Kwanini JF ni tamu kuliko kazi?

Kwanini JF ni tamu kuliko kazi?

Bujibuji Simba Nyamaume

Platinum Member
Joined
Feb 4, 2009
Posts
79,037
Reaction score
168,677
Niko na jamaa yangu hapa ofisini, yeye daima hufika kazini saa kumi na mbili kamili akitokea nyumbani kwake Bunju. Huko sijui huwa anaondoka saa ngapi, lakini afikapo ofisini huingia JF na hujifungia humo hadi saa tatu kamili muda wetu wa kuanza kazi.

Muda wa lunch yeye haendi, huwa anaagiza chakula, hukaaa ofisini huku akiwa akiperuzi JF hadi saa nane kamili. Tutokapo ofisini saa kumi na moja, yeye hubaki ofisini akiperuzi JF hadi saa tatu usiku ndipo huanza safari ya kurudi home.

Humu ndani kuna watu yaani huwa hawabanduki kabisa jukwaani. Hivi kwanini JF imekuwa tamu kuliko kazi zituingiziazo kipato, na tamu kuliko familia zetu tuzipendazo sana?

Najua kuna watu humu, wakisha log in, hata wakisemeshwa na wapendwa wao (mke/mume au watoto) huwajibu vibaya wakiona kwamba wanawapunguzia utamu wa jamvi...
 
jimboni kumeshinda umeamua kuja jf? wamekukong'ori nini hukio nenda kachukue fomu ujaze kwa msimu ujao uenda ukakashinda tena ubunge chipukizi
 
Bujibuji.......umefunguliwa? Aisee welukam sana!

Jf ni gusa unase!!!
 
Last edited by a moderator:
Last edited by a moderator:
Last edited by a moderator:
Usiku (wa zile siku za uchuchaji nafaka) Nimepewa utaratibu , kabla sijaingia maperuzini , basi ni baada ya Tendo tukufu.
 
Usiku (wa zile siku za uchuchaji nafaka) Nimepewa utaratibu , kabla sijaingia maperuzini , basi ni baada ya Tendo tukufu.
 
Yaaani huyu faunda wa jf atakuwa kapaka servers na laptop yake asali...mi niko usingizini namuwaza paw......aaaah maxence udumu.....
 
jf ndio kila kitu mi na kifurushi changu cha mwezi uko facebook sijui twitter nilihama nimesahau hadi pass word .
 
Mama sosoliso nimekumissije? Nimekumbuka zile raha za mtaroni, hebu tujipange na mshirikina wetu Mtambuzi tukutane pale Legend Club LEO TUKO HAPA PUB

hata mie nimezikumbuka sana.....tena na vile sasa wewe ni ex-con hisia zangu zaniambia raha zitakuwa maradufujeee!
Ngoja niongee na Mtambuzi basi!
 
Last edited by a moderator:
jf udumu milele.
jamani mme nionea wapi my akanana Passion Lady.
 
Last edited by a moderator:
Jf ukishika unashikamana,sometimes unaiwaza kabisa


Jf tamu aisee
 
Hapa ni mahala ambapo tunazipunguza zile stress zetu na kuyajua yaliyojiri na yanayojiri nchini.
Nalog off
 
Back
Top Bottom