Stroke
JF-Expert Member
- Feb 17, 2012
- 38,658
- 49,095
Wana jF
Inawezekana huwa tunajitosa kwenye mambo ambayo hatuyajui na huwa hatufanyi utafiti. Kuhusiana na Mwenge nimekuta ushauri wa Busara wa mzee wetu, mzee Kasori, aliyekuwa PrivatecSecretary yaani Katibu Myeka wa Rais Wa kwanza wa JMT ambaye ndiye mwanzilishi wa Mbio za Mwenge. Ninanukuu
Comrade G.H.Mkuchika, Pole kwa yote ysliyojiri Bungeni Ijumaa 30August,2013 kuhusu Mbioza Mwenge Tz. Nakumbuka hata Mwl. J.K. Nyerere kabla hajafariki alikwisha shauri kuwa Ratiba ya Mbio za Mwenge itazamwe upya kwamba ukimbizwe kila baada ya muda fulani au matukio maalum!Bila kumung'unya maneno alionya juu ya gharama na Serikali kutofanya tathmini ya miradi inayozinduliwa na kwamba baadhi ni magofu yaliyotelekezwa tangu akiwa Rais. Kwamba nidhamu katika siku za mkesha wa Mwenge imeanza kutia shaka. Hapo alikuwa na maana ya ulevi na ngoni.Comred Mkuchika huo ndio ukweli tu. Umuhimu wa Mwenge km ulivyosema kwa usahihi mkubwa upo pale pale. Tatizo ni management na Financing ya Mbio hizo na ubora na ufuatiliaji wa miradi kulingana na thamani ya fedha na jinsi gani Serikali pia inavyofuatilia kila kauli mbiu husika kwa mwaka au miaka iliyopita. comrade huo ndio ushauri wangu bila kuathiri angalizo la Mwl. J.K.Nyerere. Namaliza kwa kusema kuwa, pale ambapo tumepuuza ushauri wa kizalendo wa J.K.Nyerere Taifa letu Tanzania sasa tunaogelea katika matatizo lukuki tu. as ante Comrade. Kasori S.H., Arusha. Copy Mhe. Rais,Jakaya M.Kikwete" (tel.0716 267 879). Ni vema tukafanya utafiti wa mambo, badala ya Ushabiki ambao madhara yake ni makubwa kwa Taifa. Tutetee mambo si kwa ushabiki Bali kwa mantiki yake, kwa umuhimu wake, na tukubali kukosolewa pale ambapo historia inaonyesha dhahiri tumetokq nje ya malengo ya msingi.
Um
Faida za hayoi niliyoyawakilisha hazina value in terms of money, na sishabikii ili kukamilisha ratiba ya ushabiki kwa chama cha ccm, bali kuona umuhimu wa kuwepo kwa mwenge wa uhuru katika taifa letu, kiwango cha thamani kimepunguzwa na uzalendo wetu binafsi, nazungumza hayo nikijaribu kufananisha na mataifa mengine yasivyoacha kutumia gharama katika kuzimamia core value za taifa lao, marekani ni taif aambalo limeundwa kwa misingi ya kidemeokrasia na inatumia gharama kubwa sana kuona nchi nyingine za dunia zikisimama katika demokrasia wanayoiamini, tukiachia mbali dhana ya kusimamia national interest ambazo wengi tunaweza kusema kua wanafanya hayo kutokana interest zao, hivyo basi kuna kila sababu ya kuendelea kuprserve our core national values at any cost, hiyo itatujenga kama taifa kuona kwamba kuna gharama kwa kila tunalo amini, tukiacha sasa, vizazi vyetu vijavyo vitatuona kama wazembe na wabinafsi, mwenge wa uhuru ukipotea sasa, tutakosa urithi bora kwa vizazi vyetu