Kwanini Chumvi haipandi bei kama bidha nyingine!?

Kwanini Chumvi haipandi bei kama bidha nyingine!?

Njia ya uzalishaji wa chumvi ni rahisi kuliko uzalishaji wa bidhaa zingine kama vile sukari,pia upatikanaji wake ni rahisi.
 
Nina maswali machache kwako; Je, wewe ni muuza chumvi na hivyo na wewe unataka ipande bei ili uvune faida kubwa kama ilivyo kwa wauza mafuta? au umejikuta unashangaa tu kwa nini haipandi?

Sahii.

Hamna kitu hakijapanda bei ila vinatofautiana speed tu..
Unazani kwa speed ya Chumvi inaendana na umuhimu wake?
 
Unazani kwa speed ya Chumvi inaendana na umuhimu wake?
KIla zama na nyakati zake. Chumvi ishawahi kuwa madini ghali sana hapa duniani mpaka kufikia kuleta vita na mapigano makali....

Ukianza na neno salary lilitokana na neno salarium kipindi cha dola ya warumi wanajeshi walikua wanalipwa salarium (malipo ya chumvi) yani mshahara wako ni chumvi kwa namna ilikua na thamani zaidi ya dhahabu. Chumvi ilikua dili kubwa mno.

Afrika ya kati biashara zilikua zinaendeshwa na chumvi. Unanunua dhahabu kwa mabadilishano ya chumvi yani gramu moja ya chumvi kwa gram ya dhahabu. Chumvi alikua hakamatiki alikua adimu sana.

Ufaransa utawala ulishawahi kupinduliwa kwa sababu ya kodi ya chumvi.
Ugiriki mtumwa alikua ananunuliwa kwa chumvi.

Chumvi ilikua ni dhahabu nyeupe kiungo adimu kilichotumiwa kwa zaidi ya ladha ilikua ni imani.

Baada ya binadamu kugundua namna ya kuichimba ikaja kushuka thamani mno na baada ya ugunduzi wa majokofu kwa ajili ya kuhifadhia chakula chumvi ikabaki kiungo cha kawaida isiyo na thamani.

So swali lako jibu ni kuwa enzi zake zimepita ila chumvi ashakua mbabe kuliko dhahabu.

NA kukurahisishia tu. Chumvi inapatikana karibu kila mahali na supply ni kubwa kuliko demand.
 
Back
Top Bottom