Saa 7 mchana
JF-Expert Member
- Dec 30, 2018
- 6,563
- 13,024
Mkuu kamari ikifungwa sisi ma jobless tunaishije?Tanzania biashara ya kamari ni kubwa sana mpaka wacheza kamari wamekuwa kama Taaluma kabisa watu wanaojipatia kipato chao cha kudumu kupitia kamari wakijiita "wakamaria"
Ninavyofahamu kamari ni jambo haramu kwa dini zote mbili za Uislamu na Ukristo, kwa nini imeruhusiwa na haijapigwa marufuku kama ushoga ukizingatia kamari ni mbaya kuliko hata ushoga?
1. Ibara ya 3(1): Inaeleza kuwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni nchi ya kidemokrasia na ya kijamaa isiyokuwa na dini, yenye kufuata mfumo wa vyama vingi vya siasa.Kwani hii nchi inaendeshwa kidini kumbe?
Inaumika dini ipi kama mwongozo?
Ubaya wa kamari kwanza ni shughuli isiyoongeza thamani yoyote katika uchumi na taifa, inaharibu maisha ya vijana wengi kwa sababu inahitaji watu wengi wapoteze pesa ili wachache wapate pesa ndio hiyo biashara iweze kuendelea.Kwani ubaya wa kamari upo sehemu gani? Siku utakuja kusema kwamba Pombe ni mbaya hivyo serikali ifunge viwanda vyote?
Ubaya wa kitu inategemea mtazamo wako ,hata kitu ambacho wewe unaona ni kizuri na kinafaa mwingine anaweza kuona ni Kibaya.
Sasa umebet kwamba kwenye mechi ya leo mf Simba na mtibwa ,simba itashinda ukaweka elfu 10 na simba ikashinda ukalamba elfu 30 ,hapo umetenda dhambi gani? Je una tofauti gani na aliyenunua ndizi mkoani bukoba mkungu elfu 5 akaja kuuleta Dar akauuza kwa elfu 10? Je ikitokea ajali ndizi zikaharibika akala hasara ndiyo the same simba imefungwa mkeka umechanika.
Daa mkuu kumbe ww ni mweupe kichwan namna hiyo?Ubaya wa kamari kwanza ni shughuli isiyoongeza thamani yoyote katika uchumi na taifa, inaharibu maisha ya vijana wengi kwa sababu inahitaji watu wengi wapoteze pesa ili wachache wapate pesa ndio hiyo biashara iweze kuendelea.
Huwezi kufananisha kamari na biashara ya ndizi ambapo mkulima anapata kipato,muuza pembejeo anapata kipato, msafirishaji anapata kipato na watu wanapata chakula.
Katika hayo maelezo yangu hapo hakuna mahali nimetaja kodi kwa sababu kama ishu ni kodi biashara ya dawa za kulevya na umalaya zikiruhusiwa rasmi watu watalipa kodi nyingi kuliko hata hiyo ya kamari.Daa mkuu kumbe ww ni mweupe kichwan namna hiyo?
Ungejua wakamalia tunalipa kodi kubwa kuliko Ata uyo mkulima wa Ndizi unae muongelea apo
Kumbe hutumika kwenye baadhi ya mambo tu sio kwamba ni sheriaDini zote mbili huwa zinatumika kama muongozo kwenye mambo yanayoshabihiana mfano ushoga, kupiga marufuku biashara ya umalaya, abortion n.k
Wewe mkata viuno Bora sana wa Lumumba huachagi TU kudandia vitu virivyo juu yako? Mambo mengine yanazidi ukubwa mbalii sana usiyashobokee au unapenda unavyotukanwa? Wewe mkata viunoacha upotoshaji gentleman,
kamari hairuhusiwi Tanzania kwa mujibu wa sheria, unless una refer jambo jingine kabisa kwasababu ya uelewa wako mdogo eti kwamba hiyo ndio kamari.
kamari ni marufuku Tanzania na ni mchezo ulio kinyume cha sheria 🐒
Kwahiyo dini inaendeshwa kulingana na kiongozi aliyopo sio kwamba ni sheria?Angalia awamu za viongozi ...
Unajuaje kama wanaocheza siyo Sikh, Budha, Hindu, Shinto, Confucius, Tao ama Falun gong?Ninavyofahamu kamari ni jambo haramu kwa dini zote mbili za Uislamu na Ukristo,
Pombe nayo si inadaiwa ni dhambi na hizo dini unazozitaja, imepigwa marufuku?Mbona bangi imepigwa marufuku ?
Kwa mantiki hii inchi sio ya kidini sio?1. Ibara ya 3(1): Inaeleza kuwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni nchi ya kidemokrasia na ya kijamaa isiyokuwa na dini, yenye kufuata mfumo wa vyama vingi vya siasa.
2. Ibara ya 19(1): Inampa kila mtu uhuru wa mawazo, imani na uchaguzi katika mambo ya dini, pamoja na uhuru wa kubadilisha dini au imani yake.
3. Ibara ya 19(2): Inaeleza kuwa kutangaza dini, kufanya ibada na kueneza dini ni jambo huru na la hiari ya mtu binafsi, na shughuli za jumuiya za dini zitakuwa nje ya shughuli za mamlaka ya nchi.
Kwamba bongo ndio kuna hizo dini mbili pekee.Tanzania biashara ya kamari ni kubwa sana mpaka wacheza kamari wamekuwa kama Taaluma kabisa watu wanaojipatia kipato chao cha kudumu kupitia kamari wakijiita "wakamaria"
Ninavyofahamu kamari ni jambo haramu kwa dini zote mbili za Uislamu na Ukristo, kwa nini imeruhusiwa na haijapigwa marufuku kama ushoga ukizingatia kamari ni mbaya kuliko hata ushoga?