SAMAHANI, mwenge wa uhuru hauna maendeleo yoyote unayoyaleta, bali unakimbizwa kuzindua miradi na kudumisha amani ya nchi, lakini hili amani ya nchi ni idealist sana kwa walioanzisha. gharama za kuukimbiza mwange wa uhuru ndo zinafanya chadema wapinge, leo hii tunakimbiza mwenge kuzindua miradi ya watu binafsi kama shule na vituo vya kulelea watoto, pia miradi ya serikali ambayo tunaweza kumuita mkuu wa wilaya au mkoa akaja kuzindua then gharama za kuja mwenge zikaenda hata kwenye mpango wa big results kusaidia elimu inayoshuka ubora kila siku, fikiri chanya juu ya mwenge wa uhuru na ulinganishe na uchumi wetu ulivyo, je tunastahili kugharamia mbizo za mwenge ambazo zina madhara hasi kwa jamii hasa mwenge unapo lala?