Anonymous
Senior Member
- Apr 6, 2006
- 129
- 358
Habari wana JF,
Nimekuwa nikishuhudia sana tena kwa kiasi kikubwa mnoo kulaumia baina ya wanawake na wanaume katika suala zima la mausiano(ndoa),iwe ktk jamii huku tunakoishi au humu JF..
Wanawake huwalaumu wanaume na wanaume huwalaumu wanawake.
Sasa leo naomba niongelee lawama haswa za wanaume kwa wanawake,Wanaume huwalaumu kwa kiasi kikubwa zaidi wanawake na kuwaachia mabaya yote kuwa wao(wanawake) ndio huwa chanzo cha mivurugano mingi ktk mahusiano na ndoa kwa ujumla.
Mifano dhahiri ni humu ndani, endapo mwanaume ataleta uzi kuhusu tatizo ktk mahusiano yake lawama zoote humwagwa kwa wanawake(hasa wanaume), na watu huenda mbali zaidi na kutoa ushauri kama "achana naye asikusumbue wanawake ni wengi sana" na ushauri wa aina hii ndio huwa mwingi zaidi kutoka kwa wanaume.
Iwapo mwanamke atatoa uzi pia juu ya matatizo katika mahusiano yake basi wanaume wengi kwa kiasi kikubwa humuona huyo mwanamke ndiye mwenye matatizo yaliyopelekea mgongano au hata kuvunjika kwa mahusiano yake.
Utasikia "jichunguze wewe utakuwa ndiye mwenye tatizo"
Na wengine husema wanawake hujisahau sana ktk mahusiano na ndoa kwa ujumla, hivyo anapaswa kuwa mbunifu,mvumilivu,nk. Je wanaume hawajisahau? Au wao wamekamilika hawana tatizoblolote?
Jamani hivi mahusiano huwa ni ya mwanamke peke yake au mwanamke na mwanaume? Je mwanaume hapaswi kuwa mbunifu,mvumilivu,mwenye heshima,nk kwa mkewe/mpenziwe?Sisi sote ni binadamu,hatujakamilika, hivyo twapaswa kurekebishana, kusaidiana na kuvumiliana kwa yale ambayo hatujakamilika kwayo.
Hata mwanaume anapochepuka, husingizia kuwa "mwanamke ndiye chanzo" hawataki kabisa kukubali fault yao ktk suala hili, jamani sisi sio malaika na tuna mioyo yenye nyama kama yenu, kwanini kila lawama mtutupie ilihali nanyi mna mapungufu mengi tu tunayoyavumilia?
Wanawake kwa kiasi kikubwa nimeshuhudia wakishauriana sana juu ya "uvumilivu" na masuala mengine ambayo yataongezea chachu ktk mahusiano/ndoa zao, ila kwa upande wa wanaume hili ni nadra sana kulikuta, zaidi ya "achana naye" au "tafuta mchepuko" "mpuuze" je kweli hii ndio suluhisho pekee kwenu? Na wengine huenda mbali na kuona kuwa kuoa ni hisani tu kwa mwanamke!!
Na kadri muda unavyozidi kwenda ndio bala zaidi linaongezeka, mahusiano/ndoa walaaa hayana uzito tena, hivyo kupelekea hata kizazi tunachokitengeneza tunakilaumu wakati sisi ndio tumesababisha kiwe hivyo.Familia ndio base ya kila kitu, pakiharibika hapo basi hatutokuwa na jamii,taifa na dunia salama.
Play yo part men, hizi lawama ni zetu wote.
Karibuni kwa maoni na mafunzo zaidi ili tuweze kuwa na mahusiano yaliyo imara.
#peace#