Kwanini kulaumiana wanawake/wanaume katika suala la ndoa?

Kwanini kulaumiana wanawake/wanaume katika suala la ndoa?

Mtu hata hajaoa ashajijengea na wanaambiana kuwa wanawake ni lazima wanajisahau kwenye ndoa. Na mke akijisahau tu basi mchepuko ndo dawa yake. Sasa unategemea akiwa kwenye ndoa ataishije kama sio kuwa tu busy kungojea ile siku ya ahadi utakapojisahau akachepuke. Hayo mema yako anaya-overlook, anaamini ni ya muda tu yataisha na utajisahau sawasawa na imani yake

Hii ni kweli kabisa, I can imagine!!!
 
mjenga hoja umekuwa mbinafsi sana. Shida kuu katika mahusiano ni kuwa mke na mume hamuwezi kupendana sawa bin sawia. Yule anayependwa zaidi LAZIMA ARINGE. Hayo maringo ndo yanayoleta matatizo. Katika hoja yako umependela wamama, lakini kuna wanaume WANANYANYASIKA na ndoa zao usipime. Utawaonea huruma.
 
Looh ulivyo mwanga hivyo nijikute tu Nakwambia mambo yangu pyeeee

Hahahaaaaaa!! Khaaah kweli umekuwa jeuri, vipi ndio unanitafutia sababu nikufukuze kazi? Sema tu kuna wanaozitaka, maana ushanukia sasa naona umetoa miiba.
 
Hahahaaaaaa!! Khaaah kweli umekuwa jeuri, vipi ndio unanitafutia sababu nikufukuze kazi? Sema tu kuna wanaozitaka, maana ushanukia sasa naona umetoa miiba.
Me sijasema Sitaki kazi, ila ukiamua kunifukuza ni sawa tu hehheheehheh
 
Hii ni kweli kabisa, I can imagine!!!
Bora my kaka uwaambie hao wenzako ambao wanaconcentrate kuangalia mabaya tu. Tukiishi kwa kubebeana mapungufu, ndoa inaimarika zaidi.
 
Hahahaaaaa! My kaka yaani we acha tu, acheni kututegea tukosee jamani maana kukosea kupo na tutakosea tu, sasa tukikosea turekebishane na sio kusimangana na kutumia kama loop hole ya kutunyanyasa. Zile akili mlizoambiwa mzitumie ili mambo yaende sawa.

Ni kweli unachoongea sista, ujumbe unaniingia kweli kweli japo mapenzi ni very complex, siyo straight forward kama tunavyojadili hapa
 
Ndoa ni two way traffic.
Ndoa haileti shida pale mnapokuwa mnaendana kimtazamo.
Ndoa za siku hizi zinaanguka kwasababu wanawake wanakimbilia kuolewa na wanaume ambayo hawaendani.
Hawapati muda mzuri wa kufikiri na kufanya maamuzi thabiti.
Baadae mnakuja kugundua kuwa makosa yametendeka mpo ndani ya ndoa na hamuwezi kutoka.
Kwanin baadhi ya ndoa zinadumu na nyingine hazidumu?
Kwanin za wenzako zidumu na yako haidumu?
Mmekosea kuanzia kwenye kufanya maamuzi ya nani wa kuwaoa.

Sista atoto hao wanawake kwenye group lako wanaolialia khs ndoa zao, chanzo ni hapo kwa red. Fuatilia vizuri utaamini nachosema. Hata juzi wakati tunazungumzia ucha Mungu nimegusia khs wrong choices mnazofanya.

Kifupi msilaumu wanaume, laumuni maamuzi yenu mabovu mnayofanya wakati wa kuchagua mr right wako. I'm sorry to say this but wengi wenu mko blind sana wakati wa kufanya maamuzi nani akuoe. Hii ndo inayowakosti sana mkishaingia ndoani na mapenzi ya kuigiza kuisha. Waliofanya right decision wanaenjoy tu kwenye ndoa zao.

Mjue wanaume wote hatufanani kwa tabia, kuna magalasa kibao na kuna kete vile vile, hali kadhalika wanawake wote hamfanani kwa tabia, wapo wife material na wa kupotezia muda tu. So you have to play your role, usiende kichwa kichwa tu ukaambulia galasa, choose careful so you get the one you are compartible with. Maisha ya ndoani ni tofauti kabisa na maisha ya girlfriend na boyfriend ambayo kwa kiasi kikubwa yamejaa maigizo.

cc Heaven Sent
 
Last edited by a moderator:
Gelofriend unamchukulia poa RRONDO eeh!!! Ngoja nisiongee teh. Ila huyu ni half brod wake paulo so anajua vizuri tu kuhusu ndoa yangu na paulo, ananichokoza tuu

Paulo ni simu af huyu powerbank :wink:
 
Last edited by a moderator:
mjenga hoja umekuwa mbinafsi sana. Shida kuu katika mahusiano ni kuwa mke na mume hamuwezi kupendana sawa bin sawia. Yule anayependwa zaidi LAZIMA ARINGE. Hayo maringo ndo yanayoleta matatizo. Katika hoja yako umependela wamama, lakini kuna wanaume WANANYANYASIKA na ndoa zao usipime. Utawaonea huruma.

Sijapendelea walaaa, angalia utangulizi wangu nimesema kabisaaa nitaongelea upande mmoja kwasababu inaonekana sisi wanawake pekee ndio wenye shida, wanaume kamwee hamuoni wala hamkubali nafasi zenu ktk matatizo haya, na inakuwa kama mlitegemea kuoa malaika, na najua utakubaliana nami kuwa wanawake ni wahanga zaidi ktk hili.

Sasa kwa upande wa hao wanawake wachache wanaowanyanyasa waume zao, ukiachilia mbali mapungufu ya huyo mwanamke pia huyo mwanaume lazima anachangia tena kwa kiasi kikubwa tu, just be a man uone kama mwanamke atakunyanyasa, sasa kama hutaki kuwa mwanaume ndani ya nyumba what do you expect?


Hapo sasa ile "akili" mloambiwa muitumie inatakiwa ichukue nafasi yake kwa kiasi kikubwa mnooo(sio kuchepuka au kupiga) mwanamke atabaki kuwa mwanamke tuu hata iweje kwahiyo mwanaume kuwa mwanaume tu uone how easly these things goes.

Punguzeni kutulaumu, yatatueni matatizo yenu siyo kuyakimbia, Mungu hakukosea kuwaumba mwanzo then tukafuatia.

Mwanamke awe mama bora na mwanaume awe baba bora ili watoto wetu wawe image zetu.
 
Me sijasema Sitaki kazi, ila ukiamua kunifukuza ni sawa tu hehheheehheh

Teh teh teh teh, kila la kheri ktk hilo unalolichokonoa mama, ushavuka mto eeeh? Umejisahaaaau, angalia tu usijejisahau na huko uendako.
 
Ni kweli unachoongea sista, ujumbe unaniingia kweli kweli japo mapenzi ni very complex, siyo straight forward kama tunavyojadili hapa

Ni complex kwasababu tumeamua kuyafanya yawe complex, sisi tuliumbwa na utashi ili tukabiliane na mambo kama hayo.
 
mito my kaka,

Hivi kumbe choices zinafanywa na wanawake tu? Nyie hamna choices eti? Au ndio muendelezo wa kila baya ni la mwanamke? We all play part on this, nakumbuka uliongelea zaidi kuwa sisi wanawake huangalia pesa zaidi kama ndio kigezo kikuu cha kumpata mr right japo kweli mwanaume pesa(msinimeze jamani hata nyie mwajua hilo). Japo kuna waloolewa na mahohehae lkn cha moto wanakiona(maybe ni wrong chice pia au vinginevyo)

Na ktk hili huwa mnatulaumu sanaaaa kuwa huwa tunapata wrong choices kwasababu wanaume huwa mnaona kama sisi wanawake hatuna hisia wala vigezo vya kumpata mume, so yeyote aweza kuwa mume wa mwanamke yeyote,kama mwanaume ananipenda basi anatosha, jamani unakuta mwingine kweli anakupenda ila sasa hata uvute hisia za marehemu bado unakuwa hupati hisia nae, sasa ukiingia kwenye ndoa na mtu wa hivyo ndio yale utakuta unamuandaa mwanamke kuanzia asubuhi hadi jioni ila walaaaa hastuki(hii ni shida pia).

Na maneno kuwa "mnachagua sana" wakati kumbe mwajua kabisaaa kuwa kati yenu kuna magarasa pia kama ambavyo pia si wanawake wote ni wife materials, sasa jamani nijibebee tu mtu ilimradi mtu kwakuwa mwanamke sina choice, tukifika ndani tushindwane napo bado nilalamikiwe.

Kama ulivyosema kuwa waliofanya right choices wanaenjoy hii ni kwa both sides, maana nanyi huwa mnasema mwanamke sura tabia tutarekebishana, oooh mara sioi tabia, alafu ndani vikiharibika ndio unaanza kumlaumu mwanamke ana tabia mbaya wakati ulishasema tangu awali hauoi tabia, sasa sijui hii tabia unayoitaka sasa inatoka wapi.

Na kutokana na kusimangwa huku kwa wanawake ndio maana unaona wanawake huangukia mikononi mwa wrong choices, ilimradi tu aolewe nae aonekane ameolewa(big mistake) matokeo yake ndio hayaaa tunayoyaona sasa full tafrani.

Sote twapaswa kufanya chaguzi zilizo sahihi, sio mwanamke wala mwanaume.
 
Last edited by a moderator:
Kwani anayeapproachiwa nani sista atoto hadi uulize 'Hivi kumbe choices zinafanywa na wanawake tu?'

Nijuavyo mwanamke ndo anakusanya applications za wanaume mbalimbali then anachagua yupi mr right kwake. Sisi tunatuma applications, then wewe unatuassess kisha unachagua unayemtaka. So unapochagua garasa usimlaumu huyo uliyemchagua, bali jilaumu wewe kwa kuchagua mume hewa. Ndo point yangu hii.

So mi nabaki kukazia pale pale kwamba mnaishia kulia lia kwenye ndoa kwa sababu mnafanya wrong choice ya yupi akuoe. Ni kwa kutambua hili ndo maana enzi za mababu zetu wanawake walikuwa wanachaguliwa wenza. Wanajua wazi mwanamke ktk mahusiano ni myopic ndo maana anaishia kuchagua korona.

Kizazi chetu mmekataa habari za kuchaguliwa wenza. Hoja yenu ndo hii kama ulivyoiweka hapa "jamani unakuta mwingine kweli anakupenda ila sasa hata uvute hisia za marehemu bado unakuwa hupati hisia nae, sasa ukiingia kwenye ndoa na mtu wa hivyo ndio yale utakuta unamuandaa mwanamke kuanzia asubuhi hadi jioni ila walaaaa hastuki (hii ni shida pia).

Mmeachia uhuru wa kuchagua wenyewe mnaishia kuchagua magarasa. Sasa sijui hapo wa kumlaumu nani??!! Mkishaelewa chanzo cha tatizo mtaweza kuliepuka, lakini ukiendelea kuamini eti tatizo ni kwamba hampati ushirikiano wa wanaume ktk kutatua migogoro ya ndoa, bado hiyo short term solution ndg yangu.

Ushauri wangu kama nilivyosema siku ile ni kwamba m-review vigezo vyenu kwa mwanaume. Otherwise majanga yataendelea as there is no way wanaume wote wakafanana. Wewe ndo mwenye jukumu la kupick the mr right from the pool.
 
Last edited by a moderator:
Kwanin baadhi ya ndoa zinadumu na nyingine hazidumu?
Kwanin za wenzako zidumu na yako haidumu?
Mmekosea kuanzia kwenye kufanya maamuzi ya nani wa kuwaoa.

Hii mambo ya kujionyesha kwa watu ndo inawaponza watu. Yani mwanamke anaona bora avumilie matusi, vipigo, michepuko etc ili mradi tu huko nje waone "eh ndoa yao ina miaka ishirini. Safi sana "

Kwa nilichoshuhudia maishani mwangu hakuna mtu anayeweza kunidanganya kuhusu ndoa kudumu. Mtu huna furaha unaringia ndoa miaka ishirini.

Mapenzi ni two-way traffic. Nahisi inafikaga point wanachokana au ni kuwa tu hawakuwa wanaendana, jitihada zoote za kujipikilisha na kujirembesha na kujishusha zikibuma, ukijumlisha na mmoja kuwa na tabia za hovyo, basi anajiona kama anamfanyia mwenzake favor kubaki naye. Na isingekuwa kubanwa na dini wengi wangetoka tu.
 
Mna matatizo sasa kama Mimi tokea jana usiku mwanamke kanuna tu.nimempigia simu mchana bado kanuna sasa hapo unategemea nini.hapa napitia sehemu natulia nikirudi nacheza na mwanangu atajua mwenyewe.wanawake wasababisha mwanaume ajifunze mambo ambayo hakuwa nayo kabla.
 
mito unajua katika hili tunaweza kulaumiana hadi hasubuhi lakini bado suala linabaki pale pale kuwa huu ni mzigo wetu wote, kama mtaendelea kutulaumu hivi na kuona kuwa katika balaa hili nyie hamna cha kulaumiwa kwalo mnakosea sanaaaa, naweza nikawa nimekupima kwa vigezo vyangu nikakuona kuwa unastahili(kwakuwa awali ulipretend, and yo very good pretenders) na tukaingia ndoani ukatoa makucha, hili pia alaumiwe mwanamke?

Kumbuka tunatakiwa "tuoane" ili maisha yaende vyema, sasa kama mmejiandaa kupima mapungufu yetu tu na mwisho mje mtulaumu kuwa tulikosea kuwachagua, is this right? Sasa kwanini uliamua kuingia nami ndoani? Unaoa ili iweje? Hii ndio akili eti?

Ndio hiyo nilokuwa nikiongelea kuwa mwaona sie ndio wenye makosa tu, hivyo lawama zote ni kwetu,nyie malaika bwana.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom