Lakini pengine pia ule msemo wa damu italipwa kwa damu ndo unaochukua nafasi sasa. Hivi vifo vimekuwa vingi sana. Utasikia huyu kashumbuliwa na nyuki, huyu ajali, huyu kaumwa ghafla yaani asubuhi jioni kafa. Mambo ni mengi sana kwa ndugu zetu hawa.

Ikumbukwe kuwa wao pia ni wanadamu, kufa kwao ni sehemu ya ukamilisho wa ubinadamu wao. Lakini ikitokea vifo vinazidi hasa katika kundi fulani tu la watu lazima tujiulize kuna nini? Kwani hawa tu na kwanini sasa na kwanini eneo fulani tu.

Mi ningewashauri wamrudie Mungu kuliko walivyowahi kumrudia hapo kabla. Wasiishi kama nguruwe, unajua nguruwe anatengwa na waislamu wa dunia nzima lakini bado ananenepa tu. Wasiishi hivyo wao ni binadamu ile sare ni vazi la kazi kama ilivyo kwa madokta au makondakta.

Bado tunawapenda hivyo watafute namna kama ipo lakini, namna italayowafanya wakubalike na kupendwa na raia kama zamani. Hivi vifo vinanipa wasiwasi sana na wananchi bado wanafurahia kufa kwao.

Wiki hii hii kulikuwa na ajali maeneo ya airport ya dsm. Gari la polisi liligongana na Eicher moja hivi ya abiria. Kwa taarifa nilizozipata hakuna mwananchi hata mmoja alietoa msaada kwa askari wetu hawa.

TUNAELEKEA WAPI KAMA TAIFA?

Niliwahi kusema hapo kabla kuhusu watanzania kufurahia vifo vya watawala wao. Hili ni tatizo nalo litafutiwe ufumbuzi. Tena ufumbuzi wa haraka kama itawapendeza viongozi wetu.

Naomba mwenye data ya rate ya vifo vya mapolisi atujuze. Je imeongezeka? Ipo vile vile au imepungua?

Natamani kwenda mahospitalini huko ningeweza kupata majibu sahihi zaidi lakini mtu unawezaje kwenda kuulizia kitu kama hiki?😂

Nitaonekanaje? Au niandae study ya kunipa back up?

Nawasilisha.
 
Polisi wanakufa kama tunavyokufa sisi. Hakuna cha ajabu. Iwe kwa maradhi, ajali au kuuliwa.
 
Askari ni binadamu kamili kama wewe, sifa nilizonazo mimi, ulizonazo wewe alizonazo aliyopo Australia mpaka Marekani zote ni aina moja na njia yetu wote ni moja. Kifo ni lazima kwa kila mwenye sifa za ubinadamu ili mzunguko ukamilike. Kuna mtu alishawahi kusema "Kifo ni kifo tu"
 
Hivi karibuni matukio ya mapolisi kufariki yamekuwa mengi sana tanzania. Sijui kama na nyie mmegundua au nimeona peke yangu tu.

Yaani ukiingia mtandao wowote ule iwe instagram, x zamani twitter au hata facebook ndani ya dakika mbili lazima ukutane na post ya msiba wa aliyekuwa askari polisi au mwanajeshi japo wanajeshi sio sana.

Sasa nikawa najiuliza je ni algorithm kwenye akaunti yangu ndo inaniletea taarifa za misiba ya polisi? Jibu likawa hapana kwasbabu nimeuliza watu kadhaa wenye interest tofauti na mimi na wao wameniambia hivyo hivyo kuwa wanakutana nazo.

Pengine tukio la tarehe 29 na siku zilizofuata zimefanya watu kuwafaitilia zaidi askari na hivyo kupelekea taarifa zinawahusu kusambaa kwa haraka. Pengine rate ya vifo vyao ipo vile vile ila tasnia ya habari kwa upande huo umekuwa mkubwa ndo maana tunaona ripoti nyingi za misiba yao. Hili bado sijalipatia jibu kamili.

Lakini pengine pia ule msemo wa damu italipwa kwa damu ndo unaochukua nafasi sasa. Hivi vifo vimekuwa vingi sana. Utasikia huyu kashumbuliwa na nyuki, huyu ajali, huyu kaumwa ghafla yaani asubuhi jioni kafa. Mambo ni mengi sana kwa ndugu zetu hawa.

Ikumbukwe kuwa wao pia ni wanadamu, kufa kwao ni sehemu ya ukamilisho wa ubinadamu wao. Lakini ikitokea vifo vinazidi hasa katika kundi fulani tu la watu lazima tujiulize kuna nini? Kwani hawa tu na kwanini sasa na kwanini eneo fulani tu.

Mi ningewashauri wamrudie Mungu kuliko walivyowahi kumrudia hapo kabla. Wasiishi kama nguruwe, unajua nguruwe anatengwa na waislamu wa dunia nzima lakini bado ananenepa tu. Wasiishi hivyo wao ni binadamu ile sare ni vazi la kazi kama ilivyo kwa madokta au makondakta.

Bado tunawapenda hivyo watafute namna kama ipo lakini, namna italayowafanya wakubalike na kupendwa na raia kama zamani. Hivi vifo vinanipa wasiwasi sana na wananchi bado wanafurahia kufa kwao.

Wiki hii hii kulikuwa na ajali maeneo ya airport ya dsm. Gari la polisi liligongana na Eicher moja hivi ya abiria. Kwa taarifa nilizozipata hakuna mwananchi hata mmoja alietoa msaada kwa askari wetu hawa.

TUNAELEKEA WAPI KAMA TAIFA?

Niliwahi kusema hapo kabla kuhusu watanzania kufurahia vifo vya watawala wao. Hili ni tatizo nalo litafutiwe ufumbuzi. Tena ufumbuzi wa haraka kama itawapendeza viongozi wetu.

Naomba mwenye data ya rate ya vifo vya mapolisi atujuze. Je imeongezeka? Ipo vile vile au imepungua?

Natamani kwenda mahospitalini huko ningeweza kupata majibu sahihi zaidi lakini mtu unawezaje kwenda kuulizia kitu kama hiki?😂

Nitaonekanaje? Au niandae study ya kunipa back up?

Nawasilisha.
Kuficha ushahidi
 
ukikutana na post ya msiba wowote usiiangalie mpaka mwisho wala kulike au kukoment,maana system inadhani unapenda kuona misiba.
post mbili ya tatu unakula msiba mwingine.

kwa sababu huelewi chochote wala huna muda wa kukagua unadhani kila mtu anatizama hicho unachotizama,na kuamini ni misiba ya hivi karibuni.

polisi wanakufa kawaida kabisa kama wanavyokufa watu wengine,wala usisikilize wajinga wanaotaka uamini kwamba kuna laana inawaua zaidi ya watu wengine.
 
We ulitaka waishi hadi lini ili wakifa isiwe ajabu?
 
Ni kundi lenye waajiriwa wengi...
Pengine ni wa kwanza au wapili kwa wingi kutoka waalimu
Watu wakiwa wengi na matukio yanakuwa mengi pia
LAKINI PIA wabongo hatuna elimu ya utandawazi, tumedandia Treni kwa mbele...
Taarifa moja inaweza kujirudia kila baada ya muda au kusambaa na kuzusha taharuki kwa sababu ya kukosa elimu ya utandawazi.
 
Pole mkuu kwa kufikiri wanaokufa sana ni polisi tu. Watu wanaokufa daily ni wengi sana. Anyway ukiwa unaupenda sana kufuatilia post za vifo na hata kusearch na kugusa link zihusianazo na vifo basi kila siku utapata Kuona makumi ya post za vifo .
 
Back
Top Bottom