Kwanini Israel inapewa msaada wa kijeshi/ silaha na Marekani?

Kwanini Israel inapewa msaada wa kijeshi/ silaha na Marekani?

Hii akili ya kusema waisraeli wana akili sana ya kutengeneza silaha kwahiyo marekani anawategemea ni uwongo mtupu. Silaha za N.korea ni muisraeli anatengeneza? Iran, China , Russia nao wanatengenezewa na hao waisraeli? Acha kuleta propaganda zisizo na kichwa wala miguu marekani lazima aisaidie Israeli kwasababu ndio alioitengeneza Tarehe 14 May 1948
 
Ushahidi huo hapo.
 

Attachments

  • Screenshot_20240428_094127_Google.jpg
    Screenshot_20240428_094127_Google.jpg
    222.5 KB · Views: 15
Kinalindaje maslahi ya marekani embu fafanua?
Nenda kwenye mtandao wa BBC utafute makala moja yenye kichwa cha habari kinachosomeka hivi:Nini chanzo cha ushirika usiyo yumba kati ya Nchi za Magharibi na Israel,bila shaka utajifunza mengi.
 
Kwani israel ikipewa misaada na marekani nyie wafia dini inawauma nini ? Kwani ni pesa zenu mmechangishwa huko misikitini ? Mbona mnauchungu na pesa za marekani ila hamna uchungu na pesa za iran kusaidia magaidi wa hezbollah na hamas kufanya ugaidi
Huna akili hakuna anaye umia bali watu huwa wanawaelimisha nyinyi warokole uchwara mnadhani kuwa Israel ana weza kila kitu.
 
Sasa hicho kijitaasisi wao si ndo wamiliki na ndio maana wanakitengea bajeti ya kutosha?
yaani kiufupi tuseme Israel ni base kubwa ya kijeshi na kijasusi ya Marekani iliyo jificha kwenye sura ya nchi.
Sawa ilimradi inasaidia kupambana na ugaidi na kuifanya dunia iwe mahali salama
 
niwakumbushe tu bila misaada ya silaha za Marekani, Urusi ingekuwa sehemu ya Ujerumani, China ingekuwa Mali ya Japan
 
Katika mambo ambayo yamekuwa yakieleweka vibaya, kukanganya na pia kuzua dhihaka kutoka kwa watu wasioipenda Israel ni pamoja na hili la kupewa misaada wa jeshi/ silaha na Marekani pamoja na kuwa ni nchi tajiri iliyoendelea.

Ni vizuri tujifunze na kuelewa mambo bila ushabiki, kuna sababu kadhaa muhimu Israel kupewa msaada na Marekani.

1. Kwanza karibia nchi zote duniani ikiwemo US huwa kwa kiasi fulani zinajiendesha kwa mikopo, kwa hiyo ikitokea unaweza kupata pesa za bure sehemu nyingine ni jambo la kufurahia na huwezi kuzikataa kwa sababu inakuwa umeepushwa kukopa na kuingia madeni. Israel wataendelea kuzipokea na kuzifurahia pesa za bure za US na Ulaya.

2. Taasisi za ushawashi za kutetea maslahi ya Israel "Jewish/ Israel lobby" huko Marekani ni mahiri sana, zenye ushawashi mkubwa kwa jamii kubwa ya Wamarekani na zinajua kusuka mipango na mikakati kupitia wanasiasa wa Marekani kuipatia Israel pesa. Wanaweza kushawishi matajiri kutofadhili kampeni za uchaguzi za baadhi ya wanasiasa wasiowakubali au kufadhili kampeni za wapinzani.

3. Marekani ni kama Inawalipa Israel zaidi badala ya msaada. Pesa inazowapa Israel ni zaidi ya msaada kwa sababu ina usemi na maamuzi makubwa katika biashara ya silaha ya Israel. Waisrael ni watu wenye akili sana kiteknolojia na wanaweza kushindana vikali na Marekani vikali katika utengenezaji wa Silaha za hali ya juu za kila aina. Wamarekani wasingependa kuona ushindani wa aina hiyo utakaopunguza faida kwa kampuni zao na pia hata kupelekea baadhi ya silaha kuangukia mikononi mwa adui zake kama Israel itaachwa huru kuuza vyovyote katika hiyo biashara na pia ikiwemo wanasayansi wake kununuliwa au kufadhiliwa na mahasimu kama Urusi, hiyo inayoitwa msaada ni sehemu ya gharama hiyo kuepusha hayo yasitokee.

4. Marekani inadumisha mshirika wa uhakika wa Mashariki ya kati. Katika Mataifa mengine yote ya Mashariki ya kati ambayo ni washirika wa Marekani Israel peke yake ndio haitegemewi kubadilika kuwa kinyume au adui wa Marekani wakati wowote.

5. Udini, Ukristo ulianzia Israel. Hii japo sio sababu ya msingi sana ila kuna Wamarekani wengi ambo wengine wako kwenye vyombo vya maamuzi wanaiona Israel ni sehemu muhimu katika dini yao.

6. Tamaduni na tunu(values) zinazoshabihiana kati ya Israel na West. Israel ni demokrasia imara yenye kuzingatia uhuru wa raia wake na uchumi unaoeendeshwa na soko. Hakuna nchi nyingine ya Mashariki ya kati inayokaribiana na West kama Israel.

7. Kujisikia vibaya "Guilty feeling" ya US/West kutokana na mauaji ya kiyahudi "holocaust" yaliyofanywa na Ujerumani pamoja na washirika wake kuelekea vita vya pili vya dunia. US na mataifa mengine kama Uingereza yanajiona hayakuwajibika vya kutosha wakati huo kupunguza au kuepusha kabisa.
Uskute unaongea vitu kiushabiki
 
niwakumbushe tu bila misaada ya silaha za Marekani, Urusi ingekuwa sehemu ya Ujerumani, China ingekuwa Mali ya Japan
Marekani aliingilia vita ya dunia mwishoni na aliingia kusaidia Uingereza na ufaransa . Walikua pamoja na Urusi kwakuwa walikua wanapambana na adui mmoja lakini baada ya vita Marekani alizikumbatia nchi zote za ulaya na kuunda ushirika Urusi alikataa na hajawahi kupokea msaada wa silaha kutoka marekani. Kama una ushahidi lete hapa.
 
Hakuna inchi inaitwa Israel, hiyo Israel unaoijua wewe ni kundi la majambazi wakimarekani na Uingereza ambao waliletwa hapo Kwa madhumuni ya kulifanya eneo la mashariki ya kati lisitulie lengo likiwa kuzivuruga nchi zenye nguvu kama Iran, Saudia, Syria na Egypt zisipae kiuchumi na kuleta ushindani Kwa West kupitia Uchumi wa MAFUTA.
Israel ni jina tu kiufupi ni wafaransa, Britons na USA. Hawa wazayuni walipewa sifa na nguvu nyingi za kimalaika Ili kuwanasibisha na WA Israel wa kwenye biblia, lakini muda unavyozidi kwenda wanazidi kuumbuka.
Shambulizi la HAMAS la October 7 ni jibu Tosha kuwa waisraeli wa kwenye biblia sio Hawa wanaokalia maeneo ya Palestine.
 
Marekani aliingilia vita ya dunia mwishoni na aliingia kusaidia Uingereza na ufaransa . Walikua pamoja na Urusi kwakuwa walikua wanapambana na adui mmoja lakini baada ya vita Marekani alizikumbatia nchi zote za ulaya na kuunda ushirika Urusi alikataa na hajawahi kupokea msaada wa silaha kutoka marekani. Kama una ushahidi lete hapa.
 
Screenshot 2024-04-28 103831.png


Bila msaada wa USA nchi kama Russia, China leo zisingekuwepo

Ila wafuasi wa Russia na China wanabonga sana utadhani hawajawahi kupewa msaada.

Bila USA kuingia Vita ya pili na kuseama akae kwa kukutilia Uingereza inge surrender, Russia na china wangekula vipigo vya mbwa koko
 
Back
Top Bottom