Kwanini Israel inapewa msaada wa kijeshi/ silaha na Marekani?

Kwanini Israel inapewa msaada wa kijeshi/ silaha na Marekani?

View attachment 2975991

Bila msaada wa USA nchi kama Russia, China leo zisingekuwepo

Ila wafuasi wa Russia na China wanabonga sana utadhani hawajawahi kupewa msaada.

Bila USA kuingia Vita ya pili na kuseama akae kwa kukutilia Uingereza inge surrender, Russia na china wangekula vipigo vya mbwa koko
Hamna kitu kama hicho kwanza wakati wa hiyo vita China alikua bado sana anajitafuta hakua hata miongoni mwa mataifa yaliyokua yameamua kupigana upande gani.
 
Hqmna kitu kama hicho kwanza wakati wa hiyo China alikua bado sana anajitafuta hakua hata miongoni mwa mataifa yaliyokua yameamua kupigana upande gani.
This is the reason Jamiiforumns ni tofauti na forums kama Quora.

Yaani hata kusoma tu WWII in pacific inakushinda, yaani hata kufatilia why Korea is devided unashindwa kufatilia
 
This is the reason Jamiiforumns ni tofauti na forums kama Quora.

Yaani hata kusoma tu WWII in pacific inakushinda, yaani hata kufatilia why Korea is devided unashindwa kufatilia
Ukifuatilia wewe inatosha siyo lazima wote tufuatilie.
 
Mbona hata Ukraine wanapata msaada wa pesa nyingi tu na silaha kutoka marekani?

Mengine porojo tu kubwa ni mwendelezo wa marekani kupitia huyo kibaraka wake hapo Middle East kuendelea kutaka kuitawala dunia ila mambo yanakwenda kubadilika haraka sana. Mataifa Kama urusi, China na Iran yanaongoza mapambano ya kuvunja huo mwiko.
Ukraine ni nchi tajiri?
 
Hii akili ya kusema waisraeli wana akili sana ya kutengeneza silaha kwahiyo marekani anawategemea ni uwongo mtupu. Silaha za N.korea ni muisraeli anatengeneza? Iran, China , Russia nao wanatengenezewa na hao waisraeli? Acha kuleta propaganda zisizo na kichwa wala miguu marekani lazima aisaidie Israeli kwasababu ndio alioitengeneza Tarehe 14 May 1948
Sio kweli, ndani ya Russia kuna jamii ya waisraeli wako kwenye fani mbalimbali hasa ktk sayansi na teknologia na Urusi inawategemea mno na hilo liko wazi kabisa na anayepinga hilo basi ni udini tu unamsumbua.

Hizo nchi zingine kama sijui China, Korea Kz na Iran hazina lolote kabisa kiteknolojia ila ni kupiga tu chabo kwa wajuzi ndipo watengeneze bidhaa zao feki.
 
Wewe acha uongo wako tutajie hiyo jamii ya waisraeli inayotegemewa na urusi kwenye Teknolojia peleka umbea huko.
Halafu kuhusu teknolojia kuanza nchi kama za China , Iran na Korea nyamaza maana ndio hao wanaowajambisha waisraeli hivi sasa.
 
Ísrael ni watch dog wa mataifa ya magharibi, limetengenezwa kimkakati hata wale wayahudi wenyewe asili ambayo hawakuwahi kwenda nje ya palestina wana msemo kuwa WALIPOKUJA HAO NDIPO TUKAANZA KUGOMBANA NA MAJIRANI ZETU kumbe wao Kwa miaka maelfu walikuwa wanaishi na waparestina kama ndugu ila lilipo Anza vuguvugu la wazungu (wayahudi wakiimani )kuhamia humor NDIPO vurugu zikaanza
 
Urusi iwe sehemu ya ujerumani!!¡!!!!
Ujerumani walipiga Ulaya yote.

Walishindwa kuivamia Uingereza sababu ya Jeshi la anga na Uingereza.

Mwaka 1941 Ujerumani wakahamia upande wa Russia walipiga pote Hadi wakafika miles 18 kutoka Kremlin, sawa na kutoka Gongo la Mboto Hadi Posta.

Wakati huo Ujerumani alikuwa anapigana sehemu mbili West na East na kuhakikisha analinda fukwe zote za Ulaya has Ufaransa.

Sasa take alternative thoughts. Ujerumani asingelazimika kupeleka Jeshi Mashariki na Magharibi, akafocus effort zake zote Upande wa Russia, na Russia asingepokea misaada ya Lend lease.

Ndio maana Hadi Leo Russia hawataki kambi za NATO Zikae karibu yake
 
Wengi umu mtakuwa hamjui ila waisrael ambao ni raia wa Marekani ni wengi kuliko waisrael wanaoishi israel.Na ndio wanao wamiliki wa media ,mabank na teknolojia toka zamani hauwezi kuwa rais wa Marekani kama hujasupport Israel kwenye kampeni ndio masponsa wakubwa wanachangia kote kote
 
Ukiachana na USA & china ni nchi gani nyingine duniani haipokei silaha kutoka nchi nyingine?
China imetumia silaha nyingi za Russia hata technology za kijeshi walitoa huko kutengeneza ndege na silah zingine kabla hawajajiongeza
 
Wengi umu mtakuwa hamjui ila waisrael ambao ni raia wa Marekani ni wengi kuliko waisrael wanaoishi israel.Na ndio wanao wamiliki wa media ,mabank na teknolojia toka zamani hauwezi kuwa rais wa Marekani kama hujasupport Israel kwenye kampeni ndio masponsa wakubwa wanachangia kote kote
Naona Kuna shida ya kutofautisha kati ya 'Waisrael' na 'Wayahudi'!
 
Katika mambo ambayo yamekuwa yakieleweka vibaya, kukanganya na pia kuzua dhihaka kutoka kwa watu wasioipenda Israel ni pamoja na hili la kupewa misaada wa jeshi/ silaha na Marekani pamoja na kuwa ni nchi tajiri iliyoendelea.

Ni vizuri tujifunze na kuelewa mambo bila ushabiki, kuna sababu kadhaa muhimu Israel kupewa msaada na Marekani.

1. Kwanza karibia nchi zote duniani ikiwemo US huwa kwa kiasi fulani zinajiendesha kwa mikopo, kwa hiyo ikitokea unaweza kupata pesa za bure sehemu nyingine ni jambo la kufurahia na huwezi kuzikataa kwa sababu inakuwa umeepushwa kukopa na kuingia madeni. Israel wataendelea kuzipokea na kuzifurahia pesa za bure za US na Ulaya.

2. Taasisi za ushawashi za kutetea maslahi ya Israel "Jewish/ Israel lobby" huko Marekani ni mahiri sana, zenye ushawashi mkubwa kwa jamii kubwa ya Wamarekani na zinajua kusuka mipango na mikakati kupitia wanasiasa wa Marekani kuipatia Israel pesa. Wanaweza kushawishi matajiri kutofadhili kampeni za uchaguzi za baadhi ya wanasiasa wasiowakubali au kufadhili kampeni za wapinzani.

3. Marekani ni kama Inawalipa Israel zaidi badala ya msaada. Pesa inazowapa Israel ni zaidi ya msaada kwa sababu ina usemi na maamuzi makubwa katika biashara ya silaha ya Israel. Waisrael ni watu wenye akili sana kiteknolojia na wanaweza kushindana vikali na Marekani vikali katika utengenezaji wa Silaha za hali ya juu za kila aina. Wamarekani wasingependa kuona ushindani wa aina hiyo utakaopunguza faida kwa kampuni zao na pia hata kupelekea baadhi ya silaha kuangukia mikononi mwa adui zake kama Israel itaachwa huru kuuza vyovyote katika hiyo biashara na pia ikiwemo wanasayansi wake kununuliwa au kufadhiliwa na mahasimu kama Urusi, hiyo inayoitwa msaada ni sehemu ya gharama hiyo kuepusha hayo yasitokee.

4. Marekani inadumisha mshirika wa uhakika wa Mashariki ya kati. Katika Mataifa mengine yote ya Mashariki ya kati ambayo ni washirika wa Marekani Israel peke yake ndio haitegemewi kubadilika kuwa kinyume au adui wa Marekani wakati wowote.

5. Udini, Ukristo ulianzia Israel. Hii japo sio sababu ya msingi sana ila kuna Wamarekani wengi ambo wengine wako kwenye vyombo vya maamuzi wanaiona Israel ni sehemu muhimu katika dini yao.

6. Tamaduni na tunu(values) zinazoshabihiana kati ya Israel na West. Israel ni demokrasia imara yenye kuzingatia uhuru wa raia wake na uchumi unaoeendeshwa na soko. Hakuna nchi nyingine ya Mashariki ya kati inayokaribiana na West kama Israel.

7. Kujisikia vibaya "Guilty feeling" ya US/West kutokana na mauaji ya kiyahudi "holocaust" yaliyofanywa na Ujerumani pamoja na washirika wake kuelekea vita vya pili vya dunia. US na mataifa mengine kama Uingereza yanajiona hayakuwajibika vya kutosha wakati huo kupunguza au kuepusha kabisa.
Israel & Saudi Arabia ni nchi zenye ushawishi mkubwa mashariki ya Kati na ata duniani Kwa ujumla. Kwaiyo marekani anatumia hizo nchi mbili kama watch dogs wa Maslai yake na ndio maana licha ya vurugu zote za hamas Saudia ni kama anasita kuonesha msimamo wake...! Wote ni machawa WA marekani...! Kwa namna yoyote marekani lazima atalinda Maslai yake kwenye hizo nchi.
 
Sio kweli, ndani ya Russia kuna jamii ya waisraeli wako kwenye fani mbalimbali hasa ktk sayansi na teknologia na Urusi inawategemea mno na hilo liko wazi kabisa na anayepinga hilo basi ni udini tu unamsumbua.

Hizo nchi zingine kama sijui China, Korea Kz na Iran hazina lolote kabisa kiteknolojia ila ni kupiga tu chabo kwa wajuzi ndipo watengeneze bidhaa zao feki.
Achana na hizo fikra..! Tumekuwa nunaaminishwa kuhusu ilo Kwa mda sasa.! Ila ukweli 95% ya silaha za maangamizi za Israel zimeundwa Kwa ushirikiano baina ya ya Israel na mataifa mengine mfano Iron dome imeundwa Kwa ushirikiano wa Israel & marekani. Ukiwa na fikra hizo utasema pia wafrika hawana akili
 
Huo ndio ukweli na dunia nzima
inafahamu hilo sasa unaweza tu ukapinga kwa sababu za kidini lakini haibadilishi huo ukweli.
 
Back
Top Bottom