Kwanini makampuni makubwa ya kimataifa yanayouza bidhaa za rejareja yanaondoka Tanzania?

Kuna kitu kinaitwa consumption patterns, Tanzania kwa asilimia kubwa shopping malls au supermarkets can't work well for some years to come, mfano mtu anayekaa Kimara kabla hajaenda supermarket Mlimani City kununua bidhaa nyingi za jumla, atakutana na masoko makubwa mawili ambayo atapata groceries kwa zaidi 90% ya mahitaji yake.

Au Kuna ile shopping mall ya Aura au ile ya waislam, mtu anayekaa kwenye ile neighborhood kabla ya kwenda kwenye hizo malls ana option ya kwenda kisutu au Kariakoo sokoni and bad news to these malls and supermarket (Soko la kariakoo linajengwa).

Shopping malls can work sehemu kama mji wa serikali unajengwa (hii ni nafasi ya kutoachia) au maeneo ambayo yako mbali na masoko makubwa ambayo yana options za bei nafuu.

Also kama nchi yetu haitakuwa Industrial country basi hata maduka yanayofanya kazi hasa ya nguo au electronics yatakuwa disrupted na online business
 
Kodi ndio kikwazo watu hawawezi kumudu hizo kodi zinazowekwa kwenye bidhaa ukute Tv Lg SA inatoka kwa gharama ndogo ikifika Tanzania kodi ya Tv inafika 100 usd na zingine ni zaidi wakati wenzetu Simu na Laptop zimewekwa sehemu ya kutoa Elimu huku kwetu ni anasa inachapwa kodi bidhaa za watoto chini ya miaka mitano hazina kodi SA wakati Tanzania mpaka bidhaa ambazo mtoto yupo tumboni zinachapwa kodi na pia Watanzania wanaogopa Electronics mpya kwa sababu ya bei iliyochanganyikana na kodi kubwa mbona Lusaka hapo Game wanapiga kazi na hao Shoprite kwa sababu wenzetu wanachapa kodi ila zile favourable sio za kuumizana kama Tanzania na haya makampuni hayataki ujanja ujanja..

Well said
 
Kwa hali ilivyo hata wazalishaji wa ndani ngoma ni ngumu vitu vingi vya matumizi muhimu vimekua anasa!? Yaani ni mpaka iwe lazima sana tena kwa ushauri wa daktari
JamiiForums-1502650973.jpg
 
Sahihi, Tanzania supermarkets aina ya game ni ngumu sana kufanikiwa.
Kila nyumba ina kaframe nje.. nani ataenda Supermarket?
Nchi nyingi watu wanaenda fanya shopping sehemu rasmi za biashara kwa ajili ya wiki au mwezi, wanahifadhi. Kwetu, unatumwa chumvi kwa mangi mboga ipo dukani.
 
Simple..Tanzania has no middle class .tuna masikini wa kutupwa wengi,na matajiri wa kutupwa wachache .hayo maduka yanawekwa hai na middle class..

How do you define middle class in countries like TZ? Hapo wachumi watanisaidia..ila kwangu kama Una familia na nyuma ya kuishi pia Una magari si chini ya mawili unayoweza kuyabadilisha every 3-5 years,watoto wanaoenda private school..then you are in the middle class.kama siyo karibu kwenye kundi la masikini wa kutupwa
 
Hii nchi ina culture fulani very unique duniani. Always deviate from normal.
Tanzania haina unique culture wala ñini, ukweli ni kwamba tangu serikali ya awamu ya nne nchi ilianza kurudi kwenye ujima.

Awamu hii ndiyo imetia fora zaidi kwa kuwanyang'anya wananchi hata kile kidogo walicho nacho.

Watu wamepunguza matumizi yao kwa kiasi kikubwa, ukiongezea na ukosefu wa maji, umeme; ukame na kupanda kwa bei za vitu na petroli/ dieseli, nani aende supermarket?
 
Hawa wanajiondoa nchi zote za afrika mashabiki kuanzia Kenya, Uganda, Tanzania, Rwanda nk
Ni kama Hao shoprite walivyofunga, waliondoka nchi zote za afrika mashariki
Sidhani ni kama suala la Tanzania kua na gharama au kukosa wateja.
 
Makampuni mengine yanaondoka east africa lakin mnapokuja kuanzisha thread mnaizungumzia Tanzania pekee
Ndio Shida ya watanzania mkuu, kazi ya kukandia kwetu
Hao jamaa wametangaza kufunga stoo zao za afrika mashariki Sio Tanzania pekee ila mtu anavyoshadadia kua ni Tanzania pekee inafikirisha.
 
Gharama za uendeshaji mkuu.....umeme ghali halafu haupatikani, maji ya shida pamoja na wizi....wabongo wapigaji sana....halafu pia purchasing power iko chini sana....watanzania wachache sana ambao wanaweza fanya shopping pale...
Bongo labda uuze bia/vyakula au bidhaa zinazohusiana na magari-spea au mafuta. Vinginevyo Lazima ufunge biashara.
 
Back
Top Bottom