CHAGOSI GERALD
Senior Member
- Jan 25, 2020
- 162
- 286
(Gafla Mwendawazimu akanyang'anya mic)
MWENDAWAZIMU:
Hebu njoo hapa kijana… njoo karibu, usiogope, mimi siwezi kukugusa - tayari nimegusa ukweli, na huo ndio ugonjwa pekee unaoambukiza nilio nao.
Uliniuliza “Kwa nini siku hizi kujitolea JKT ni hekima ya mpumbafu?”
Sikiliza basi.
Sijasema kujitoa kwa nchi ni upumbavu. HAPANA.
Nimesema kujitoa kwenye mfumo unaotafuna wanaojitoa - huo ndiyo ujinga uliofunikwa kwa bendera.
Nitakuuliza maswali, maana mimi ni mwanafunzi wa Socrates; najifanya mjinga ili nikuoneshe wenye akili wangapi wanatembea uchi.
Kijana, kama JKT ni mahali pa uzalendo… kwa nini wanaoenda huko wanarudi wakiwa wanajua kuimba nyimbo za kuamsha njaa kuliko nyimbo za kuamsha sekta ya viwanda?
WEWE (kijana):
“Labda ndio mafunzo?”
Aha!
Kwa hiyo mafunzo ya uzalendo ni kujua kupanga viatu na kuoga kwa sekunde 17?
Nzuri sana. Na huko viwandani, ambapo China wanafanya robot?
Hawajui kupanga viatu. Tumewashinda.
Kijana, kama JKT ni daraja la taifa imara… kwa nini hakuna daraja lililojengwa na JKT?
Uzuri, sema ukweli tu.
Hata daraja la akili halipo - maana vijana wanarudi wakiwa na miili imara na mawazo yaliyovunjika.
Wanajua kutembea "kwa hesabu".
Lakini hawajui kuhesabu biashara.
Wanajua kumaliza mazoezi ya viunguzo.
Lakini hawajui kumaliza mzunguko wa mtaji.
Wanajua kunyanyua matofali.
Lakini hawajui kufanya valuation ya mradi.
Lakini oh! Wanaitwa "vijana wa kujenga taifa."
Ni taifa gani?
Taifa la nani?
Kwa njia ipi?
Tafakari kabla mfumo haujakutumia kama kifuta machozi kwenye macho makavu ya wanasiasa.
Kijana, kama kujitolea JKT ni heshima… kwa nini heshima hiyo haikupi ajira?
Unarudi na "cheti cha uzalendo."
Ukikipeleka TRA: “Hiki kipo wapi kwenye NACTE classification…?”
Ukikipeleka kwenye kampuni binafsi:
“Hatuajiri uzalendo, tunaajiri ujuzi.”
Ukikipeleka ATM:
Kile kimashine kinakutazama kama kiumbe wa ajabu. Hakijawahi kukutana na "cheti cha kujitolea."
Kijana, kwa nini serikali yenyewe haijitolei JKT?
Wabunge hawajawahi kupangwa mstari wakipiga "attention."
Mawaziri hawajawahi kupigwa pushup 40 kwa kuchelewa.
Na kama ni kujenga taifa,
kwani taifa linaanza kujengwa chini?
Kwanini mawaziri hawaanzi?
Hivi ni wangapi wamewahi kupelekwa JKT kwa kukiuka maadili ya uongozi?
Hawapo.
Ni vijana tu wanaotakiwa kuwa watakatifu.
Wale waliobomoa taifa - wao ni "waheshimiwa."
Wale wanaojaribu kulijenga - wao ndio "wapumbavu wa kujitolea."
Kijana, kujitolea kunafanywa na watu wanaoamini watakatiwa jiko baada ya kutoa nguvu zao.
Lakini hapa, nguvu zako zinalishwa mfumo, na mfumo haujawahi kurudisha hata mfupa.
Umeona waziri akisema:
"Vijana wa JKT wametusaidia kuvuna mazao"?
NDIO.
Je, umewahi kuona waziri akisema:
“Na sisi tutawasaidia kumiliki viwanda”?
HAPANA.
Wanataka nguvu zako.
Hawajali mustakabali wako.
Sasa sema ukweli…
Kujitolea kwenye mfumo usiotakiwa kukutolea chochote – si hekima ya mpumbavu?
Lakini hebu niseme kitu cha mwisho kabla hawajanifunga kamba mkono na mguu:
Kujitolea si tatizo -
Kujitolea bila mfumo unaokujenga, huo ndio upumbavu.
Maji ukiyamwagia mbegu, yanakua.
Maji ukiyamwagia mawe, yanatiririka kama machozi ya mfungwa.
JKT ingeweza kuwa:
• Chuo cha viwanda
• Tanuru la utaifa
• Kiwanda cha viongozi
• Shule ya ujasiri, ujuzi, na uzalendo wenye matokeo
Lakini ikawa kambi ya matumizi, si taasisi ya uzalishaji.
Na kijana yeyote anayeingia humo bila kujua ukweli huu…
ameamua kupima kina cha bahari kwa mguu.
Ukiona nimekuita "mpumbavu,"
sio kwa sababu hukupenda nchi yako.
Ni kwa sababu nchi yako haijawahi kukupenda kama wewe unavyoipenda.
Sasa nenda ukafikiri.
Kwa sauti ndogo.
Kwa akili kubwa.
Kwa roho iliyoamka.