Kwanini Levina Mukasa alijiua UDSM?

Huyo aliyesababisha kifo chake bila shaka ni mzazi kwa sasa na angependa binti yake aende kusoma mlimani na arudi salama. Atajisikiaje au atasingizia enzi za ujinga?
 
haaa ha nauli sh. moja!!!!!! Ablessed.....shkamoo dada
Marahaba mdogo wangu . Naona umeshangaa tulilipa shilingi moja na watu wazima walikua wanalipa shilingi tano au dala na ndipo jina la dala dala lilipozaliwa mpaka leo hata nauli ilipopanda bado waliendelea kuita dala dala.
 
aisee...sioni kitufe,pokea like
 
EMT kwa kweli umenikumbusha mbali. Those days PUNCH ilikua ni hatari kwa maisha ya chuoni. Rest in Peace Regina Mukasa.
 
Last edited by a moderator:
Marahaba mdogo wangu . Naona umeshangaa tulilipa shilingi moja na watu wazima walikua wanalipa shilingi tano au dala na ndipo jina la dala dala lilipozaliwa mpaka leo hata nauli ilipopanda bado waliendelea kuita dala dala.

heshima kwako dada
 
Duh EMT umenikumbusha mbali sana sana. Nakumbuka pia mbali ya 10 commandments of Mzee Punchi kulikuwa na Makundi Hasimu, moja ni hilo la Mzee Punch majority wakiwa wanafunzi wa Engineering has mwaka 3 na wa 4 na lile na ma-Hill Siders (Hapa akina magori wa NSSF, Mh. Lau Masha, Peter Makere etc na Mabebs wa nguvu wanahusika) Hili kundi la Hill Siders lilikuwa ni la Kishua zaidi waliojinadi wana mkwanja wanajua matanzi, kuvaa nk nk
 
Last edited by a moderator:
Ooh ! So sad ! Sipendi hata kukumbuka! Siku ya tukio nilitoka na girlfriend wangu (hakuwa mwanafunzi) kwenda kupata chakula cha jioni pale Savei. Tukiwa tunakula, Levina aliingia pale hotelini akaenda moja kwa moja kwenye bomba la maji. Alichukua glass akateka maji bombani. Sikumjali. Mimi na mpenzi wangu tuliendelea na chakula huku tukizungumza, ilikuwa majira ya saa 12 hivi jioni.
Baada ya kama dk 5 hivi niligeuka nikamuona Levina akifungua karatasi ya gazeti iliyofungwa akatoa vidonge na kumeza, akafungua nyingine akafanya hivyo hivyo na nyingine tena. Nilipoconcentrate kumuangalia, yule gf wangu alinigeuza kichwa na kuniuliza kulikoni namwangalia yule dada hivyo. Nikamwambia kuwa tulikuwa tunasoma naye na nilikuwa nashangaa kwa nini anameza vidonge vingi namna ile. Kisha nikatania, isije ikawa anataka kujiua maana nyie wanawake amkawii !!!

Levina alimaliza kumeza dawa, akatoka nje. Alikuwa amevaa khanga na kandambili huku nywele zake nyingi nyeusi zikiwa hazijachanwa vizuri. Jambo hili lilinishangaza kidogo maana Mzee Punch alikuwa haruhusu wanawake kuvaa mvao ule na kwenda mbali na mabweni yao.

Tulimaliza kula, nikarudi chuo nikaenda kujisomea baadaye nikalala. Asubuhi nakwenda cafeteria nakuta wanafunzi wamesimama makundi makundi kuuliza kulikoni naambiwa Levina amefariki kwa kumeza vidonge vingi vya Chloroquine. Nilipata mshituko ambao ulinifanya nikose raha hadi namaliza chuo kwani niliona sikuwa responsible enough kiasi cha kumfuata pale alipokuwa anameza dawa na kumuliza pengine angebadilisha uamuzi wake.

Hata hivyo, pengine ningekuwa peke yangu ningeweza kumfuata lakini kwa vile nilikuwa na gf wangu, kumfuata mwanamke mwingine tukiwa naye ingeweza kuwa issue labda kama ningekuwa na uhakika wa alichokuwa anakifanya Levina.

R.I.P Levina Mukasa, X B.A Ed class UDSM !!!
 
Marahaba mdogo wangu . Naona umeshangaa tulilipa shilingi moja na watu wazima walikua wanalipa shilingi tano au dala na ndipo jina la dala dala lilipozaliwa mpaka leo hata nauli ilipopanda bado waliendelea kuita dala dala.

Asishangae sana mshahara wenyewe ulikuwa shilingi elfu moja mia nne mpaka 1,800/- kwa aliemaliza degree, na ulikuwa wa kutosha kabisa. Noti kubwa kabisa ilikuwa ya shilingi mia.

Usidhani hiyo ni chee mimi mwenyewe nimeanza na huo.
 
Loh wewe uliiona live lazima hilo tukio ligande kichwani.
 
Dah! Mkuu.....umeniumiza sana ulipomtaja marehemu dkt. Masanja
 
Reactions: kns
Asishangae sana mshahara wenyewe ulikuwa shilingi elfu moja mia nne mpaka 1,800/- kwa aliemaliza degree, na ulikuwa wa kutosha kabisa. Noti kubwa kabisa ilikuwa ya shilingi mia.

Usidhani hiyo ni chee mimi mwenyewe nimeanza na huo.
Duh kumbe wewe mkubwa mwenzangu tumezeeka sasa.
 
Naamini inawezekana kufungua jalada upya kwa ajili ya upelelezi na kuwafikisha watuhumiwa wote mbele ya sheria. Ni muhimu hili likafanyika kwa kutenda haki kwa Levina na wale wote walio/wanaoonewa si tu na akina punch bali na wadhalilishaji wote ambao wamejazana kila kona ya nchi yetu. Tusipoungana tukamtetea Levina tutakuwa ni washirika wa mauaji yake na wenzake wengi ambao wanaweza kuwa hawajajiua lakini walikwishakuuawa na watesi wao.
 
Mbaya zaidi Huko Nigeria wanatumia hata uchawi na uganga ili wapate nguvu zaidi.
 
R.I.P Levina
Dah dunia hii sometymz bora ukutane na simba kuliko binadamu mwenzio.
 
Haaah! Yaani wewe akili yako inawaza mabebs tu?

Wale wabeba wawili wa kwenye ile dvd yako niaje bana? Wasalimie

Haaaa haaaa niaje Majomba? Of course bila Mabebs dunia ingepwaya.

Afu jana nilikuwa na Maxence na Lemutuz studio tukiongelea social media. Kipindi kinarushwa Sunday.

Si wakaniambia ulikuwepo Bongo? Inakuwaje JULIUS unafika Bongo hunitafuti?
 
Reactions: Ame
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…