Kwanini CHADEMA wanauchukia Mwenge wa Uhuru?

Kwanini CHADEMA wanauchukia Mwenge wa Uhuru?

Mkuu umepinga nini na umekubari nini,sioni kama kuna gharama zozote za kuendesha mwenge ukilinganisha na faida zinazopatikana.

Hapo penye wekindu:gharama ni kubwa kuagiza dawa za kutibu waathirika wa UKIMWI ni kubwa sana ukitilia maanani kuwa wafadhili wamejito kusaidia ktk hili baada ya kugundua wagonjwa hawanufaiki bali mafisadi.ktk bluu funguka zaidi juu ya faida hizo!
 
hili liko wazi chadema ni wapinga maendeleo hatushangai kupinga maendeleo yanayofanywa na serikali.

vitu vyote vinavyofanywa na mwenge,ikiwemo kufungua miradi vinaweza kufanywa bila mwenge.So ukiangalia cost-benefit analysis huwezi support mwenge.Walimu,manesi,watendaji wanakatwa mishahara yao bila ridhaa;inasikitisha sana!
 
Suala la mbio za mwenge wa uhuru ni suala ambalo hakuna mtu mwenye uchungu na nchi ya Tanzania anayeweza kuliunga mkono, ni suala ambalo limebakia kisiasa mno, gharama zinazotumika katika mbio za mwenge wa uhuru ukilinganisha na faida ambazo ZINAWEZA KUPATIKANA (tilia mkazo) katika mbio hizo ni kubwa mno, mbio za mwenge wa uhuru zimebakia ni mbio za kufungua miradi (ya watu binafsi kwa asilimia 70%) na kuchangisha wananchi pesa ambazo kwa bahati mbaya huwa hazifahamiki huwa zinaenda wapi, ukiangalia kwa undani miradi ya serikali ambayo inafunguliwa haingeihataji mbio za mwenge kuifumgua, uchukulie kwa mfano wanakijiji wa kijiji X wameshirikiana na serikali kuchimba kisima cha maji katika hicho kijiji X, hivi mwenyekiti wa kijiji X akifungua kile kisima cha maji cha kijiji X yale maji ya kisima kile yatakuwa na tofauti iwapo badala ya kufunguliwa na mwenyekiti yatafunguliwa na kiongozi wa mbio za mwenge? Je ina maana kwamba kama mbio za mwenge zisingekuwepo wananchi wa kijiji X wasingepata maji ya kisima?

Suala linaloumiza ni kwamba gharama zinazotumika kwa kufanikisha mbio hizi za mwenge ni kubwa kuliko faida zinazopatikana kwa mbio hizi. Suala lingine linalonigusa ni kwamba siamini kama katika dunia hii kuna nchi nyingine ambayo inafanya tukio kama hili (mbio za mwenge) zaidi ya Tanzania, kama kuna mtu mwenye taarifa hizo ningependa aziwasilishe katika mjadala huu.

WANACHOKIPINGA CHADEMA
Wanachokipinga CHADEMA na naamini hii inawagusa na Watanzania wote wenye mapenzi mema na nchi yao ya Tanzania ni kwamba wakati umefika sasa wa Watanzania ambao ni watu wazima na wenye akili zao kuacha kukimbizana na moto huu barabarani (mwenge wa uhuru) na badala yake watumie muda huo na gharama hizo kujikita kwenye kazi kazi za kuleta maendeleo na gharama wanazotumia kwenye shughuli za kukimbiza mwenge zingeelekezwa katika kugharamia shughuli za kuleta maendeleo.


NB:
Tafadhali Watanzania rudisheni woyo wa uzalendo mlionao kwa nchi yenu, najua kwamba mnakatishwa tamaa na viongozi wasioijali nchi yetu lakini moyo wenu wa uzalendo ndio silaha pekee ya kuweza kuikomboa nchi hii.
 
Umempa jibu zuri kabisa 100%. Kwanza huku Kusini kuna malalamiko ya watumishi wa Serekali kukatwa shs 1000/ bila hiari yao.

sio kusini tu,hata huku Shinyanga,na ni kosa kubwa kumkata mtumishi hata shilingi ya mshahara wake bila ridhaa yake.
 
Kwa mda mrefu sasa wabunge wa CHADEMA wamekuwa wakiendesha harakati za kupinga mwenge wa uhuru.

Najiuliza chadema wanachukia mwenge wa uhuru au wanachukia shughuri zinazofanywa na mbio za mwenge, Pengine wanadhani mwenge usipopita wao watazidi kuungwa mkono kwenye maeneo mengi.
Lakini imani yangu ni kuwa chadema wanapingana na maendeleo yanayozinduliwa na kufunguliwa wakati wa mbio za mwenge kwani wao ni wapinga maendeleo ili serikali ionekane haijafanya kitu,hizi siyo siasa bali ni kupotoka kwani siyo busara kupinga kila kitu.
Ulevi wa mataputapu mchana na jua kali ni mbaya sana.Sasa hiki nini huyu anaandika? Chadema wanauchukia mwenge na wanatoa hoja za msingi ambazo upande wa wakimbiza mbio hizo za mwenge wamekuwa wana
shindwa kuzijibu.
 
Iam an employee wa taasisi flani( jina kapuni) nimehudhuria sherehe kadhaa za kukabidhiana mwenge, Kaka ni matumizi mabaya sana fedha za umma, unajua escort ya magari yanayozunguka na mwenge? Totally ni matumizi mabaya sana, bado sijazungumzia posho hapo.

...nakuunga mkona 100%.Mwezi huu(agosti) mwanzoni nimeshiriki ktk ziara wilayani kwetu.Ni upuuzi, i can tell you!Hotuba za wakimbiza mwng ni kuuponda vyama vya upinzani hasa Chadema na kusifia ccm badala ya kufanya mambo ya kiserikali neutrally.Nilikuwa nasikia kichefuchefu!
 
kwa mda mrefu sasa wabunge wa chadema wamekuwa wakiendesha harakati za kupinga mwenge wa uhuru.

Najiuliza chadema wanachukia mwenge wa uhuru au wanachukia shughuri zinazofanywa na mbio za mwenge, pengine wanadhani mwenge usipopita wao watazidi kuungwa mkono kwenye maeneo mengi.

Lakini imani yangu ni kuwa chadema wanapingana na maendeleo yanayozinduliwa na kufunguliwa wakati wa mbio za mwenge kwani wao ni wapinga maendeleo ili serikali ionekane haijafanya kitu,hizi siyo siasa bali ni kupotoka kwani siyo busara kupinga kila kitu.

soma [isaya 50;11]
 
We kweli una akili mgando kama sio tope lililo kichwani mwako...!! Kitu cha muhimu ni kuzindua miradi na hao viongoz wa maeneo wanafanya nn....!!! Umesha zeeeka kweli....!!!!
 
kimsingi kukimbiza mwenge ni hasara tu kwa taifa.na sioni hoja ya msingi kuendelea kutetea mbio hizi maana zimekuwa mzigo mkubwa kwa serikali na wananchi.sehemu nyingine wananchi wanapigwa hadi na sungusungu kwa ajili ya kuchangia mwenge huu.
 
waziri makala leo kashindwa kuonyesha hizo faida za kukimbiza mwenge.kabaki anajikanyaga tu.yan kwenye ukweli watanzania tusitafute pakujificha.haimaanishi kila aloasisi nyerere n jema.linaweza kuwa jema kwa wakati huo lakini si kwa sasa.lazima tuangalie hali ya uchumi wetu kulinganisha na mahitaji yetu.mahitaji yasiyo ya msingi kama haya tuyaache maana hata huo mwenge wenyewe umepoteza maana yake halisi sasa.
 
Vincent Nyerere ni Mwongo mkubwa ! Mwananchi gani wa Musoma mjini kamtuma kuukataa Mwenge wa Uhuru! Tunataka viongozi visionary sio akina Vincent hawa ambao wanakurupuka kutokana na upeo mdogo unaosababishwa na UTAPIAELIMU! CHADEMA na viongozi wenu wenye upeo mdogo kama akina Mbowe tambueni kuwa kila Nchi ina TUNU zake.Nyerere (Julius) was a great thinker,hawezi kuwa challenged na mtu mwenye kichwa cha Panzi kama Mbunge wa Musoma mjini eti Vincent Nyerere! Kuna watu majina yanawabeba sana mmoja wao ni huyu Vincent Nyerere,isingekuwa jina la Nyerere hasingeaminiwa hata kuwa kiongozi wa CHOO!
 
Hujajibu swali kwa nini chadema wanaupinga mwenge wa uhuru hata sababu wanazotoa hazina maana.

Sio CHADEMA tu ndio wenye kupinga Mwenge,but also wa Tanzania wote wenye kujitambua wana laani na Kupinga Huu upuuzi.
Bahati Mbaya kwenu CCM ni kuwa CHADEMA wanafanya vitu vinavyoeleweka na kukubalika kwa wa Tanzania wenye kujitambua.
Nyie Mtawapata Mazuzu tu katika hili
 
Vincent Nyerere ni Mwongo mkubwa ! Mwananchi gani wa Musoma mjini kamtuma kuukataa Mwenge wa Uhuru! Tunataka viongozi visionary sio akina Vincent hawa ambao wanakurupuka kutokana na upeo mdogo unaosababishwa na UTAPIAELIMU! CHADEMA na viongozi wenu wenye upeo mdogo kama akina Mbowe tambueni kuwa kila Nchi ina TUNU zake.Nyerere (Julius) was a great thinker,hawezi kuwa challenged na mtu mwenye kichwa cha Panzi kama Mbunge wa Musoma mjini eti Vincent Nyerere! Kuna watu majina yanawabeba sana mmoja wao ni huyu Vincent Nyerere,isingekuwa jina la Nyerere hasingeaminiwa hata kuwa kiongozi wa CHOO!

Kwa hiyo Mwenge ni Tunu???
Sasa kati Vincent na wewe nani Kichwa Panzi??
 
Mkuu we hewa kweli ambacho sijui nini hapo nilijua utatoa data unazojua lakini umetokwa povu tu.

Ucjitoe ufahamu wewe,kwan wewe umetoa data gani hapo kusupport mwenge?,mbona una tabia za kishoga hvyo?
 
Hujui kitu. Kuzindua mradi hadi mwenge? Ina maana mwenge ukizimwa huwa hakuna miradi? Hivi wajua mwenge ukiwashwa hadi kuzimwa unatumia sh. ngapi ukimbizwa mikoa yote au ni wachache kupata posho.?

Halafu kuna ufisadi mkubwa hufanyika kupitia huo mwenge; gharama za kuuendesha ni kubwa mno, misafara mikubwa ya magari, per diems, upotevu mkubwa wa muda kwa wafanyakazi wa serikali wakati mwenge ukupokelewa, kukimbizwa na kukabidhiwa sehemu nyingine.

Nilishawahi kushuhudi mradi feki ukizinduliwa na Mwenge huko mkoani Mara; mradi wa ujenzi wa jengo la zahanati lililofadhiliwa na NGO, serikali ya Wilaya ikasema Halmashauri imelijenga hilo jengo kwa milioni kadhaa!
 
CDM wanapinga kila kitu hata Mungu wanampinga sembuse Mwenge wa Uhuru? Wao ni wapinzani wa kupinga kila kitu kizuri na mabingwa wa kuitakia mabaya nchi yetu.

Wakiona barabara zinajengwa wanakereka kweli kwa mfano barabara za Dar sasa wao wanaumia sana. Yaani Kwao falsafa Yao ni adui mwombee njaa ndio maana hata kuchangia Kwao ni shida ati hadi malazi serikali itagharamia
 
Wana jF
Inawezekana huwa tunajitosa kwenye mambo ambayo hatuyajui na huwa hatufanyi utafiti. Kuhusiana na Mwenge nimekuta ushauri wa Busara wa mzee wetu, mzee Kasori, aliyekuwa PrivatecSecretary yaani Katibu Myeka wa Rais Wa kwanza wa JMT ambaye ndiye mwanzilishi wa Mbio za Mwenge. Ninanukuu

Comrade G.H.Mkuchika, Pole kwa yote ysliyojiri Bungeni Ijumaa 30August,2013 kuhusu Mbioza Mwenge Tz. Nakumbuka hata Mwl. J.K. Nyerere kabla hajafariki alikwisha shauri kuwa Ratiba ya Mbio za Mwenge itazamwe upya kwamba ukimbizwe kila baada ya muda fulani au matukio maalum!Bila kumung'unya maneno alionya juu ya gharama na Serikali kutofanya tathmini ya miradi inayozinduliwa na kwamba baadhi ni magofu yaliyotelekezwa tangu akiwa Rais. Kwamba nidhamu katika siku za mkesha wa Mwenge imeanza kutia shaka. Hapo alikuwa na maana ya ulevi na ngoni.Comred Mkuchika huo ndio ukweli tu. Umuhimu wa Mwenge km ulivyosema kwa usahihi mkubwa upo pale pale. Tatizo ni management na Financing ya Mbio hizo na ubora na ufuatiliaji wa miradi kulingana na thamani ya fedha na jinsi gani Serikali pia inavyofuatilia kila kauli mbiu husika kwa mwaka au miaka iliyopita. comrade huo ndio ushauri wangu bila kuathiri angalizo la Mwl. J.K.Nyerere. Namaliza kwa kusema kuwa, pale ambapo tumepuuza ushauri wa kizalendo wa J.K.Nyerere Taifa letu Tanzania sasa tunaogelea katika matatizo lukuki tu. as ante Comrade. Kasori S.H., Arusha. Copy Mhe. Rais,Jakaya M.Kikwete" (tel.0716 267 879). Ni vema tukafanya utafiti wa mambo, badala ya Ushabiki ambao madhara yake ni makubwa kwa Taifa. Tutetee mambo si kwa ushabiki Bali kwa mantiki yake, kwa umuhimu wake, na tukubali kukosolewa pale ambapo historia inaonyesha dhahiri tumetokq nje ya malengo ya msingi.
Um



CCM is just preserving one among the national emblems, Uhuru torch was introduced symbolically to shine the country and across the borders, to bring hope where there is despair, love where there is enmity, and respect where there is hatred!! we race it across the country to remind us of our roots as a nation...sasa kama unapingana na haya mawazo chanya, nitashangazwa na uzalendo wako.
 
Nchi zilizo mbele kuliko Tanzania ina maana na wao wana kitu mfano kwa mwenge wanakimbiza? Umbulula tuu
 
Kwa mda mrefu sasa wabunge wa CHADEMA wamekuwa wakiendesha harakati za kupinga mwenge wa uhuru.

Najiuliza chadema wanachukia mwenge wa uhuru au wanachukia shughuri zinazofanywa na mbio za mwenge, Pengine wanadhani mwenge usipopita wao watazidi kuungwa mkono kwenye maeneo mengi.
Lakini imani yangu ni kuwa chadema wanapingana na maendeleo yanayozinduliwa na kufunguliwa wakati wa mbio za mwenge kwani wao ni wapinga maendeleo ili serikali ionekane haijafanya kitu,hizi siyo siasa bali ni kupotoka kwani siyo busara kupinga kila kitu.[/:ban:

viongozi wanakazi gani shughuli za maendeleo zizinduliwe/kufunguliwa na Mwenge? Acha uvivu wa kufikiri, mwenge ni kero kwa wananchi hasa walimu na wanafunzi
 
CDM wanapinga kila kitu hata Mungu wanampinga sembuse Mwenge wa Uhuru? Wao ni wapinzani wa kupinga kila kitu kizuri na mabingwa wa kuitakia mabaya nchi yetu.

Wakiona barabara zinajengwa wanakereka kweli kwa mfano barabara za Dar sasa wao wanaumia sana. Yaani Kwao falsafa Yao ni adui mwombee njaa ndio maana hata kuchangia Kwao ni shida ati hadi malazi serikali itagharamia

wewe ni Mnyiramba wa ajabu sana na sishangai kwani sifa ndio asili yenu! Hivi uozo unaofanyika kwa mwavuli wa mwenge huuoni? Au ndio ujuha umekuvaa na unafiki wa kiccm?
 
Back
Top Bottom