Kwanini hatupendi kuwaomba ushauri watu masikini?

Kwanini hatupendi kuwaomba ushauri watu masikini?

Katika ukuaji wangu huu sijawahi kuona mtu yeyote yule akienda kuomba ushauri kwa maiskini.

Sababu kuu itakuwa ni nini?​
  • Tunawadharau,​
  • Hawana mawazo,​
  • Hawana dira,​
  • Ubongo wao haufanyi kazi au​
  • Sababu inaweza kuwa ipi?​
Maskini ni kama Inspiration Speaker anashauri vitu ambavyo yeye mwenyewe hafanyi.

Au mganga anayekupa utajiri wakati Watoto wake ni maskini wa Kutupwa.
 
Maskini ni kama Inspiration Speaker anashauri vitu ambavyo yeye mwenyewe hafanyi.

Au mganga anayekupa utajiri wakati Watoto wake ni maskini wa Kutupwa.
Hoja yako ni kama kusema fundi anayetengeneza magari lazima awe na gari lake mwenyewe , kumbe kazi yake ni kuhakikisha gari lako linakuwa sawa.

Maskini anaweza kukupa ushauri mzito unaoweza kukuokoa, kwa sababu ameliishi janga hilo. Tajiri anaweza kukuangusha kwa ushauri wa mazoea yasiyoendana na uhalisia.
 
Katika ukuaji wangu huu sijawahi kuona mtu yeyote yule akienda kuomba ushauri kwa maiskini.

Sababu kuu itakuwa ni nini?​
  • Tunawadharau,​
  • Hawana mawazo,​
  • Hawana dira,​
  • Ubongo wao haufanyi kazi au​
  • Sababu inaweza kuwa ipi?​
Labda ni huko ulikokulia. Mimi nimekulia kijijini na katika watu waliokuwa wanafuatwa kwa ushauri ni mama mmoja aliyekuwa anaishi kwenye kibanda cha nyasi. Ni kesi gani ingefanyika bila yeye kuombwa kwenda kusikiliza na kutoa ushauri? Ni mama mmoja alikuwa na busara mno. Kwa uapnde mwingine alikuwepo baba mmoja alikuwa tajiri lakini watu walikuwa wanamwita jina la utani wa''lijinga'' (kwa kilugha lakini). Napingana kabisa na hii dhana yako.
 
Hoja yako ni kama kusema fundi anayetengeneza magari lazima awe na gari lake mwenyewe , kumbe kazi yake ni kuhakikisha gari lako linakuwa sawa.

Maskini anaweza kukupa ushauri mzito unaoweza kukuokoa, kwa sababu ameliishi janga hilo. Tajiri anaweza kukuangusha kwa ushauri wa mazoea yasiyoendana na uhalisia.
Sema wewe kiazi, mimi mhogo nitaambiwa nina mizizi. Asante sana. Jamaa amepotosha kabisa na nadhani anaweza kuwa mtoto wa juzi juzi ambaye hajapambana na maisha. Kwa kiwango kikubwa kwenye jamii yetu watu wanaofutwa kuombwa ushauri ni watu wasio matajiri.
 
Hoja yako ni kama kusema fundi anayetengeneza magari lazima awe na gari lake mwenyewe , kumbe kazi yake ni kuhakikisha gari lako linakuwa sawa.
Fundi hatengenezi gari anarekebisa matobo na kufunga nati zilizolegea.

Mganga yeye Pesa anakwambia anakufanyia mpango ili hali ana ndugu zake wamechoka mno na hawafanyii mpango.
 
Huwezi kushauriwa kitu na mtu aliyeshindwa kufanya hicho kitu hata kama mawazo yake ni mazuri..in short unatakiwa kutajirika kwanza ndo utoe ushauri
Na bahati mbaya matajiri nao hawatwambii njia za utajiri hata akisema basi ni uongo.
 
Back
Top Bottom