Kwanini Makao Makuu ya CHADEMA hakuna picha ya Rais wa nchi?

Hivi baba wa taifa alikuwa Rais na wakati huo huo mwenyekiti wa chama cha chadema?
 
inawezekana Dr Slaa bado anaweweseka na mzimu wa Jk kumwangusha uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 na Mbowe 2005. kuweka picha ya JK chadema makao makuu ni kutafuta makuu.
 
Ofisini kwa Nape kuna picha ya Dr Slaa akikumbatiana na Nape katika tukio ambalo sijajua chanzo cha picha hiyo lakini Dr Slaa sio mwenyekiti wa CCM. Nape yumo humu Jf ataniunga mkono kwa kuweka ukweli huu wazi
 
Mtei na Dr slaa wamewahi kuwa wana ccm endapo nitaweka picha zao ukutani nyumbani kwangu zitakuwa ni picha za wanaccm wa zamani au chadema wa leo. kuweka picha za kumbukumbu ukutani kunategemea sababu za mtundika picha. kama chadema wanaogopa kuweka picha ya Jk pengine mganga wao kawaambia hivyo ili kushinda uchaguzi wa mwaka 2015 tutajuaje......ni mfano tu.
 
Imefika wakati sasa KATBA MPYA ijayo iseme wazi kuwa tubaki na picha mbili tu maofisini na kwenye noti zetu. Ya Mwalimu na Sheikh Karume waasisi wa Taifa hili.
 
Huyu alieleta post hii kweli ni great thinker,yaani katafuta vitu vyote akaona hili ndo jambo muhimu,kweli ni great thinker yuko jukwaani
 
Pumba! Kwani makao makuu ya ccm kuna picha ya Mwenyekiti wa Chadema? Yule ni Mwenyekiti wa CCM!

Mkuu, tofautisha Mwenyekiti wa chama na Rais wa nchi.

Ndiyo maana hata Chadema walivyokwenda Ikulu walikwenda kuonana na Rais wa nchi turudi kwenye mada.

Ni utaratibu wa kawaida tulioachiwa na Mwalimu Nyerere ni vizuri kuweka picha ya Rais kwenye ofisi zetu.

Ni Mkuu wa nchi...
 
Great Thinkers..

Siku za karibuni nilipata nafasi ya kutembelea Makao Makuu ya Chadema, Kinondoni Mtaa wa Ufipa.

Kitu cha kushangaza kama kawaida za ofisi kuna picha mbili ya Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere na Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete.

Ofisi za Chadema hakuna picha ya Rais Kikwete, kuna picha ya Nyerere tu.

Chadema, Rais Kikwete ni Rais wa Tanzania wekeni picha ya Rais ukutani ndani ya ofisi zenu
utawekaje picha ya mwenyekiti wa chama kingine tena cha mafisadi kwenye ofisi ya chama chako!!!!!!!!!
 
utawekaje picha ya mwenyekiti wa chama kingine tena cha mafisadi kwenye ofisi ya chama chako!!!!!!!!!

Mkuu, unaweza kunisaidia mie pamoja na wana JF wengine.

Uongozi wa Chadema walivyokwenda Ikulu walikwenda kuonana na nani?
 
Ni jambo la aibu kabisa kujaza picha za Mustafa Sabodo, na kumusahau Mkuu wa nchi Rais Jakaya Kikwete
 
Back
Top Bottom