Kwanini Chadema haiwalipi hawa?

Kwanini Chadema haiwalipi hawa?

wewe subiri uje sikia sehemu walipoandika sijui kabila gani ndio utajua ,harafu huoni anaweza kutoka bagamoyo,lindi lakini ni mchaga
wewe waja kweli ndugu yangu

Huoni wabunge wakuteuliwa wanatoka mikoa mingine lakini wachaga .Taratibu mkulu

Kati ya watendaji wote wa ngazi za juu niliowataja wa makao makuu hakuna hata mmoja zaidi ya hao 3 ambaye anauhusiano ama wa kuolewa ama wa kuoa huko uchaggani.

Mwenye hilo na aseme,tuache unafiki na uongo tutaigawa nchi hii bila sababu za maana .
 
Ndio maana nimemuuliza mkamap alete ushahidi tofauti au ataje hao ambao yeye anadhani ni wachaga zaidi ya hao watatu waliotajwa hapo. Unajua ccm imekosa cha kusema kuhusu upinzania na sasa watakuja na vitu vya ajabu ambavyo havipo.

Wakipewa data wanakimbia kama zemarcopolo sijui kaishia wapi.
 
Tatizo lenu wengi ndio hilo wanao watakia mema kwa kukifanya chama kua na sura ya kitaifa zaidi ya sura ya KILI mwaja juuuuuuu

Vitu vya wazi mwabishaaaa .
Mpelekeni mahakamai CHACHA WANGWE kwa kudhalilisha CHADEMA na mkoa wa Kilimanjoro akiwa na nia ya uchochezi kwa kudaganya ya kwamba

1.MAJORITY makoa makuu ni wachaga
2.Wabunge 5 kati ya sita wanatoka KILI
3.Ruzuku ya laki moja imeanza kupelekwa mikoani baada ya yeye kuingia madarakani.
Kwanini tuandikie mate na wino upo !!! Kama mnaona ananjama ya kukiangusha chama mpelekeni MaHAKAMANI kwa maneno yake Harafu mkishinda kesi mmwadhibu ama msimuadhibu naye ikionekana alichosema ni kweli naye afanye atakavyo.
Mambo haya ya kubishana na Radio yanatoka wapi??

Mtu anampango wa kuhujumu chama mnamwachisha uongozi tu na endelee na chama hii ni sawa na uhaini ktk chama.
 
Ama kweli ubishi ni ubishi tu, kila mara ukibanwa kutetea ulichoandika unakosa cha kusema. Ndio maana kwenye ile thread nyingine umejifanya kuwa unamwongelea ndugu yako anayeitwa Mbowe Mkama wakati ambapo unajua kabisa uliyekuwa unamwongelea.

Mkama, hii issue ya ukabila imekosa ushahidi na baada ya dozi ya mpaka kieleweke hapo juu, inaoneka ccm hamna msingi kwenye hili. Wewe tafuta kingine maana hili limekosa msingi.
 
Ushaidi gani unataka wewe ndg yangu
Nimekwambia hivi mpeleke CHACHA mahakamani ama mwiteni mbele ya vyombo vya habari akane aliyoyasema ya kwamba.

1.majority makao makuu hawatoki KILI
2.wabunge 5 kati ya 6 hawatoki KILI
3.Hizo laki moja mikoani zimeanza baada ya yeye kuingia madarakani.
Mda wote mimi hoja zangu zipo hapo sijahama WANGWE mnaye hapo Mbowe mnaye hapo nenda basi hata kwenye vyombo vya habari WANGWE akakane hayo na muwaonyeshe waadishi wa habari makaratasi yote mbona ni rahisi sana. KUSPIN hakusaidii.

Nendeni na list nzima kutokea mfagizi hadi juu mkanushe hilo na wangwe akili.
mje la wabunge nalo mseme hawatoki kili mkanushe wangwe akili,harafu mje la ruzuku muonyeshe mmeanza lini mkanushe wangwe akili .Na mwisho mwambieni wangwe ayakane maneno yake.

Kuhujumu CHAMA ni swala zito msingeliachia hapohapo kumushusha jamaa tu cheo.

Moderator!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!! NAomba muongozo wa JF
Je nihalali kuniita mimi kutaja ID yangu kwamba ni CCM Na marufuku kutaja ID ya jina????
 
naona bado unaendeleza ubishi bila kurudi kwenye majina na makabila uliyopewa na mpaka kieleweke na wewe ukaanza kubisha kuwa huu kuna wachaga zaidi ya watatu waliotajwa pale.
 
naona bado unaendeleza ubishi bila kurudi kwenye majina na makabila uliyopewa na mpaka kieleweke na wewe ukaanza kubisha kuwa huu kuna wachaga zaidi ya watatu waliotajwa pale.

Wewe acha kupotosha watu mimi nimeomba DOC za kiofisi zaidi na nikasema kuandika mtu unaweza andika utakayo.

Ya watu 5 kutoka KILI ni ya wabunge wa kuteuliwa ,wewe waja kweli na SPIN zako na ubishi wa kupika

na nikaongeza kuna uwezekano wa mtu kutoka Lindi lakini ni MSUKUMA kama ilivyo kwa wabunge wa kuteuliwa CHADEMA wanatoka mikoa tofauti lakini ni WACHAGA.

Nimekuambia hicho kibano unajosema ni UBISHI tu unaoondekeza kwanini MBOWE asiende na CHACHA akakanushe na si hapa wewe na mpaka kieleweke kukanusha hapa na kutulazimisha tuamini mnavyosema.

Pia sio kunipa kibano mimi bali muwafahamishe wapiga kura wenu kwa uwazi na ukweli Mchukueni CHACHA na MBOWE akakanushe kwenye vyombo vya habari kwa kuwataja majina kazi zao mahali na makabila yao kama alivyofanya hapa .Mbona mnakwepa hilo???
Hapo tutaamini na kua ule uzushi wa CHACHA na ukome.

pia wabunge wale watano kati ya 6 pia wakanushe tuone uzushi wa CHACHA anayetaka kuhujumu chama.Kama ni uongo na akome kabisa

Pia akane kuhusu hizo ruzuku kua hazikuanza wakati wa uongozi wake

Hizo ndizo hatua mhimu za kufutilia mbali majungu na matope kinyume cha hapo ni SPIN tu.

Moderator!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!! NAomba muongozo wa JF
Je nihalali kuniita mimi kutaja ID yangu kwamba ni CCM Na marufuku kutaja ID ya jina????
 
Wewe acha kupotosha watu mimi nimeomba DOC za kiofisi zaidi na nikasema kuandika mtu unaweza andika utakayo.

Ya watu 5 kutoka KILI ni ya wabunge wa kuteuliwa ,wewe waja kweli na SPIN zako na ubishi wa kupika

na nikaongeza kuna uwezekano wa mtu kutoka Lindi lakini ni MSUKUMA kama ilivyo kwa wabunge wa kuteuliwa CHADEMA wanatoka mikoa tofauti lakini ni WACHAGA.

kama unajua kuwa kuna uwezekano wa kuwa haya unayosema hapo ya kuchanganya mikoa na ukabila, inakuwaje unasisitiza kuwa unajua wabunge 5 kati ya sita wa chadema walikotoka?

Umejuaje?

Nimekuambia hicho kibano unajosema ni UBISHI tu unaoondekeza kama MBOWE aende na CHACHA akakanushe na si hapa wewe na mpaka kieleweke kukanusha hapa na kutulazimisha tuamini mnavyosema.

Pia sio kunipa kibano mimi bali muwafahamishe wapiga kura wenu kwa uwazi na ukweli Mchukue CHACHA na MBOWE akakanushe kwenye vyombo vya habari kwa kuwataja majina kazi zao mahali na makabila yao kama alivyofanya hapa .Mbona mnakwepa hilo???
Hapo tutaamini na kua ule uzushi wa CHACHA na ukome.

pia wabunge wale watano kati ya 6 pia wakanushe tuone uzushi wa CHACHA anayetaka kuhujumu chama.

Pia akane kuhusu hizo ruzuku kua hazikuanza wakati wa uongozi wake

Hizo ndizo hatua mhimu za kufutilia mbali majungu na matope kinyume cha hapo ni SPIN tu.

Moderator!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!! NAomba muongozo wa JF
Je nihalali kuniita mimi kutaja ID yangu kwamba ni CCM Na marufuku kutaja ID ya jina????

unauliza swali ambalo linakufunga mwenyewe, wewe umesema kuwa kuna wanachadema hapa, je kuna kosa gani la wewe kuwa miongoni mwa wana ccm?

Haya ndiyo mnajifunza huko ccm?
 
kama unajua kuwa kuna uwezekano wa kuwa haya unayosema hapo ya kuchanganya mikoa na ukabila, inakuwaje unasisitiza kuwa unajua wabunge 5 kati ya sita wa chadema walikotoka?

Umejuaje?

unauliza swali ambalo linakufunga mwenyewe, wewe umesema kuwa kuna wanachadema hapa, je kuna kosa gani la wewe kuwa miongoni mwa wana ccm?

Haya ndiyo mnajifunza huko ccm?

Mgaya na wewe nitakutaja jina lako !!!!!!! mimi nachukua Paketi za maseji yako nasoma IP adress ya comp unayotumia harafu natuma wajamaa wangu wanakuja kukopi mafili yote yako nakutaja jina ohhhhhhh.Nakutania tu mkulu wangu hicho nikikorobwezo tu.

Mzee tuhitimishe huu mjadala.
 
Fair, tukubaliane kutokubaliana na kuelewana kadri wengi walivyochangia hapa.

Asante mkuu, nakusubiria sasa kule kwenye mjadala wa kama ccm ni chama cha kidini (kiislam) tuendeleze mambo.
 
Kitu ambacho wapenda mageuzi na wazalendo wa nchi yetu tunatakiwa kukikubali bila ni kwamba wanaochangia vyama vya upinzani ni wazalendo sana. Unajua hawa jamaa wote (akina Mbowe, Slaa, Zitto, Ndesamburo na wengine wengi) ni watu maarufu tu na wangetaka maisha ya kutelezea (ufisadi) wangejiunga na CCM na wengine hapa wangekuwa mawaziri (hata PM kabisa) na tusingepata mtu wa kutusemea bungeni!! CCM inawatolea udenda hawa watu. Hawa watu ni wazalendo wenzetu. Wakati mwingine inashangaza, kuona mtu anahoji kwa nini mtu anasaidia Chadema, kwa argument kwamba wanachama ndio wangekuwa source ya financing ya chama!! Wanachama wenyewe watanzania hawa hawa. Hoja kama hii ikiletwa na watu tuliowazoea kwa kuvuga hoja (mawakala wa mafisadi ndani ya JF) isingejadiliwa sana, lakini ikiletwa na mzalendo mwenzetu, ndipo hapo mimi nahitaji kujua context ya hoja.

Frankly (kwa mtazamo wangu), bila akina Slaa na watu wa aina hii nchi yetu ingekuwa ni zaidi ya Zimbabwe. Hawa wezi waliojificha CCM wangefanya vioja sana. Mimi nadhani tulio na nia njema tuendelee kuwatia moyo wenzetu waliojaliwa kuwa na karama za kusema na pia wakawa wabunge na pia wengine wakatokea kuwa na mali. Vyama vya siasa katika mazingira ya Tanzania vikiachwa viendeshwe bila kupigwa tafu na wenye moyo vitakufa au vitakuwa kama NCCR (samahani kwa wanaNCCR). Chama na katiba nzuri na viongozi wazuri lakini bila ambition ya kisiasa!!!!!

Mimi sisemi tusihoji tunapokuwa na ushahidi kuwa mtu katumia madaraka vibaya au ana finance chama kama NGO yake na kwa maana hiyo hata akikutwa na tatizo asiulizwa wala kuhojiwa. Au mchango wake uwe ndio bei ya yeye ku dictate terms katika chama. Mtu ukiwa na hoja leta ushahidi wote, lakini sio hisia tu. Unajua hawa viongozi (wahanga) wa upinzani wanahitaji sana support ya raia. Wakati mwingine tusichunguze sana makosa madogomadogo kwa saababu tukifanya hivi tutaishia kumark time! Kwa mfano leo hii tukisikia Slaa, Zitto, Mbowe, na wengine kama hao wamehamia CCM tutafanyaje? Of course CCM watasherehekea sana. Na wanaweza wakapata hata mijhela ya ufisadi ili nao wayale na hatimaye wanyamaze milele kutamka neno ufisadi.

Tupigane vita ya ufisadi wote, tusianze kulaumiana. Tuwaache wanaojulikana kwa kuharibu threads waendelee kutia chachandu mijadala. Lakini wengine tuwe focused

Naungana kwa kiasi fulani na wachangiaji wengine kuwa baadhi ya viongozi wa Chadema wako too aggressive kujibu kila hoja! Mimi naona hoja zingine ziachwe zipite maana si kila muulizaji anataka jibu, wengine wanataka kuwaprovoke! Wakati mwingine tumia the power of silence - 'if saying something does not make a difference, then better keep quiet' Mzee Slaa amesema vizuri kama una hoja ya matumizi ya Chadema nenda kweye Audited Accounts zao au mpigie Slaa mwenyewe, au jiunge nao uwe unahaki ya kuhoji!

Habari ya kuchangia vyama ingekuwa clear kama JK angetekeleza ahadi yake ya kuweka sheria kwa ajili ya hilo. Kwa sasa, kama ni shida sana basi hawa wanaotoa michango basi wawe wanaikopesha Chadema (kama mama Clinton alivyoikosha kampeni yake $ 12 miliion). Lakini Chadema ikikopa italipa kutoka wapi? Jamani watanzania, uzalendo ni pamoja na matendo sio kukosoa tu!!!!!!

Samahani maelezo marefu halafu yamekaa kama utetezi kwa Chadema, mimi si mwanachadema, na sijawahi kuwa mwanasiasa (mwanachama wa chama chochote). Lakini nadhani kama tunataka mabadiliko, Chadema wapo pamoja nasi, lakini sio CCM!). Naamini mwanendo wa Chadema haujawa sawa na vyama vingine ambavyo ruzuki ndio imekuwa kila kila kitu. Chadema tangu akina Mzee Mtei, Bob nk, sidhani kama kulikuwa na shida sana ya ruzuku! Hawa wazee walichangia wakapita, sidhani kama walikuwa wanatarajia kuja kuwa marais kupitia chadema! Tuwaamini hata hawa viongozi wa sasa kuwa wanajua kuwa uongozi ni succession na si lazima mafanikio yatokee wakati wao wapo madarakani. Heshima ya kuwa ulichangia kitu fulani kuifia nchi yako inatosha sana!
 
Kuelekea ukombozi ni lazima wachache ama wengi wawe tayari kuumizwa kwa faida ya wengi.

Hii ni vita ya kuelekea ukombozi ,na ijulikane kuwa wafanayabiashara na wenye pesa hawakichangii CHADEMA kwani wanaogopa CCM.

vitu vingine tuwe tayari kusema ukweli mbona hata hapa JF inaendeshwa kwa kuchangiwa na wanachama wake wenye uwezo wa kuchangia?

Mbona hapa hamlalamiki kuwa waache kuchangia?

Nani anamlipa Invisible na JF Crew yote hapa ?mbona wao wanajitolea na kufanya bure?

Ama kujitolea CHADEMA ndio dhambi na kosa?

Nadhani hapa kuna hoja nzuri. Tusitake vyama vingine vifuate utaratibu wa CCM wa kujiendesha kwa kulipana mishahara. Siasa lazima iwe utumishi, na utumishi uwe wa watu kujiolea, siyo kuchuma. Kabla ya Mbowe na Dk. Slaa kuwa viongozi kwa nyadhifa walizonazo leo, utendaji wa wakati ule, chini ya Dk. Aman Kabourou, ulikuwa unalipana mishahara, na chama hakikukua mikoani.

Mbowe alipopiga vita hii tabia ya viongozi kula ruzuku kwa kujilipa mishahara, ilikuwa sababu ya kwanza ya Dk. Kabourou kutafuta mlango wa kutokea hasa baada ya Mbowe kuwa mwenyekiti. Sababu hizi hiiz za ulaji ndizo zilimuondoa Paul Kyara aliyekuwa mweka hazina na aliyeshirikiana kwa karibu na Dk. kabourou kutumbua ruzuku.

Sasa, kwa vyama visivyo na ruzuku kubwa, visivyoungwa na wafanyabiashara wengi (maana waliopo wanachangia CCM), kuna kosa gani kwa kina Mbowe na Ndesamburo kukichangia chama chao? Kuwataka wasichange pesa nyingi wakati wanazo ni mbinu nyingine ya kutaka kukidhoofisha chama hicho. Tuwatendee haki katika hili....Chadema hakina wahindi wa kukichangia, lakini hata CCM yenye Wahindi bado inategemea pesa za EPA! Shame!
 
Kwa maelezo ya Dr. Slaa CHADEMA ni sawa na kusema haina mfadhili hivyo inabidi miongoni mwa majukumu ya uongozi yawe ni kugharimia uendeshaji wa chama.

Kufananisha CHADEMA na TANU ni spin aliyoitumia DR. Slaa kama katibu wa chama ili kukitetea.Ukweli ni kwamba pesa za kuendesha TANU zilikuwa zinatolewa na watu ambao hawakuwa na mamlaka ya kikatiba ya kufanya maamuzi ya chama.Nyerere alikuwa na kamshahara ka ualimu ambako hakawezi kununua hata typewritter ya chama, lakini yeye ndio alikuwa mwamuzi mkuu wa chama unlike CHADEMA ambayo wale wanaotoa fungu ndio wanaotoa maamuzi.Hii sio sahihi.
CHADEMA bado ni NGO.

Dk. Slaa yuko sahihi. Unadhani kama Nyerere angekuwa nazo kama kina Rupia angebania kwa kuwa yeye ni rais wa TANU? AU je, unadhani kama Rupia ndiye angekuwa rais wa TANU asingechanga pesa nyingi eti kwa kuwa angekuwa kiongozi? Usisubiri kusoma threads hapa, soma katiba ya chadema ujue maamuzi yanafanyikaje, na nani ana kauli kwa ajili gani. MBowe ni mwenekiti leo, kesho atakuwa mstaafu, lakini akiwa kiongozi haweze kuona chama kinakosa mchango anaoweza kutoa, akabania eti kwa kuwa kuna watu watasema haya unayosema. Kauli ya Dk. Slaa iko sahihi kabisa.
 
Yale yale, ya chama kina wenyewe na wenyewe ni sisi tuliojitolea tu-vijisenti; kazi kweli kweli
 
Yale yale, ya chama kina wenyewe na wenyewe ni sisi tuliojitolea tu-vijisenti; kazi kweli kweli

Hivi mbali na siasa za kwenye blogu hapa, ni wangapi miongoni mwetu wamewahi kufanya siasa zenyewe na kuona jinsi ilivyo vigumu kuendesha na kufadhili harakati hasa katika vyama vya upinzani? Je, ni nani miongoni mwetu amewahi kutoa pesa yake mfukoni kuchangia harakati za kujenga mfumo wa mageuzi nchini?

Upo uwezekano wa kukebehi watu tu hapa kwa kubonyeza keyboard, lakini watu wale wale hawako tayari kushiriki katika kujenga Tanzania bali kuzomea wachache waliojitoa mhanga kusukuma gurudumu kwa nyenzo walizonazo. Kwa kujua hali ilivyo nchini mwetu, nawapongeza sasa wanaotoa chochote walichonacho kujenga vyama hivi vya upinzani, siyo kwa kuvifanya kuwa miradi ya kuchuma bali miradi ya kuwekeza harakati za kifikra kwa sasa na siku zijazo.

Tukubali kuwa katika harakati za namna hii, wachagiaji watakuwapo na michango yao haitalingana. Huo ndio ukweli ambao hatuwezi kuubeza. Vyama havijengwi kwa maneno tu, na hatuwezi kuwabeza wanaotoa jasho lao la haki kuviendeleza.
 
Nadhani hapa kuna hoja nzuri. Tusitake vyama vingine vifuate utaratibu wa CCM wa kujiendesha kwa kulipana mishahara. Siasa lazima iwe utumishi, na utumishi uwe wa watu kujiolea, siyo kuchuma. Kabla ya Mbowe na Dk. Slaa kuwa viongozi kwa nyadhifa walizonazo leo, utendaji wa wakati ule, chini ya Dk. Aman Kabourou, ulikuwa unalipana mishahara, na chama hakikukua mikoani.

Mbowe alipopiga vita hii tabia ya viongozi kula ruzuku kwa kujilipa mishahara, ilikuwa sababu ya kwanza ya Dk. Kabourou kutafuta mlango wa kutokea hasa baada ya Mbowe kuwa mwenyekiti. Sababu hizi hiiz za ulaji ndizo zilimuondoa Paul Kyara aliyekuwa mweka hazina na aliyeshirikiana kwa karibu na Dk. kabourou kutumbua ruzuku.

Sasa, kwa vyama visivyo na ruzuku kubwa, visivyoungwa na wafanyabiashara wengi (maana waliopo wanachangia CCM), kuna kosa gani kwa kina Mbowe na Ndesamburo kukichangia chama chao? Kuwataka wasichange pesa nyingi wakati wanazo ni mbinu nyingine ya kutaka kukidhoofisha chama hicho. Tuwatendee haki katika hili....Chadema hakina wahindi wa kukichangia, lakini hata CCM yenye Wahindi bado inategemea pesa za EPA! Shame!

Kichwamaji,

Hapa tunajadili viongozi wa juu kutokulipwa lakini naona huwezi kujizuia kutoa vijembe juu ya viongozi waliohama CHADEMA kama Kabouru.

Waliokomaa kisiasa huwa hawaongelei watu waliohama vyama vyao. Jiepusheni kila saa kurusha vijembe kwa akina Kabouru kwani wanaoelewa wanaona wazi ni chuki. Kama hamkuwashambulia hao watu walipokuwa na CHADEMA iweje leo vijembe viongezeke?

Ni sawa na kuanza kumdhalilisha mkeo wa zamani huku mlipokuwa pamoja mlikuwa mnaitana honey kwa miaka na miaka.

Kabouru ameondoka CHADEMA hivyo sio tatizo lenu tena, kama Kabouru ana matatizo yoyote basi sasa ni tatizo kwa CCM. Ondoeni kabisa neno Kabouru kwenye msamiati wenu.

Kama mlitoa msimamo wenu siku kabouru anahama inatosha, baada ya hapo mkiendelea kumshambulia inakuwa sio nguvu ya hoja tena. Hivyo hivyo kwa Wangwe, lile tamko lenu lilitosha kabisa, lakini vijembe vingine vinavyorushwa baada ya hapo ni hatari kuliko hata lile tamko.
 
Back
Top Bottom