Kwenye suala hili kuna ukweli ndani yake haswa kwa HTC ONE M series kuanzia M7, M8 na baadhi ya HTC Desire models ambazo zinakabiliwa na tatizo la Pink au Blue tint hasa ukipiga picha sehemu zenye mwanga mdogo. HTC walitoa taarifa kuhusu tatizo hili wakisema kuwa sababu ilikua ni camera sensor waliotumia.
Kwa upande mwingine kwa mfano TECNO kufifia kwa ubora wa picha sababu ni ubora mdogo wa Camera lid (kile kioo pale kwenye sensor ya camera) ambavyo kutokana na udhaifu wa utengenezaji kioo kile huwa kinaruhusu hewa, vumbi kuingia kwenye jicho la kamera hivyo kupelekea picha kuwa hafifu na mara nyingi vioo hivi vinakwaruzika kirahisi sana hivyo kuzuia lens kuona mwanga katika ubora wake.
Kumbuka kwamba camera lens za kwenye simu ni ndogo sana hivyo basi vumbi au umande kidogo tu unatosha kuifanya camera kupoteza uwezo wake wa kutoa picha angavu.
CHA KUFANYA, unapopata simu yako nunua case nzuri na pia zingatia matunzo na usafi wa simu yako na mazingira unayoweka simu yako. Simu yeyote inahitaji matunzo ili idumu kwa muda iwe ni ya bei ghali kama iPhone 7, Galaxy S7 au ya bei nafuu kama Tecno Y3 zote hizi zinahitaji matunzo na usafi.