tutaweza
JF-Expert Member
- Oct 3, 2011
- 634
- 457
Kwa mda mrefu sasa wabunge wa chadema wamekuwa wakiendesha harakati za kupinga mwenge wa uhuru,
Najiuliza chadema wanachukia mwenge wa uhuru au wanachukia shughuri zinazofanywa na mbio za mwenge,
Pengine wanadhani mwenge usipopita wao watazidi kuungwa mkono kwenye maeneo mengi,
Lakini imani yangu ni kuwa chadema wanapingana na maendeleo yanayozinduliwa na kufunguliwa wakati wa mbio za mwenge kwani wao ni wapinga maendeleo ili serikali ionekane haijafanya kitu,hizi siyo siasa bali ni kupotoka kwani siyo busara kupinga kila kitu.
Naheshimu mawazo ya kila mtu.
Ila ndugu yangu nashindwa kuamini kama mtu mwenye akili timamu na mpenda maendeleo anaweza akaunga mkono 'mbio za mwenge'. Yaani unashindwa kufikiri kwamba hiyo miradi inayozinduliwa na mwenge ingekuwepo hata bila mwenge!?
Mwenge haukuleta hiyo miradi, bali ukifika mahali flani wanatafuta kitu cha kuzindua. Ndio maana wamefikia hatua ya kuzindua hata 'Guest houses' za watu binafsi. Nimeshuhudia 'guest house' iliyozinduliwa na kiongozi wa mbio za mwenge.
Nadhani tatizo lako ni CHADEMA na wala sio mwenge