Rweyemam105
Senior Member
- Sep 8, 2012
- 100
- 135
NAS STORAGE SERVER
Hebu wazia NAS(Network Attached Storage) kama "Hard Disk" kubwa, yenye akili, na nguvu nyingi inayokaa nyumbani au ofisini kwako, lakini badala ya kuichomeka kwenye kompyuta kwa kebo/wire, unaunganisha kwenye intaneti au router yako (Wi-Fi).
Kifupi cha NAS ni Network Attached Storage (kwa Kiswahili: Kifaa cha Kuhifadhia Data Kilichounganishwa kwenye Mtandao).
Ili uelewe kwa urahisi kabisa, hebu tulinganishe NAS na vitu unavyovijua/fahamu:
───
Tofauti ya NAS na Flash au Hard Disk ya Kawaida.
• Hard Disk ya kawaida: Lazima uichomeke kwenye kompyuta yako kwa kebo/waya. Ukisahau kompyuta ofisini, huwezi kusoma mafaili yako ukiwa nyumbani. Vivyo hivyo ukkwa Ofisini, ukisahau PC yako ukiwa Ofisini hutoweza kuyafikia Mafaili yako. Na mtu mmoja tu ndiye anayeweza kuitumia kwa wakati mmoja.
• NAS Server: Inakaa chumbani au Ofisini kwako ikiwa imechomekwa kwenye Router ya Wi-Fi. Inawaka saa 24/7. Mtu yeyote wa familia au ofisini mwenye account ya ku log in, anaweza kuingia na kuweka(Upload/Download) au kuchukua mafaili yake kwa wakati mmoja akitumia kifaa kama simu, kompyuta, au tablet, hata kama yuko mkoani kwenye seminar au nje ya nchi training au matembezi (mradi ana intaneti).
───
■ Kazi Kubwa Zisizofahamika Sana za NAS (Kwanini Watu Wanazinunua?)
Ukiachilia mbali kuhifadhi ma-faili, NAS za sasa (kama hizi za UGREEN au SYNOLOGY) ni kama kompyuta kamili na inafanya kazi hizi kubwa:
■. Mbadala wa Google Drive/DropBox au iCloud Yako Binafsi (Bure Milele/Private Cloud)
Kila mwezi watu wanalipia Dropbox, Google cloud au Apple Cloud ili kupata nafasi ya ziada ya kutunza picha na docunents zao (GB 100 au TB 2). Ukiwa na NAS, unaiweka nyumbani/ofisini kwako, na picha zako zote za simu zinasafirishwa kwenda kwenye NAS yako kiotomatiki ukiwa kwenye Wi-Fi. Hulipii mtu yeyote kila mwezi na unaweza kuweka ukubwa wa diski unaotaka wewe (hadi TB 40).
■. "Netflix" Yako Binafsi ya Nyumbani (Media Server) PLEX/JELLYFIN/EMBY/KODI.
Unaweza kuweka Muvi, tamthilia (series), au nyimbo unazozipenda ndani ya NAS. Kisha ukiwasha TV yako sebuleni, iPad, au simu, unazifungua na kuziangalia moja kwa moja zikitokea kwenye NAS bila kutumia bando la intaneti (mradi uko kwenye Wi-Fi ya nyumbani/ofisni/Popote pale dunaini ulipo). NB: Kwa watu wa Apartments, AirBnB and Lodges, hapa ndio kwao. Kila mpangaji ataweza kuingia kwenye NAS kuangalia Movie/TV series zilizohifadhiwa kwenye NAS. Hata ukiwa nyumbani, kila mwenye PC/TV/iPad/Smartphone ataweza kuingia kwenye NAS na akaperuzi anachokitaka(Movies/data/Picha etc) bila ya mkwamo wowote.
■. Ofisi ya Pamoja (File Sharing & Collaboration)
Kama mna ofisi, badala ya wafanyakazi kutumiana ma-flash disk au kutumiana ma-email yenye mafaili makubwa, wote wanaingia kwenye NAS. Mhariri wa video, mhasibu, na katibu wote wanaweza kufanya kazi kwenye faili moja lililopo kwenye NAS kwa wakati mmoja bila mtandao kukwama.
■. Ulinzi wa Data Zako (RAID)
NAS nyingi zinakuwa na nafasi ya kuweka Hard Disk zaidi ya moja (kama diski 2, 4, 6 au hata 8). Zinasetiwa kwa namna ambayo diski moja iki-Corrupt au kuungua na kufa, data zako hazipotei hata kidogo! Unachomoa tu ile iliyokufa, unaweka mpya, na mtambo unajirudisha kwenye hali yake ya awali kwa usalama wa hali ya juu.
───
■. CCTV Backup. NAS inatumika ktk kunasa na kuhifadhi footprints za CCTV yako ya nyumbani au ofisini.
■. SPOTIFY yako binafsi. Kama unazo nyimbo zako pendwa kwenye simu/PC au flash, zihamishie kwenye NAS yako, Kisha kwenye simu yako download App ya FINAMP au JELLYFIN itakayo kusaidia kuzicheza nyimbo zako popote pale duniani ulipo kutokea kwenye NAS yako.
■. REMOTE ACCESS. Waweza kuifikia NAS yako ukiwa popote pale duniani kwa kutumia VPN maarufu duniani ambayo ni free bila malipo(Tailscale VPN) na ukaweza ku-access data na mafaili yako yote. Mfano. Niwapo nimesafiri kikazi, baada ya kazi, jioni, huwa napenda kuangalia TV Series ambazo nimehifadhi kwenye Nas yangu. Au kufungua baadhi ya Mafaili ambayo nimehifadhi kwenye NAS.
■. GOOGLE PHOTOS Replacement(IMMICH)
Kwa kupitia App ya "IMMICH" ni mbadala wa Google photos, ni App ambayo imeundwa kwa ustadi wa hali ya juu, na iko na AI ambayo ina uwezo wa kutambua sura za wanyama na vitu na mazingira. Wabobezi wa Picha wanaipa credit ya juu kuliko Google Photos App. Utaipenda ilivyo na mpangilio mzuri wa Picha zake.
■. VIRTUAL MACHINES(VM)
Kwa wale wataalam wa ICT, wanaotembea na flash zenye windows OS mbali mbali. Ukiwa na NAS, Utaweza ku-install windows mbali mbali na kuamua ipi utumie kwa wakati gani. Mfano, Binafsi, nimeweka Windows11, Ubuntu, ZorinOS, Proxmox, CacheOS. Linux Mint, Arch Linux & Fedora.
■. Ad blocker(Nertwork Ad blocker)
Wakati unatumia internet yako, huwa inaambatana na Matangazo mbali mbali, mfano wakati unaangalia Youtube lazima ukutane na matangazo huku ukiangalia video Youtube. Kupitia Apps kama Ad-guard na Pi hole, zitakusaidia ku block matangazo wakati unastream au kuperuzi mtandaoni, mara baada ya ku install mojawapo ya hizo Ad blocker tajwa hapo juu.
Kwa Ufupi:
NAS ni Wingu (Cloud) yako binafsi. Ndani yake kuna ulinzi wa data, ina kasi kubwa, haina gharama za kila mwezi, na inakupa mamlaka kamili ya kumiliki picha, video, na nyaraka zako zote bila kampuni kubwa ya teknolojia kukuchungulia au kukufungia akaunti yako.
Call: 0715 240 140