Uzi ni mzuri sema sasa content yake haiendani na kichwa cha habari....katika kujadili kama kichwa cha mada kinavyosema kwa mtazamo wangu ipo hivi;Tukisimama katika misingi ya dini na mila kuwa mke ni muangalizi muhimu wa familia ndio maana lawama kwanza zinaenda kwa mwanamke moja kwa moja na mfano mzuri ni kuwa mtu anapopata maumivu huwa analia akisema mamaaa!!!!yaan ndio kimbilio la kwanza kama mtetezi wake,hiyo ni imani iliyopindukia ambayo MUNGU ameiweka kwa wanadamu ndio maana maandiko yanasisitiza MWANAMKE MWEMA NDANI YA NYUMBA ni THAMANI KUU,hajatajwa mwanaume makusudi,mwanaume amepewa majukumu yake ikiwa JUKUMU kuu nikuhakikisha kuwa familia yake inapata CHAKULA(mahitaji muhimu)...Sasa kwa ule UDHAIFU mkubwa wa mwanamke alionao(huu niwa asili/kuumbwa nao) ambao huwa na tabia yakuruhusu vitu/watu/mambo ya nje kuwa ndio WAAMUZI wake hupelekea kujiona ana mapungufu ya kimahitaji,ndio maana utaona hata hapa kuna mtu kachangia kasema "aliona mwanamke flan anapata mateso ambayo yeye asingeweza vumilia".....sasa hili ni mfano mmoja wapo wa tatizo kuu la mwanamke,anahitaji kila kinachofanyika sehemu flani AKIONA kinamvutia bila kuangalia hali halisi ya mahali alipo......Wanaume kwa asili yao ni watu wanaongozwa na ile hali yakumuamini mwanamke sasa inapotokea ile sehemu ambayo alikuwa anategemea ndio sahihi ikaenda wrong kidogo tu imani yao hushuka kwa haraka sana na pengine ni ngumu kurudi kama awali na ndipo utaona mtu anachepuka na mambo kama hayo,ndio maana utaona wanawake wengi waliingi katika mahusiano na wanaume ambao hawakujua ni waume za watu(walifichwa) ila ni ukweli kuwa wanaume wengi waliingia katika mahusiano na wanawake ambao walikuwa wanajua ni watu wa watu....Kwa hiyo UKWELI ni kuwa wanawake wengi hushauri wanawake wenzao jinsi yakuvunja ndoa/mahusiano ili hali wanaume wengi hushauri wanaume wenzao KUTAFUTA mchepuko kama njia mbadala yakutuliza akili wakat wanatafuta suluhisho la kudumu la tatizo.