Kumlipa mtu elfu kumi kwa mwezi ni sawa na kutomlipa. Haya tuone mfano wa kulipa watumishi, ungependekeza walipwe kiasi gani?
Mathalani, ukialika wanataaluma jadidi ukawalipa milioni 2 kila mmoja kwa mwezi wakiwa kumi tayari ni milioni 10. Unakaribia kumaliza ruzuku ya chama ya milioni 66.
Ukweli ni kuwa sasa CHADEMA haifanyi hayo malipo makubwa lakini Chacha ndiyo anasema makao makuu wanajipendelea. Sasa itakuwaje kama makao makuu wakaanza kujilipa mafao makubwa kama ulivyoshauri?
kama unataka suala kama hili basi wakee kwanza watu kama Chacha wanaonedesha siasa kwa nadharia.
Kama makao makuu wakilipwa milioni, wilayani watalipwa bei gani? Halafu kuna wilaya zaidi ya 130? Na majimbo je? Kuna majimbo 232! Na Kwenye kata Je, kuna kata 2300. Na vijijini je? Ukishaweka suala la malipo mbele kwa mazingira ya Tanzania basi ujue huna chama!
Hebu mtu atutengenezee hapa bajeti ya milioni 59 ambayo ndio ruzuku ya CHADEMA.
Apange matumizi ya watumishi makao makuu, gharama za uenezi, ruzuku wilayani nk! Aonyeshe mfano kuwa pengine CHADEMA ingetumia hivi fedha zake.
Asha
Fidel80, unaweza kuonyesha wapi au lini nilitetea mafisadi?
CHADEMA hawawezi kutumia pesa za BOT kwa sababu hawana access nazo, tatizo lao hata zile pesa ndogo za ruzuku wanazopata zinatumika kumboresha Mbowe na marafiki zake peke yao na anayeleta fyoko tu anapigwa benchi kama Chacha Wangwe na yule aliyekuwa mwenyekiti wa Morogoro.
unachoshindwa kujua ni kwamba JF sio chama cha siasa chenye malengo ya kuongoza nchi siku moja kama chadema, Hii ni forums ambayo watu wachache wamejitolea kwa moyo mmoja na hata wewe hujakatazwa kufanya hivyo, lakini Chadema ni chama cha siasa na kina katiba na dhumini la kuongoza nchi yetu kama ikibahatika,we unategeme siku Mbowe akisema anataka kulipwa pesa zake zote alizo jitolea wakati wako IKulu si watauza nchi yetu , kuwa makini ndugu yangu
Haina haja ya Kumlipa Mbowe sababu hapo CHADEMA ni sehemu ambapo ni kijiwe chake cha kusemea.Yeye si Mwanazuoni maarufu hivyo hawezi kutumia Elimu kueleza watanzania wakamwelewa.ndiyo maaana alienda Shule hivi karibuni ili aonekane na yeye ana Elimu
Suala la Pili ni kwamba CHADEMA kama wao wameshindwa kutafuta Wafadhili wa kuendesha chama sababu hakuna watu wabunifu ambo wanaweza kuandika Proposal nzuri labda waandikiwe na kina Baregu au Zitto ila wengi wao ni watu wanotawaliwa na Emotion.
The Truth is Upinzani wa kweli utapatikana mpaka pale CCM itakapogawanyika na kupatikana wapinzani wenye uwezo wa kuongozi siyo wanaotafuta Uongozi.
Kimsingi ni kuwa Serikali yetu inashindwa kuendelea kwasabu ya watu wengi ambo wanafanya kazi serikalini ni Vilaza wa kutupwa na kila siku wanataka kushindana na watu wenye uwezo na wanalipwa vizuri na hii inasababisha Rushwa.The same as CHADEMA.
watu wanapo kushishia flani ni fisadi mbona unakuwa wa kwanza kuclash?
Angalia post zako vizuri basi,Jitahidi kubadilika mkuu.
Wananchi wanaumia sana kwa ajili ya ufisadi.
Tatizo la wana CHADEMA wengi wao hawataki kukubali mapungufu,kukosolewa cha mhimu kwao ukiwapinga wanakuita CCM fisadi huu si ni UDIKITETA WA MAWAZO!!
Badala ya kujadili kilichoandikwa wengi wao watakimbilia kukuambia FISADI yani ndani ya CHADEMA ni ndio mzee hakuna kupinga hata kama kuna mambo unayaona yanakimong'onya chama.
Wangwe kajifanya kwenda kupingapinga mambo yao Umeona kilichompata.
Tatizo mimi naona hatujui CORE ya chama cha siasa, watu wanafikiri nikuchukua hatamu kuingia ikulu mambo yamekwisha,ama kutafuta wafanya biashara wenye pesa zao wawafadhiri hapo kiama ndipo kinaanzia.
CORE ya chama ni kubadili ATMOSPHERE ya wananchi hatimaye nchi ,huwezi badili atmosphere ya nchi ili uje ubadili atmosphere ya wananchi.
Kwa yule anayedhani CORE ya chama ni kuombamba ili aje aiingie ikulu ili aje alipe fadhira kwa wale aliowaomba ndio chazo cha akina ROSTAM.
Kuomba omba kwa chama yaliyofanywa na akina Nyerere ni mazingira waliokua nayo na khali yao ya kwamba siamini kama serikali ya kikoloni ingependa kuona TAA inakampuni inayoiigizia fedha na hata kuombaomba kwa TAA ni kwa wakati ule na si tamaduni ya kuilinda.
kuendelea ku REF:mambo aliyofanya Nyerere miaka ile na kuyaendeleza kama ilivyo huo ndio ukosefu wa ubunifu,kinachotakiwa ni kuyangalia na kuya advance zaidi yani ya kwamba mambo ya Nyerere na TANU yake yalikua mazuri lakini yapo ANALOG sana kumbe CHADEMA ama CUF,ama CCM,ama UDP inatakiwa iya process na kuya DIGITALIZE.Mambo ya wakati ule kuyacopy kama yalivyo na kuyapaste wakati huu ndio inakuja ile phenomenani yakua ndivyo tulivyo.
Kama ingekua hivyo maendeleo yasingekuwapo.
Mchelea Mwana,
Mbowe hawezi kuidai CHADEMA imlipe fedha zake kwa sababu yeye amejitolea kwa hiari kuchangia chama chake. Mbowe atakuwa na haki ya kudai fedha yake kama kuna makubaliano ya kuwa anachofanya kwa ajili ya CHADEMA ni mkopo kwa chama hicho, na siyo mchango wa kujitolea. Kujitolea na kukopesha ni mambo mawili tofauti.
Kumbukeni tamko la CHADEMA baada ya uchaguzi mkuu 2005. Mbowe alipozungumza na waandishi wakati huo alisema pale kabisa kuwa Kamati Kuu, Baraza Kuu na Mkutano mkuu 2005 wote waliruhusu chama kikope kufanikisha kampeni za 2005. Chama kilikopoa takaribani milioni 700. Kati ya hizo yeye mwenyewe alikopesha 500. Baada ya uchaguzi kamati kuu, baraza kuu na Mkutano Mkuu vilikaa mwaka 2006, Agosti 11, 12 na 13. Vikakubali kulipa madeni yote. Lakini Mbowe akasemee zaidi ya milioni 200 na akataka zingine zihesabike kama mchango wake kwa chama. Sasa badala ya Chacha Wangwe kupongeza anabaki akilalama maneno ya uwongo. Huyu ndiye Chacha Wangwe ambaye kampeni zake za Ubunge zilitumia zaidi ya milioni 20. Mbowe akiwa amempatia milioni 5, chama chake milioni 4, Tundu Lissu pamoja na kumtoa jela alipokuwa amefungwa bado akaingia gharama za milioni 11 kumwezesha kushinda. Si mnakumbuka yale mahojiano ya Chacha na Tanzania Daima baada ya uchaguzi ambapo aliwashukuru hawa? Unakumbuka wakati ule Mbowe alimsaidia Chacha kuanzia Toa Chambiri Tarime(TOCHATA) na vikao vyote kufanyika Billicanas kwa gharama za Mbowe? Hebu vuteni kumbukumbu kwa kuwa Tanzania Daima ilikuwa ikiandika vikao hivyo.
Asha
Tatizo la wana CHADEMA wengi wao hawataki kukubali mapungufu,kukosolewa cha mhimu kwao ukiwapinga wanakuita CCM fisadi huu si ni UDIKITETA WA MAWAZO!!
Badala ya kujadili kilichoandikwa wengi wao watakimbilia kukuambia FISADI yani ndani ya CHADEMA ni ndio mzee hakuna kupinga hata kama kuna mambo unayaona yanakimong'onya chama.
Wangwe kajifanya kwenda kupingapinga mambo yao Umeona kilichompata.
Tatizo mimi naona hatujui CORE ya chama cha siasa, watu wanafikiri nikuchukua hatamu kuingia ikulu mambo yamekwisha,ama kutafuta wafanya biashara wenye pesa zao wawafadhiri hapo kiama ndipo kinaanzia.
CORE ya chama ni kubadili ATMOSPHERE ya wananchi hatimaye nchi ,huwezi badili atmosphere ya nchi ili uje ubadili atmosphere ya wananchi.
Kwa yule anayedhani CORE ya chama ni kuombamba ili aje aiingie ikulu ili aje alipe fadhira kwa wale aliowaomba ndio chazo cha akina ROSTAM.
Kuomba omba kwa chama yaliyofanywa na akina Nyerere ni mazingira waliokua nayo na khali yao ya kwamba siamini kama serikali ya kikoloni ingependa kuona TAA inakampuni inayoiigizia fedha na hata kuombaomba kwa TAA ni kwa wakati ule na si tamaduni ya kuilinda.
kuendelea ku REF:mambo aliyofanya Nyerere miaka ile na kuyaendeleza kama ilivyo huo ndio ukosefu wa ubunifu,kinachotakiwa ni kuyangalia na kuya advance zaidi yani ya kwamba mambo ya Nyerere na TANU yake yalikua mazuri lakini yapo ANALOG sana kumbe CHADEMA ama CUF,ama CCM,ama UDP inatakiwa iya process na kuya DIGITALIZE.Mambo ya wakati ule kuyacopy kama yalivyo na kuyapaste wakati huu ndio inakuja ile phenomenani yakua ndivyo tulivyo.
Kama ingekua hivyo maendeleo yasingekuwapo.
Asha, msemo wa Kiswahili unasema mtu hujikuna pale mkono unapofika. Kila kitu kinaenda na bajeti na bajeti ni kupanga na kupanga ni kupangua, na unapopangua unachagua. Huwezi kufanya mambo yote with a limited resources, hii ni uchumi 101. Katika kuchagua unafanya kile kinachofuata opportunity cost na unapima kipi kifanywe kwanza.
Ukinipa mimi bajeti ya 59 nitaiangalia na kukuambia ok.. hiki tunaweza kukifanya mwezi huu hiki hatuwezi kukifanya. Hiki lazima kifanyike kila mwezi na kipi kisifanyike kila mwezi. Naomba ieleweke pia kuwa sina maana kuwa wanachama wasichangie fedha zao kwenye kuendesha chama, si kweli vyama huendeshwa kwa michango ya kawaida na michango ya wanachama wake au mashabiki.
Niwape idea: Chadema ina watu maarufu kama Zitto, Chacha mwenyewe, Mbowe, Dr. Slaa na Tundu Lissu. Why not organize a fundraising gala ambapo Chadema inaandaa dinner kwa watu mbalimbali na wafanyabiashara n.k na wananchi wa kawaida? Wakati wa suala la Zitto ilikuwa ni perfect timing kwa chama kujijenga kifedha, hakikufanya hivyo. Likaja suala la Richmond, hawakufanya hivyo, na mambo haya mengine yote Chadema hawajakaa chini na kutumia clout waliyonayo kujijenga financially.
Guess what? CCM ikipata jambo lolote la msingi hawachelewi kucapitalize financially. Nakumbuka jinsi walivyoweza kuchangisha milioni 400 kule Butiama kiulaini tu...that is what political parties do. Leo hii Obama amekuwa mchangishaji wa fedha kwa chama chake kuliko hata Clinton kabla yake! Kwanini wasitumie Popularity ya Zitto na Slaa kupata fedha zaidi za kuendeshea chama au kukipiga jeki.
Leo hii kuna watu mamia wanaofurahia utendaji kazi wa Chadema na wabunge wake, kuna mtandao wa kiintaneti, kwanini hadi leo hii Chadema haijawa ya kwanza kuwa na akaunti ambayo watu wanaweza kuchangia moja kwa moja toka nje? Kwa kutumia mtandao wa intaneti wangeweza kujipatia kiasi fulani cha fedha kwa mashabiki wake. Sitoshangaa CCM muda si mrefu wakaweka akaunti zao kwenye mtandao na ya kuwa wameanza kupokea Visa, Mastercard, AE na DC na kwa kadiri wanavyofungua matawi nje ya nchi sitoshangaa wakapata fedha nyingi tu! Kwanini Chadema wameshindwa kuja na kitu kama hicho?
Kwenye kuchangia kutoka kwa prominent leaders au members.. Badala ya kuchangia hivi hivi tu why not sit down with these members na waambia ni kiasi gani wanaweza kuchangia mara moja kwa mkataba wa kama uwekezaji? Sema kina Zitto (wabunge) na wanachama wengi mashuhuri kila mmoja anasema anaweza kuchangia Shs. milioni 2.5 kuanzisha akaunti ya kuwekeza kwa muda maalumu (Fixed Deposit).
Binafsi ninachosema ni kuwa sidhani kama njia zote za kutafuta fedha za kuendeshea chama zimeweza kuangaliwa na fully explored and exhausted. Nadhani wakikaa chini wanaweza kuona jinsi nyingi tu ya kuweza kukusanya fedha za chama. Vipi kuhusu kutengeneza Tshirt za viongozi mashuhuri!? halafu zikauzwa baada ya kuwa autographed!? Siasa ni mchezo wa mikakati, mbinu, kuthubutu na kufikiri nje ya kisanduku. Chadema haina sababu ya kutegemea ruzuku tu, jinsi ile ile CCM haina sababu ya kutegemea ruzuku.
Tatizo ni kuwa wenzao CCM wana uwezo wa kuchota hata kutoka katika altare!
Mwanakijiji
Hayo yote uyasemayo CHADEMA imeshayafanyia kazi. Labda uongezeke na wewe usaidie hiyo kazi. Kwani nani kakwambia kwamba CHADEMA ni Zitto na Dr Slaa tu, hivi kwanini mnapenda kukaa pembeni na kunyoosha vidole tu!
Hizo fundraising gala zinafanyika. Kwani hapa si tuliwekewa Hotuba ya Fundraising Dinner ya Arusha ambayo Mgeni Rasmi alikuwa Mtei, Zitto na Mhonga akiwepo? Iliandaliwa na vijana wa CHADEMA?
Tatizo ni kuwa wafanyabiashara wengi wanaogopa athari za kujitokeza kuchangia upinzani. CCM wanawabana. Ndio maana utawakupa wakina Ngurdoto, Impala wote wanakwenda kwenye harambee za CCM. Halafu ni huko huko wakina Johnson Lukaza wanakwenda kubariki mabilioni ya EPA kuwa fedha halali za chama.
Hamishia huu mjadala kwenye makala zako usaidie kujenga demokrasia Tanzania badala ya kulalama tu humu.
Hiyo link ya akaunti niliyotoa si iko kwenye website ya CHADEMA? Kwa nini watu wa nje hawachangii? Labda unachoweza kuwasidia ni kuwatengenezea pay pall uunganishe na hiyo akaunti namba kama ambavyo umefanya kwa KLH. Lakini jua hawa watanzania ni wakosoaji tu, maneno mengi bila vitendo.
Kama mntaka upinzani makini Tanzania chukueni hatua badala ya kukaa tu na kunyanyua vidole juu.
Ile like you because you take action. Go go go go go. Tutafika tu. Na jua wakuu wa CHADEMA wanakusoma, lakini mambo si rahisi kama unavyodhani.
Unaweza kuamua kuwaleta wakina beyonce bongo, lakini wakijua tu wanaletwa na upinzani Afrika wataishia Airport. Siasa Afrika si sawa na ulaya. We have to transform the terrain. Then we can make it
Asha
Kwanza I take offense kuwa tunakaa Ulaya na kunyanyua vidole tu! yaani kusaidia chadema hadi wote turudi nyumbani? Hii ni argument ambayo imekuwa ikitolewa na wana CCM kila tunapotoa hoja. Ni lini Chadema wameweka akaunti yao hadharani na kuomba kuchangiwa ni mashabiki na wanachama wake walioko nje ya nchi? Hivi hili nalo inabidi hadi turudi nyumbani?
Suala la wafanyabiashara ni moja lakini ni kwa kiasi gani Chadema na vyama vingine vya upinzani vimethubutisha wafanyabiashara kujiunga nao. Hapa sizungumzii wafanyabiashara wakubwa tu nazungumzia hata wadogo. CCM na serikali yake haiwezi kuwawekea ngumu wafanyabiashara wadogowadogo bila kusababisha dhuluma!
Sasa kama mawazo na hoja ni za wale walioko nyumbani tu na michango ni mpaka turudi wote nyumbani basi endeleeni kupeana mawazo ninyi wenyewe, kwani si wote mashabiki wa Chadema ni wanachama wa Chadema!

Kwanza I take offense kuwa tunakaa Ulaya na kunyanyua vidole tu!
Wapi Asha kasema tunakaa Ulaya na kunyoosha vidole?
Asha, msemo wa Kiswahili unasema mtu hujikuna pale mkono unapofika.
Niwape idea: Chadema ina watu maarufu kama Zitto, Chacha mwenyewe, Mbowe, Dr. Slaa na Tundu Lissu. Why not organize a fundraising gala ambapo Chadema inaandaa dinner kwa watu mbalimbali na wafanyabiashara n.k na wananchi wa kawaida? Wakati wa suala la Zitto ilikuwa ni perfect timing kwa chama kujijenga kifedha, hakikufanya hivyo. Likaja suala la Richmond, hawakufanya hivyo, na mambo haya mengine yote Chadema hawajakaa chini na kutumia clout waliyonayo kujijenga financially.
Guess what? CCM ikipata jambo lolote la msingi hawachelewi kucapitalize financially.
Leo hii kuna watu mamia wanaofurahia utendaji kazi wa Chadema na wabunge wake, kuna mtandao wa kiintaneti, kwanini hadi leo hii Chadema haijawa ya kwanza kuwa na akaunti ambayo watu wanaweza kuchangia moja kwa moja toka nje?