Mheshimiwa, anachozungumzia mtoa mada ni ughali wa huduma za Dstv ikiwa ni pamoja na malipo ya kila mwezi na ndio maana akapendekeza angalau iwe 50,000/= flat rate na amelenga kwenye mipira na mimi nimekubaliana naye ila nimejaribu kuonesha kuwa unaweza kuwa na Dstv kwa vifurushi unavyoweza kumudu. Mtoa mada pia ametahadharisha kuwa wasipokuwa makini watakosa wateja hasa wadau wengine wa huduma kama zao wakiingia sokoni kama ilivyo kwenye mabenki na mitandao ya simu kwa upande wa pesa ambapo wateja watakuwa na uwanja mpana kujichagulia hasa ving'amuzi vitakavyokuwa na huduma za mipira kama Dstv. Sasa hiyo mada B unayoizungumzia wewe mkuu wangu ni ipi? Mimi naona nipo ndani ya mada na ndio maana baadhi ya wachangiaji wamekubaliana na maoni yangu. Hebu mheshimiwa nitofautishie hiyo mada A na B huenda nikaelewa zaidi ni nini unachopingana na mimi. Elimu kwanza!