Kwanini iwe Watanzania vs Wakenya na si vinginevyo?

GoldDhahabu

JF-Expert Member
Apr 29, 2023
4,694
6,396
Humu jukwaani, kunapotokea ubishi wenye mwelekeo wa "Kimataifa", utaukuta ni baina ya Mkenya na Mtanzania.

Lakini inafahamika kuwa Jumuia ya Afrika Mashariki ina nchi kadhaa zaidi ya Kenya na Tanzania. Kwa nini ubishani wa kiutani uwe ni kati ya Mkenya na Mtanzania na siyo na Mtanzania na raia wa nchi zingine za East Africa?

Je! Inaweza ikawa,

1. Watanzania wanawahusudu Wakenya?

2. Wakenya wanawahusudu Watanzania?

3. Kwa sababu lugha kuu inayotumika humu jukwaani ni Kiswahili, lugha inayoongelewa zaidi Tanzania na Kenya?

4. Watanzania wanawaamini zaidi Wakenya kuliko wana Afrika Mashariki wengine?

5. Watanzania na Wakenya wana uasili wa karibu zaidi kuliko wengine?

Kwa nini imekuwa hivyo?
 
Tanzania na Kenya tunafanana zaidi kuliko Tanzania na uganda au na Rwanda na hao wengine, kuanzia lugha, vyakula, tamaduni, ufisadi serikalini (refer safari za viongozi wa nch nje ya nchi, hapa ila Kenya katupita mbali sanaaa)
 
Wewe ni mtumwa wa akili
Hili li inchi bado sana,
Acheni kujidanganya..
Maduka yote yamejaa bidhaa za Kenya....
Na haitotokea kamwe bidhaa za Bongo ziuzwe madukani Kenya, kwanza wanaziona ni low quality...
Wakati sisi huku unaomba kabisa kwa Mangi , "nipe ile panadol ya Kenya"..
1701729620086.png
 
Humu jukwaani, kunapotokea ubishi wenye mwelekeo wa "Kimataifa", utaukuta ni baina ya Mkenya na Mtanzania.

Lakini inafahamika kuwa Jumuia ya Afrika Mashariki ina nchi kadhaa zaidi ya Kenya na Tanzania. Kwa nini ubishani wa kiutani uwe ni kati ya Mkenya na Mtanzania na siyo na Mtanzania na raia wa nchi zingine za East Africa?

Je! Inaweza ikawa,

1. Watanzania wanawahusudu Wakenya?

2. Wakenya wanawahusudu Watanzania?

3. Kwa sababu lugha kuu inayotumika humu jukwaani ni Kiswahili, lugha inayoongelewa zaidi Tanzania na Kenya?

4. Watanzania wanawaamini zaidi Wakenya kuliko wana Afrika Mashariki wengine?

5. Watanzania na Wakenya wana uasili wa karibu zaidi kuliko wengine?

Kwa nini imekuwa hivyo?
Namba 5
Watani wa jadi.
Zingatia Mwalimu na Kenyata Sr. Walikuwa wanapa lile Jani pamoja.
 
Tanzania na Kenya tunafanana zaidi kuliko Tanzania na uganda au na Rwanda na hao wengine, kuanzia lugha, vyakula, tamaduni, ufisadi serikalini (refer safari za viongozi wa nch nje ya nchi, hapa ila Kenya katupita mbali sanaaa)
Mkuu, hujaitaja Demokrasia!
 
Back
Top Bottom