GE2025 Kwanini maandamano ya 29 October yatafeli vibaya sana

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Hizi mambo za maandamano siku ya uchaguzi , nahisi itaathiri zaidi wapiga kura , kama ilivyo kawaida yetu ya uoga hata wenye nia ya kupiga kura wengi watajichimbia uvunguni .

Yaani Wapiga kura wasipojitokeza. Hata kama maandamano hayatafanyika tayari ni mafanikio makubwa sana.

Mpaka sasa Maza salamu keshazipata ndiyo maana unamuona akifanya makosa mengi mengi wakati wa Kampeni. Mambo yamemzidia kiasi kwamba anasahau sahau na kufanya mistake nyingi kwenye hotuba zake.
 
Umeelewa nilivyosema hakuna checks and balance kwenye jeshi letu mkuu? Yaani kesi ya nyani unampa ngedere asuluhishe, unategemea nini?

Ukiona nchi nyingine nyingi zinafanya peaceful demonstrations kuna mambo yapo kisheria na hata watu wakiandamana huoni jeshi la polisi likijichukulia sheria mkononi, kwetu haipo. Unaandamana mbele ya polisi anayeweza kushoot risasi za moto na kuuwa watu kadhaa bila yeye kuchukuliwa hatua zozote za kisheria, hii ipo kwetu na baadhi ya nchi chache duniani.

Hata hapa Tanzania sheria zinaruhusu watu muandamane kwa amani sio huko nje tuu

Nishasema polisi mnawasingizia. Lazima ujue wenye shida ni watanzania wenyewe. Katiba ni kitabu tuu ni kama gazeti la udaku au gazeti la mwananchi.
Ishu ipo kwa watu wameamua kuichukuliaje.

Huwezi kuliteja jeshi na wananchi wake. Huwezi.
Tabia zote za jeshi ni matokeo ya jamii husika.

Halafu ujue tu polisi wanachohitqji ni equipment, wala sio idadi. 10,000 wanatosha kabisa kuifanya Dar ikae sawa wakiwa na right artillery/machinery. Kama unadhani kwa jeshi letu ni rahisi kuandamana basi toka peacefully uandamane ndio utaelewa jeshi letu linatumia akili, mabavu, kulinda maslahi ya watanzania au kundi fulani la watu.

Unaweza kumlaumu mtanzania kuwa mwoga na ukasahau weledi wa jeshi letu kumlinda mtanzania vs mtawala.

Polisi au jeshi hata liwe milioni moja na silaha za namna yote halina uwezo wa kukabiliana na wananchi milioni 40 walioamua kudai jambo lao.

Watanzania tuache visingizio.

Ni kwamba sisi ndio tumezalisha jeshi unaloliona alafu tunatafuta wa kumlaumu
 
Maandamano kwa nchi yetu labda yawe ya kuipongeza serikali au yale ya May Mosi ila mengine mengine haya wataandamana vijana wa miaka ya 2000 kuja mbele.
Wataandamana pale ambapo watakuwa wameamua wenyewe kwa kukosa
Ajira
maisha mazuri
Mambo ya msingi
Endeeeni kuishi kwa kukariri.

Safari hii Watanzania tuko serious kulikomboa kweli Taifa letu kutoka mikononi mwenu Mafisadi.
 
juliusnyerere.jpg
 
Hata hapa Tanzania sheria zinaruhusu watu muandamane kwa amani sio huko nje tuu

Nishasema polisi mnawasingizia. Lazima ujue wenye shida ni watanzania wenyewe. Katiba ni kitabu tuu ni kama gazeti la udaku au gazeti la mwananchi.
Ishu ipo kwa watu wameamua kuichukuliaje.

Huwezi kuliteja jeshi na wananchi wake. Huwezi.
Tabia zote za jeshi ni matokeo ya jamii husika.

Polisi au jeshi hata liwe milioni moja na silaha za namna yote halina uwezo wa kukabiliana na wananchi milioni 40 walioamua kudai jambo lao.

Watanzania tuache visingizio.

Ni kwamba sisi ndio tumezalisha jeshi unaloliona alafu tunatafuta wa kumlaumu
Sawa mkuu, naona hatutaelewana kwenye issue ya namna jeshi linavyofanya kazi.

Ila ukitaka jaribu kufuatilia hata hapo Kenya tu. Jeshi lazima liwe na vyombo independent vya kulidhibiti.
 
Nadhani Turnout ya kujiandikisha ilikuwa nzuri tu mkuu; nilipita sehemu kigamboni nilikuta msururu mrefu kinoma na wengine wakiondoka...

Pia vijijini kule watu wemgi tu wataenda kupiga kura: kuna maeneo machache ya mjini ndiyo yanaweza kuwa na shida...
Yes waliijiandikisha wengi sana Ili wapate vile vitambulisho. Vinatumika sana kwenye mikopo umiza/ kausha damu
 
Kwa hio utatoka kuandamana mkuu?
Organisers wenyewe wanapingana Maria Sarungi anasema maandamano yatakuwa ya kikatiba na ya AMANI Mange Kimambi anasema anataka kufanya Insurrection wanatuchanganya sana.
 
Kamati za mipango (planning committees)
Hizi kamati naona hazipo. Ukimfuatilia Mange Kimambi na Maria Sarungi ambao ndio vinara wa maandamano haya unagundua hawana kamati zozote zaidi ya vikao vyote vinafanyika mitandaoni na inakuwa live.
Kamati ndio msingi mkuu wa goo organization na mobilization ya maandamano haya. Kama hazipo atafanikiwa vipi? Embu msaidieni Mtibeli aelewe.
Maandamano halisi yanayotokana na vitendo vya muda mrefu vya kukoseshwa wa HAKI,kutendewa UONEVU na DHULUMA hayahitaji uwepo wa kamati ulizotaja ili ziratibu mipango physically on the ground ili kuwafanya watu washiriki maanadamano.
Kama kiwango cha uonevu na ukandamizwaji kimefikia kiwango cha kutovumilika kabisa...kiasi cha kufikia BOILING POINT mithili ya fukuto ya volcano iliyokaribia kulipuka,..kitendo cha kutaja siku na muda na mahali pa kukutania kwa ajili ya maandamano, bila kujali taarifa kuwafikia watu kwa njia ya electronic kama walivyofanya akina Mange Kimambi na Maria Sarungi, inatosha kulipua volcano ya hasira ya watu...na kushiriki maandamano; hakutakuwa na polisi wala jeshi la kuwazuia.

Kwa hiyo watu kushiriki au kutoshiriki maandamano yaliyotajwa tarehe 29,Oktoba hayatategemea uratibu wa kamati ili yafanyike,....yatategemea zaidi ukubwa wa mkandamizo wa hasira waliyonayo watu kutokana na hali wanayoipitia kuhusu yale uliyoyataja....yaani kuanzia ukiukwaji wa haki katika sheria za uchaguzi, ukosefu wa kiusalama kama ilivyo masuala ya utekwaji, ubadhirifu na rushwa serikalini na ukosefu wa ajira..n.k.

Kwa mfano, maandamano yote yaliyotokea nchi za Afrika kaskazini hayakuratibiwa kwa committees unazotaja.
Watu wa Tunisia walikuwa na fukuto la malalamiko mchanganyiko dhidi ya serikali ya Ben Ali..kuanzia ukosefu wa ajira, rushwa na upendeleo wa wazi kwa wanafamilia ya rais. Cheche iliyolipua maandamano ni muuza matunda mtaani aliyepigwa na kuporwa bidhaa zake na askari wa jiji..na kisha kisha kuamua kujichoma moto. Muda mchache baada ya hapo..baada ya video clip kusambaa watu wakawasiliana kupitia mitandao ya kijamii na kufanya maandamano.
Kule Misri, pamoja na kwamba chama cha Muslim Brotherhood kilikuwa kikiratibu maandamano mara kwa mara kupitia kamati zake,lakini walishindwa kuwaunganisha watu kushiriki maandamano.
Ilikuwa ni vijana,bila kamati...,waliopeana taarifa kupitia online media kama Twitter na FB waliofanya maandamano yaliyomng'oa Hosni Mubarak..kwa kitendo cha kutaja tu kwamba kesho yake wakutane Tahrir Square. Kwa vile kiwango cha fukuto la hasira dhidi ya serikali kilikuwa kikubwa,watu hawakujali uwingi wa polisi na jeshi uliozingira eneo la kukutana mapema kabla yao...lakini uwingi wa washiriki ukafanya askari wanywee.

Kwa Tanzania,kama fukuto la hasira ndani ya mioyo ya watu lingekuwa kubwa kiasi cha kutosha,..kitendo cha mzee Ali Kibao kuchomolewa ndani ya gari mchana kweupe, kisha kuuawa....kingetosha kuwa cheche kubwa ya kuanzisha maandamano ya nguvu kuiondoa ccm madarakani au kuilazimisha idikie mabadiliko yanayotakiwa na wananchi.
 
MAANDAMANAO YA 29OCT YATAFELI VIBAYA MAPEMA SANA KUTOKANA NA SABABU KUU ZIFUATAZO;

Anaandika, Robert Ng'apos Heriel
Mtibeli

1️⃣ Ukosefu wa Miundombinu ya Kiufanisi.

Maandamano makubwa yenye lengo la mabadiliko ya utawala yanahitaji:

a) Kamati za mipango (planning committees)
Hizi kamati naona hazipo. Ukimfuatilia Mange Kimambi na Maria Sarungi ambao ndio vinara wa maandamano haya unagundua hawana kamati zozote zaidi ya vikao vyote vinafanyika mitandaoni na inakuwa live.
Kamati ndio msingi mkuu wa goo organization na mobilization ya maandamano haya. Kama hazipo atafanikiwa vipi? Embu msaidieni Mtibeli aelewe.

b) Mfumo wa mawasiliano ulio salama,
Udukuzi, kufuatiliwa kuliko kupitiliza, usaliti wa mawasiliano ndani ya wenye nia ya kuandamana. Hayo yote yatakwamisha maandamano.

c) Mpangilio wa uongozi wa ngazi mbalimbali (national → regional → district → ward).
Unaweza kujiuliza kama wewe ni muandamanaji. Kwenye kata au mtaa wako kuna mfumo wowote wa kuyaratibu ili yatokee. Au ndio upo pekeako kwenye actual ground lakini mtandaoni ndio upo na na wenzako?
Tumia hiyo kama scale yako.

Mazingira ya Tanzania ya sasa, upinzani au wanaharakati wengi hawana mtandao thabiti wa ndani (grassroot network).
Hii inamaanisha hawana uwezo wa kuunganisha watu hata Laki moja kwa wakati mmoja bila kutambulika mapema.
Serikali inamiliki taasisi zote za mawasiliano, usalama, na inafanya doria usiku na mchana katika mitandao ya kijamii, hivyo hufahamu mipango kabla haijatekelezwa.
Kwa mantiki ya kiintelijensia, maandamano hayo yatakufa kabla hayajaanza, kwa sababu mpangilio wake utavujishwa na kusambaratishwa mapema.

2️⃣ Ukosefu wa Uratibu wa Malengo.

Maandamano yenye mafanikio lazima yawe na lengo moja linaloeleweka na kukubalika kitaifa.
Lakini maandamano haya yana malengo zaidivya moja yanayokinzana, mfano;

a). Kupinga uchaguzi,
b). Kuiondoa serikali iliyoko madarakani kumaanisha kuindoa CCM
c) Kupinga utekaji na mauaji. Wasiojulikana. Na sababu zingine.

Lengo la kwanza ni la kisiasa (kupinga uchaguzi)
lakini la pili ni la mapinduzi (kuiondoa serikali ya Samia madarakani) ambalo kisheria na kiusalama linachukuliwa kama uhaini au uasi.
Lengo la tatu ni la kijamii na haki za binadamu za msingi yaani haki ya kuishi. (Hili lingeunganisha watu wengi zaidi).

Hivyo, wapo wanaoamini wanapigania haki za uchaguzi, na wapo wanaoamini ni vita dhidi ya serikali. Na wapo wanaoamini wanatetea haki za binadamu za kuishi kwa waliotekwa na kuuawa na kutojulikana walipo.
Kukosekana kwa umoja wa tafsiri ya malengo kunafanya maandamano hayo yasifanane kihoja, kimkakati, wala kiitikadi, hivyo yatakosa mwelekeo mapema.

3️⃣ Udhaifu wa Uongozi wa Harakati.

Harakati yoyote ya kisiasa inahitaji:

a) Kiongozi mwenye karisma,
Najaribu kuangalia nani ni kiongozi aliyenyuma ya haya maandamano mwenye ushawishi. Kama ni Tundu Lisu yupo zake gerezani anapambana na kesi yake ya mchongo.

b) Mtu anayeaminika na umma,
Mwenye uwezo wa kujenga hadithi ya matumaini, hadithi zenye kuchochea chuki ya wananchi kwa serikali. Humphrey Polepole naye alitoa matumaini lakini amekamatwa dakika ya sabini ya mchezo kipindi cha pili.

Tanzania kwa sasa, licha ya kuwa na wanasiasa wa upinzani, hakuna kiongozi mmoja anayekubalika kitaifa kama sauti ya mabadiliko ya kweli.
Wengi wamechoka, wamegawanyika au wamo katika mikakati ya kisiasa ya muda mfupi. Na serikali inajaribu kila njia kuwavunja vunja na kuwagawanya kadiri inavyowezekana. Jana mumemwona Ezekiel Wenje. Ni kwamba wanawakatisha tamaa na kuwavunja moyo watanzania.

Bila kiongozi thabiti mwenye command structure, watu wanakuwa kama kundi lisilo na kichwa. Yaani kundi linajiendea endea bila mwelekeo. Hayatakuwa na tofauti na vuguvugu la Luddism kwa wale mliosoma Advance History 2.
Ndiyo maana kwa kitaalamu, maandamano kama haya huanza kwa makelele mitandaoni na kufa siku ya tukio. Haitakuwa mara ya kwanza.

4️⃣ Udhibiti Mkali wa Vyombo vya Usalama.

Kitaalamu, Tanzania ni nchi yenye mfumo wa ulinzi na usalama ulio wa kiintelijensia zaidi kuliko wa nguvu.
Taasisi kama:

I). TISS (Usalama wa Taifa),

ii) Jeshi la Polisi,

Iii) JWTZ (Jeshi la Wananchi)
Na vitengo vya cyber intelligence
vina uwezo mkubwa wa kutambua, kuvuruga, au kuzuia matukio kabla hayajafanyika.

Kwa mfano:

a) Mawasiliano ya Wapanga maandamano hufikiwa kupitia “surveillance”,

b) Viongozi wa maandamano hufuatiliwa kimyakimya,

c) Wengine huchukuliwa “preventive custody” kabla ya siku ya tukio.
Ndio hao unasikia kila siku wanakamatwa mara leo huyu kesho yule.
Wahamasisha maandamano mtandaoni au watu wenye mrengo huo nao huchukuliwa mapema kabisa kabla ya siku husika.
Mtu kama John Heche, John Mnyika, na wenzake hawawezi kuwa uraiani kufikia tarehe 29.

Watahifadhiwa kwa muda huku wakipewa usumbufu kidola mpaka upepo utakapotulia wataachiwa.

Hii inaondoa uwezekano wa maandamano kuanza kwa wingi au kwa ufanisi.
Kitaalamu, tunaita hii “preemptive disruption model” njia ambayo huzima uasi kabla haujaanza.

5️⃣ Hofu ya Kijamii.

Wengi wetu Watanzania ni watu wa amani tusiopenda vurugu, na tumelelewa kwenye misingi ya “amani ni bora kuliko vurugu, au funika kombe mwanaharamu. Apite".
Kisaikolojia, jamii imejengwa kuwa risk-averse (uepukaji wa hatari).
Hivyo, hata kama wanakubaliana kimoyomoyo na hoja za maandamano, wengi hawatashiriki hadharani.

a) Mfumo wa kiutamaduni, kiimani (dini), na kijamii unahimiza utii kwa mamlaka.
Wengi wataishia kusema “Mungu ataingilia” "Mungu atajibu", "tumuachie Mungu" au “Tusubiri uchaguzi mwingine”, hivyo kuua nguvu ya umoja wa kuandamana.

Kwa hivyo, uungwaji mkono utakuwa wa moyoni na mitandaoni lakini si wa miguu kwa mguu sako kwa bako. Watu wanakubaliana mtandaoni, lakini hawatokei barabarani.

6️⃣ Udhibiti wa Habari na Mitandao.

Serikali ina uwezo wa:

a) Kufunga mitandao ya kijamii.
Ikifunga mitandao wananchi wangapi wanauelewa wa kutumia VPN na mambo ya kidijitali. Wangapi?

b) Kudhibiti vyombo vya habari,
Media zote, redio zote, na wenye followers wengi watadhibitiwa iwe kinguvu au kwa kupewa pesa kuwatuliza
Si ndio yale mtaishia kumlaumu Millard Ayo wa watu. Atafanya nini?

c) Kuendesha kampeni za kupotosha

Vitengo vya propaganda kwa sasa vipo kazini: hakuna wakati vinatakiwa kufanya kazi kama wakati huu. Propaganda za kupotosha jamii mfano
“Maandamano yamehairishwa,”
“Viongozi wamekamatwa,”
“Maeneo fulani ni hatari.”
" Wanataka kuchafua nchi"
"Wanavuruga amani"
" Wanatumiwa na mabeberu"
" Watanzania ni waoga sana" hii pia ni. Propaganda iliyofanikiwa sana na ambayo kwa sasa watawala huipigia msumari ili iwe ni kama culture ya watanzania

Hii hufanya hata waliokuwa tayari kushiriki wakose maelekezo sahihi na motisha ya pamoja. Kwa mtazamo wa psychological operations (PSYOPS), hii ni silaha ya kisaikolojia inayotawanya umoja wa wanaharakati. Niliwaambia Saikolojia na soshiolojia ni msingi mkuu wa serikali kutawala watu.

Matokeo yake, maandamano hufa kabla ya saa sita mchana, na wale wachache waliotoka hukamatwa bila upinzani. Kisha baadaye watu huanza kulaumiana. Hoo hamjatoka. Nyie waoga n.k.

Kufikia hapa TaikonMaster sina la ziada. Nimejaribu kujadili. Kwa uhalisia na kwa kuzingatia siasa za nchi yetu, Saikolojia ambayo ninaifahamu kwa sehemu, intelijensia ambayo naifahamu kidunchu, na kwa kutumia falsafa (mantiki na hoja).
So kama utakuja kichwa kichwa na kutoa matusi yako sitaingilia uhuru wako na jinsi unavyoelewa mambo.

Nawatakia sikukuu njema ya Nyerere day.

Acha nipumzike sasa.

TaikonMaster
Kwa sasa Dar es salaam
Hatuhitaji hayo yote .Kwenye kata yangu nitaamana pekee yangu sihitaji mtu wapili Wala watu.

1.Nitaamka saa sita usiku tarehe 28.10.2025
-Nitablock njia zote pekee yangu
-Nitachoma mairi na kupiga paruti pekee yangu
-Wasimamizi wa uchaguzi(Walimu) hakuna atakaye toka nyumbani kwake
-Vituo vya KUPIGA kura vinavyoweza kuchomwa moto ,nitafanya hivyo pekee yangu
 
Gazeti hili kulisoma Hadi unilipe Hela si chini ya $130.

Na hapo Bado sitalimaliza.umeandika mbege tupu
 
Yaani Wapiga kura wasipojitokeza. Hata kama maandamano hayatafanyika tayari ni mafanikio makubwa sana.

Mpaka sasa Maza salamu keshazipata ndiyo maana unamuona akifanya makosa mengi mengi wakati wa Kampeni. Mambo yamemzidia kiasi kwamba anasahau sahau na kufanya mistake nyingi kwenye hotuba zake.
Ngoja tuone watafikia wapi
 
Organisers wenyewe wanapingana Maria Sarungi anasema maandamano yatakuwa ya kikatiba na ya AMANI Mange Kimambi anasema anataka kufanya Insurrection wanatuchanganya sana.
Nadhani wote wana lengo moja kuipambania Tanzania yetu irudi kwenye msingi wa haki unaozingatia sheria na utawala bora
 
Back
Top Bottom