Kwanini makampuni makubwa ya kimataifa yanayouza bidhaa za rejareja yanaondoka Tanzania?

Imeloa

JF-Expert Member
Jan 28, 2013
10,763
11,783
Katika siku za hivi karibuni, Tanzania imeshuhudia maduka makubwa kadhaa yakifungwa, huku la hivi punde zaidi katika orodha likiwa ni Game Stores, ambalo kufungwa kwake kutaathiri vibaya zaidi ya kazi 100 za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja. Kuondoka kwa Game kunaikumbusha nchi ya Shoprite kutoka Afrika Kusini pamoja na Uchumi na Nakumatt kutoka Kenya, ambazo kwa nyakati tofauti ziliamua kujiondoa kwenye soko la Tanzania baada ya kushindwa kufanya kazi kwa matarajio.

====

Business stakeholders and analysts yesterday pointed out possible factors over why multinational retailers are closing shop in Tanzania.

In the recent past, Tanzania has witnessed a number of supermarkets shutting down, with the latest one in the list being Game Stores, whose closure will adversely affect over 100 direct and indirect jobs.

The exit of Game reminds the country of Shoprite from South Africa as well as Uchumi and Nakumatt from Kenya, which at different times decided to exit the Tanzanian market after they failed to perform to expectations.

A statement seen by The Citizen shows that the last trading day for the Game Stores in Tanzania, Kenya, Uganda, Nigeria and Ghana will be December 25, 2022.

According to the statement, the decision by the Game Stores to exit the identified markets came after various consultations were made.

“We recognise this will be the source of disappointment for many people associated with the Game brand in these countries,” reads the statement in part.

It further states: “In terms of the immediate next step, it is our intention to initiate a stock clearance sale in our stores in each of these countries this week.”

Speaking on condition of anonymity, one of the Game Store officials told The Citizen that economic hardships caused by Covid-19 pandemic was to blame for the supermarket’s closure.

“Our cash flow has been hit hard to the extent that we cannot keep on operating. The closure of Game will see its 45 employees lose their jobs,” he said.

He added that the Game Store was also working with about 55 people from a cleaning company.

Tanzania Business Community’s communications director Stephen Chamle hinted the closure of business may have been due to some difficulties in running the business in the named states.

Noting that each type of product had a separate licence, Mr Chamle told The Citizen that some licensing laws were not in favour of supermarkets.

“It is not easy to implement these kinds of laws. Something needs to be done,” he suggested.

He also said that the Investment Act (of 1997) was not impressive in the eyes of serious investors.

The minimum capital of $300,000 for foreign investors was peanuts to the extent of attracting unscrupulous foreigners selling on the streets the same products available in supermarkets and other shops.

He noted that foreign investors should mainly focus on setting up factories, instead of bringing in ready-made products.

“If we are to get serious investors, the minimum investment capital for foreigners should be at least $1 billion,” stressed Mr Chamle.

Efforts to get comment from the Ministry of Investment, Industry and Trade proved futile as phone calls went unanswered.

However, in the government’s quest to reform the country’s economy, a new proposed Investment Act was tabled in Parliament for the first reading in September, this year.

The legislation piece seeks to encourage and attract more trade and investments.

An economics don from the University of Dar es Salaam, Dr Abel Kinyondo, said the closure of supermarkets was a reflection of the country’s economic situation.

This suggests that demand for supermarket products has dwindled after people’s pockets were negatively impacted.

“It is a matter of pockets being hit that has made people who used to go to supermarkets to consider the same as luxury,” recounted Dr Kinyondo.

For his part, economist cum trade expert Donath Olomi observed that as one of the government’s top priorities was attracting investment, one needed to go further and think not only critically, but strategically about what this decision would mean to other investors who might want to invest in the same line of business.

“The exit in supermarket business line is alarming,” warned Dr Olomi.

“The government must critically find out the reasons and impact of these exit trends linking it to the backward linkages amidst efforts the government is taking to call for more investors in the country.”

Property management strategist Andrew Kato noted that: “Given the free entrance policy of various mega tenants competing with Game within the mall, as well as Shoppers’ strategic positioning and customer value creation, the closure of Game was seen coming.”

However, he said, he did not think it was a loss to the Mlimani Holdings Ltd as a landlord, given the size of the-waiting list of the would-be renters that is in the pipeline.
 

babukijana

JF-Expert Member
Jul 21, 2009
9,977
9,626
Gharama za uendeshaji mkuu.....umeme ghali halafu haupatikani, maji ya shida pamoja na wizi....wabongo wapigaji sana....halafu pia purchasing power iko chini sana....watanzania wachache sana ambao wanaweza fanya shopping pale...
Sawa kabisa,
Miaka Shoprite inafunguliwa kuna bibi mmoja alipiga deal sana pale
 

City Owl

JF-Expert Member
Mar 21, 2014
2,231
3,964
Kila nyumba ina kaframe nje.. nani ataenda Supermarket?
Nchi nyingi watu wanaenda fanya shopping sehemu rasmi za biashara kwa ajili ya wiki au mwezi, wanahifadhi. Kwetu, unatumwa chumvi kwa mangi mboga ipo jikoni.
 

Kinyungu

JF-Expert Member
Apr 6, 2008
15,051
26,742
Imagine mtu anaenda mlimani city pale games kushangaa tu hanunui hata tooth pick. Kweli watatoboa kweli hao wenye supermarket?

Wabongo wamezoea kununua vitu kwa Mangi tena kwa kukopa. Mambo ya Games, Shoprite, Nakumatt au Uchumi watayaweza wapi?
 

Peramiho yetu

JF-Expert Member
May 25, 2018
4,856
13,309
Kila nyumba ina kaframe nje.. nani ataenda Supermarket?
Nchi nyingi watu wanaenda fanya shopping sehemu rasmi za biashara kwa ajili ya wiki au mwezi, wanahifadhi. Kwetu, unatumwa chumvi kwa mangi mboga ipo dukani.
Sasa mkuu unataka maduka ya akina mangi yafungwe? ili twende super market ambako hawauz kiwembe Cha kunyolea vuz sh 100 hawauz hoho moja tsh 50 kwa mangi hata kondomu 1 unapata kwa TSH 100
 

Isanga family

JF-Expert Member
Feb 25, 2015
11,094
16,506
Kodi ndio kikwazo watu hawawezi kumudu hizo kodi zinazowekwa kwenye bidhaa ukute Tv Lg SA inatoka kwa gharama ndogo ikifika Tanzania kodi ya Tv inafika 100 usd na zingine ni zaidi wakati wenzetu Simu na Laptop zimewekwa sehemu ya kutoa Elimu huku kwetu ni anasa inachapwa kodi bidhaa za watoto chini ya miaka mitano hazina kodi SA wakati Tanzania mpaka bidhaa ambazo mtoto yupo tumboni zinachapwa kodi na pia Watanzania wanaogopa Electronics mpya kwa sababu ya bei iliyochanganyikana na kodi kubwa mbona Lusaka hapo Game wanapiga kazi na hao Shoprite kwa sababu wenzetu wanachapa kodi ila zile favourable sio za kuumizana kama Tanzania na haya makampuni hayataki ujanja ujanja..
 

Nunio

JF-Expert Member
Sep 17, 2013
213
564
Imagine mtu anaenda mlimani city pale games kushangaa tu hanunui hata tooth pick. Kweli watatoboa kweli hao wenye supermarket?

Wabongo wamezoea kununua vitu kwa Mangi tena kwa kukopa. Mambo ya Games, Shoprite, Nakumatt au Uchumi watayaweza wapi?
Semeni ukweli jamani. Kadri mnavyozidi kutia pesa kwa mafisadi na wazee wa michongo mtaanj, ndivyo Tzs inavyoishiwa nguvu. Pesa haifanyi maendeleo endelevu zaidi ya matanuzi, manunuzi ya vitu vya anasa nje ya nchi na safari za nje.

Kama kweli vitu vya pale ni European/American standard, basi ni wazi tulio wengi hatuwezi kununua na hasa wakati huu.

Beer moja huko duniani ni kati ya Tzs 6,000 mpaka 12,000. Sasa hiyo bei ndo utaipata maeneo yote yenye mchanganyiko wa mataifa hapa ndani, na ni bia hiyo hiyo unainywa kwa Tzs 2,000 kitaa, unadhani nini kitatokea hapo?
 

binti kiziwi

JF-Expert Member
Aug 4, 2014
5,917
12,664
Naunga mkono hoja za wachangiaji waliotangulia.

1.Nchi ambayo 80% ya wananchi wake ni walalahoi, maduka makubwa uongo, hayawezi kusurvive. Wabongo sababu ya kipato hawawezi kushop kwenye one-stop stores. Nchi za wenzetu hata maduka yaliyopo mitaani ni min-markerts ambazo kwa size ni makubwa sana kulinganisha na huku kwetu, tuduka duka kila kona.

2. Kodi kodi kodi, bidhaa mfano za vyakula si zakuwekea mikodi as if tuna viwanda vya maana, wakati viwanda vingi ni small scale havitoshelezi mahitaji yaliyopo. Bidhaa zote ambazo si za anasa zinatakiwa kuwa na kodi nafuu.
 

City Owl

JF-Expert Member
Mar 21, 2014
2,231
3,964
Sasa mkuu unataka maduka ya akina mangi yafungwe? ili twende super market ambako hawauz kiwembe Cha kunyolea vuz sh 100 hawauz hoho moja tsh 50 kwa mangi hata kondomu 1 unapata kwa TSH 100
Hapana. Maduka ya akina mangi yaendelee kuwepo tu. Actually yanatusaidia.
Mleta mada amehoji chanzo cha makampuni ya biashara za rejareja kufungwa, nami nimeeleza mojawapo ya sababu hizo.
 

Teknocrat

JF-Expert Member
Oct 20, 2018
2,499
5,212
Imagine mtu anaenda mlimani city pale games kushangaa tu hanunui hata tooth pick. Kweli watatoboa kweli hao wenye supermarket?

Wabongo wamezoea kununua vitu kwa Mangi tena kwa kukopa. Mambo ya Games, Shoprite, Nakumatt au Uchumi watayaweza wapi?
😂
Hapa mnunuaji hapa,
1667146848020.jpeg
 

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
102,119
179,438
Katika siku za hivi karibuni, Tanzania imeshuhudia maduka makubwa kadhaa yakifungwa, huku la hivi punde zaidi katika orodha likiwa ni Game Stores, ambalo kufungwa kwake kutaathiri vibaya zaidi ya kazi 100 za moja kwa moja na zisizo za moja kwa moja. Kuondoka kwa Game kunaikumbusha nchi ya Shoprite kutoka Afrika Kusini pamoja na Uchumi na Nakumatt kutoka Kenya, ambazo kwa nyakati tofauti ziliamua kujiondoa kwenye soko la Tanzania baada ya kushindwa kufanya kazi kwa matarajio.

Nchi imefirisika , wananchi hawana hela , kwa sasa uwezo wa Watanzania wengi (90%) ni kununua nyanya masalo

Maisha yamekuwa magumu kuliko wakati wa vita vya kagera , ila hali hii inafichwa
 
5 Reactions
Reply
Top Bottom