Kwanini CHADEMA wanauchukia Mwenge wa Uhuru?

Kwanini CHADEMA wanauchukia Mwenge wa Uhuru?

Kwa mda mrefu sasa wabunge wa CHADEMA wamekuwa wakiendesha harakati za kupinga mwenge wa uhuru.

Najiuliza chadema wanachukia mwenge wa uhuru au wanachukia shughuri zinazofanywa na mbio za mwenge, Pengine wanadhani mwenge usipopita wao watazidi kuungwa mkono kwenye maeneo mengi.

Lakini imani yangu ni kuwa chadema wanapingana na maendeleo yanayozinduliwa na kufunguliwa wakati wa mbio za mwenge kwani wao ni wapinga maendeleo ili serikali ionekane haijafanya kitu,hizi siyo siasa bali ni kupotoka kwani siyo busara kupinga kila kitu.

Mwenge unapokimbizwa UNALETA MAENDELEO? Au Matumizi ya MALIGHAFI ovyo...
Unaongelea CHADEMA pekee? Uliwauliza CUF kama wanaupenda huo MWENGE? Au Wana CCM wa PEMBA wanaupenda huo MWENGE?

Yaani toka MWENGE uanze kukimbizwa ni MAENDELEO gani huo MWENGE umeyaleta??? Zaidi ya Wanafunzi kuondolewa Madarasani; kununuliana Sare kiufisadi badala ya kuimarisha Matakwa ya Wananchi...
 
Maneno mengi lakini ya maana ni mawili tu,
kunahaja ya chadema kuacha kuropoka kwa kupinga kila kitu badala yake ijikite kuendeleza jamii zaidi kuliko kupinga.

Naisikitia nchi yangu kwa kuwa na watu wenye mawazo kama yako, wagumu kubadilika na wanaowaza matumbo yao tu.
Hivi kweli kwa akili zako mwenyewe unaunga mkono uwepo wa mbio za mwenge kwa nyakati hizi!? Dah!
 
Chadema wakizunguka nchinzima kutoa elimu ya uraia ma ccm wanapiga kelele kuwa wanafuja pesa za walipakodi,lakini wao kuzungusha kibatari tanzania nzima kwao ni sawa.
 
Kwa mda mrefu sasa wabunge wa CHADEMA wamekuwa wakiendesha harakati za kupinga mwenge wa uhuru.

Najiuliza chadema wanachukia mwenge wa uhuru au wanachukia shughuri zinazofanywa na mbio za mwenge, Pengine wanadhani mwenge usipopita wao watazidi kuungwa mkono kwenye maeneo mengi.

Lakini imani yangu ni kuwa chadema wanapingana na maendeleo yanayozinduliwa na kufunguliwa wakati wa mbio za mwenge kwani wao ni wapinga maendeleo ili serikali ionekane haijafanya kitu,hizi siyo siasa bali ni kupotoka kwani siyo busara kupinga kila kitu.
Bora hata hao CDM mi ndo sitaki hata kuuona natamani aliyeiba stuli ya mwenge angeuiba mwenge wenyewe, unatumia gharama nyingi kuukimbiza pasi na sababu za msingi
 
Kwa mda mrefu sasa wabunge wa CHADEMA wamekuwa wakiendesha harakati za kupinga mwenge wa uhuru.

Najiuliza chadema wanachukia mwenge wa uhuru au wanachukia shughuri zinazofanywa na mbio za mwenge, Pengine wanadhani mwenge usipopita wao watazidi kuungwa mkono kwenye maeneo mengi.

Lakini imani yangu ni kuwa chadema wanapingana na maendeleo yanayozinduliwa na kufunguliwa wakati wa mbio za mwenge kwani wao ni wapinga maendeleo ili serikali ionekane haijafanya kitu,hizi siyo siasa bali ni kupotoka kwani siyo busara kupinga kila kitu.

kabla hujafikiri kuwa ni wapinga maendeleo basi fikiri ni kiasi gani kinatumika ktk kuuzungusha mwenge huo ambapo kiasi hicho kingeweza kutengeneza madawati mangapi? Kingeweza kulipa madai ya walim wangapi? Kingeweza kutoa huduma muhim ya maendeleo kwa jamii na hiyo miradi wanayozindua na akazinduliwa kwa garama nafuu tu.
 
Kwan bila mwenge miradi haifunguliwi?Chadema hawapendi mbio za mwenge kwani gharama za kukimbiza ni kandamizo tosha kwa wananchi(gharama za kukimbiza mwenga zinazidi zile za miradi inayofunguliwa),ni heri uwekwa makumbusho itasaidia kuletea pato kwa taifa

Hilo nalo wazo zuri kwani Tz bila mwenge inawezekana
 
mbio za mwenge wa uhuru ni muhimu kwa taifa. miradi mingi ya maendeleo huzinduliwa na watu hujumuika na kufurahishwa na ngoma za kitamaduni. mbali na miradi ya maendeleo, mwenge unakuza utamaduni hapa nchini

ufurahishwe na ngoma huku huna huduma muhimu kama maji safi, barabara mbovu, zahanati hakuna na kama ipo hakuna madawa wala vipimo
 
Hujajibu swali kwa nini chadema wanaupinga mwenge wa uhuru hata sababu wanazotoa hazina maana.
Wewe acha kujitoa ufahamu ndugu mwenge unaumia milioni 150 kuzindua mradi wa milioni 50 harafu mradi wenyewe tayari umeishaanza kuweka nyufa sasa kwa mwenye utimamu bado ataendelea kuupenda mwenge? Andaa post nyingine kwani suala la mwenge sio la CDM ni la watanzania walio wengi mwenge hauna faida zama hizi zaidi ya kutufilisi.
 
Haiwezekani mwenge kutokimbizwa tokeni poovu weee mpaka mchoke
 
Mwenge wa Uhuru kukimbizwa kila kona ya nchi ni upotevu wa fedha za walipa kodi.
 
Hauna faida.Labda huyu rais mpya lakini wa zamani anashindwa kutambua ufujaji wa pesa wakati wa mwenge.Kama si mtumishi wa umma basi tuulize sisi tunaambatana na wakuu wako wa wilaya na wakurugenzi wako uone jinsi per diem zinavyoliwa.Fikiri kabla ya kuandika msichana.
 
Mwenge kwa sasa ni janga,hadi taifa litakapozaliwa upya chini ya chama kipya!Penda usipende CCM SIYO CHAMA KIPYA hakiwezi kuleta SECOND LIBERATION
 
dr slaa 2uwekee gharama za mwenge kwa wilaya nimesahau uliwahi kutoa hizo data wakati ukiwa mbunge wa kara2
 
Hujui kitu. Kuzindua mradi hadi mwenge? Ina maana mwenge ukizimwa huwa hakuna miradi? Hivi wajua mwenge ukiwashwa hadi kuzimwa unatumia sh. ngapi ukimbizwa mikoa yote au ni wachache kupata posho.?

Nashangaaga sana wakati mwingine mwenge hubeba kauli mbiu za tahadhari dhidi ya ukimwi....wakati siku ya mwenge sehemu utakapolala kunakuwa ufuska wa hovyo...ngono hovyo si wa kimbizaji wala wakimbizwaji au wakimbiziwa....mwaka 2003 ulilala shule moja Sumbawanga kesho yake tukisafisha mazingira ...ikawa ni kufagia condom used nje , madarasani na hata vyumba walivyopewa mastaff....sasa niupende mwenge kwa lipi hasa
 
Ni ujinga ambao unataka kujengwa katika taifa hili, kwa watu wenye akili hawawezi kuchukia mwenge kwani imekuwa.ikihamasisha miradi mingi sana ya serikali na binafsi na michango yake ni ya hiyari na kila mwaka imekuwa ikibeba ujumbe maalum ktk kuhamasisha jambo fulani la kitaifa, watanzania mbinu zinazorumiwa na cdm kutaka kuingia madarakani ni za kuchungwa na kuogopwa sana maana wanatumia kila njia kuonyesha kila jambo linalofanywa na serikali halina maana, hata kuchangia maendeleo wao ni dhambi huku wao wamekuwa wakitembeza bakuli kila mkutano wao kuchangisha pesa ambazo hata matumizi yake hayana maelezo ya kutosha.
 
Back
Top Bottom