Kwanini Watanzania hawapendi kusafiri?

GoldDhahabu

JF-Expert Member
Apr 29, 2023
4,695
6,398
Mwanamke aitwaye Cassandra de Pecol kutoka Connecticut, alifanikisha ndoto yake ya kutembelea nchi zote duniani, 193,
akiwa na umri wa miaka ishirini na saba.

Mpaka anafikisha miaka 18, Canada ndiyo nchi pekee aliyokuwa amefika, tena, ni kwa vile mama yake anatokea huko. Sababu kubwa iliyomfanya asisafiri akiwa mdogo ni uwezo mdogo wa kifedha.

Kufanikiwa kwake kuzitembelea nchi 193 ni jitihada zake binafsi. Anavyoonekana si tajiri, ila anapenda kusafiri. Lakini kuna Watanzania ambao pengine wana uwezo mkubwa kifedha kumzidi yeye lakini bado hawasafiri.

Ukizilinganisha nchi za Afrika Mashariki, hasa Kenya, Uganda, na Rwanda, Watanzania ndiyo wanaoongoza kwa kutokusafiri kwenda nchi zingine. Kwa nini hivyo?

1. Umaskini?

2. Lugha?

3. Ugumu wa upatikanaji wa passport?

4. Ushamba?

5. Utamaduni?

Sababu ni nini?
 
Iko hivi ukiangalia wazungu wengi ni watu ambao wanafanya sana saving hata wenye vipato vya kawaida.

Wanaweza saving kwakuwa kwanza kiwango cha utegemezi kwao ni kidogo sana. Yani utakuta baba na mama wana mtoto mmoja au hawana na hamna mtu anaewaomba hela.

Hakuna sijui michango ya ukoo, sijui mtoto wa mjomba ada shule, mara rafiki anaoa, mara bibi anaumwa n.k

Birth control imesaidia wenzetu sana. Sisi huku mtu ana ndugu zaidi ya laki na akipata tu ka ajira ka kulipwa laki saba basi kila mtu anamtolea macho, vizinga visivyoisha.

Huyo mtu ata save sangapi ili aweze kutembelea nchi mbalimbali?

Kingine kwa wenzetu wa nje huko wengi wanakula generational wealth. Yani mtu anazaliwa anakuta familia iko well-off kuanzia vizazi kadhaa vilivyopita. So yeye anaendeleza kutengeneza hela tu na future ya kizazi chake so mambo kama kusafiri ni kawaida tu.

Chamwisho ni nchi yetu hii ina mifumo ya ajabu sana. Mtu kumiliki passport tu inaonekana kama vile ni jambo la ajabu sana. Ukienda uhamiaji kutaka passport inakuwa ni mchakato mgumu utadhani unataka kwenda mbinguni.

Nchi za wenzetu kuwa na passport ni kawaida na kila raia anayo kama document muhimu. Hapa kwetu passport inachukuliwa tofauti sijui kwanini CCM hawataki raia wamiliki passport?
 
Tanzania ni nchi bora sana duniani. Ukisafiri mikoani inatosha kupata kile ambacho ungekipata duniani kote.

Pia teknolijia ya sasa unaweza kwenda popote, kuonge na yeyote duniani ukiwa kijijini sitimbi na internet. Hata kuagizs chochote.

Kama huridhiki na nchi yako utakuwa unatamani kusafirisafiri hovyo.
 
Lakini kuna Watanzania ambao pengine wana uwezo mkubwa kifedha kumzidi yeye lakini bado hawasafiri.

Kupenda kusafiri ni hobby mkuu, si kila mwenye uwezo ni mpenzi wa kufanya hivyo...

Thamani ndogo ya shilingi ya kitanzania kulinganisha na sarafu ya nchi nyingine nyingi, inalazimu uwe na "madafu" mengi kuweza kukufikisha ughaibuni huko...
 
Back
Top Bottom