MMK
Nakushukuru sana kwa ushauri kuhusu uendeshaji wa fedha kwenye vyama vya siasa. Hata hivyo, Chadema ni chama kinachofanya kazi yake kwa uwazi. Hatuna la kuficha napenda kueleza ifuatavyo:
i) Uamuzi wa viongozi wakuu, tena wanaotumia muda wao wote kwa shughuli za chama, za kisiasa na uendeshaji, ni uamuzi uliofanyika kwa hiari na kupitia vikao halali vya chama. Kwa bahati mbaya maamuzi mengine hayafiki hadharani. Chadema haioni cha ajabu katika hatua hii. Mwalimu Nyerere asingejitolea enzi za uhuru, na kuchangiwa na wapenzi wachache waliokuwa na uwezo leo tusingelikuwa na Uhuru. Nadhani wenye mapenzi mema na nchi hii wataelewa kuwa mapambano tuliyonayo ni mapambano yanayohitaji kujitolea kwa kiwango kikubwa. Viongozi wakuu wa Chadema kwa kutambua hili, waliamua kwa hiari yao, kujitolea ili ruzuku kidogo iliyoko itumike kwa shughuli za uenezi. Bendera, Kadi, nyaraka mbalimbali,ujenzi wa Ofisi stahiki Makao Makuu ya Chama kama sura ya Chama, kuwekeza kwenye miradi ya muda mrefu ya kuitegemeza chama( kazi hiyo imekwisha kufanyika siyo nadharia na kwa yeyote mwenye nia ya kutaka kujua tunaweza kumpa taarifa za kina), ziara za uenezi na kadhalika.
2) Viongozi wa juu wa Chadema ni Wabunge, ukimwacha Mwenyekiti. Mishahara wanayopata ikitumika kuendeleza Chama kuna dhara gani, Chama hujengwa na wenye moyo. Hili halina maana ya wenye kuchangia chama ndio waamuzi katika maamuzi ya chama. Chama kinaendeshwa kwa Katiba, Kanuni, Maadili, na Itifaki ya Chama. Maamuzi yanapofanywa kwa imla hofu hizo hutokea. Kwa Chadema, ambayo maamuzi yake hufanyika yote na vikao halali, mipango huenda kwa kadiri ya Strategic Plan, ambayo nayo si siri, ipo wazi kwenye Mtandao wa Chama, na kila mwenye nia njema anaweza kuipata bila tatizo. iwapo kuna mwenye kuhitaji maelezo ya ziada tuko tayari kuyatoa wakati wowote, vitabu vya Hesabu ya Chama ni mali ya Wanachama na wakati wowote Mwanachama anaweza kuomba taarifa atapewa, na au anaweza kufika Makao Makuu ya Chama akaona vitabu hivyo bila gharama yeyote. Taarifa zote za fedha hutolewa kwenye vikao vya Kamati Kuu, na sijawahi kuona Taarifa ya Fedha ikikataliwa kwa ubadhirifu au kwa sababu yeyote ile. Wajumbe wa Kamati Kuu ni mashahidi. Taarifa ya Fedha hutolewa pia kwenye Baraza Kuu na Mkutano Mkuu kuendana na Ratiba ya Kikatiba ya Vikao hivyo.
3: Fedha za Chadema hukaguliwa na Wakaguzi wanaotambulika kisheria, na huwasilishwa kwa Msajili wa Vyama vya Siasa kwa wakati na kwa mujibu wa Sheria.
4: Ili kuepuka Wachache wenye uwezo kufanya chama kuwa mali yao, Chadema inaoutaratibu ambao sina hakika vyama vingapi unao, wa kutathmini na kutambu mchango wa kila mwanachama kwa maana ya fedha zake anazochangia kwenye chama, muda wake anaotumia kwa ajili ya shughuli za Chama ( hatua hii inafanyika kwa sasa Makao Makuu tu kwa vile Instruments za kufanya Tathmini hii kwenye mikoa na Wilaya bado inafanyiwa kazi na hata ya Makao Makuu bado inaendelea kufanyiwa kazi. Mathalan muda wa mtumishi wa Chama anayefanya kazi baada ya saa rasmi za kazi hutathminiwa na kupewa thamani ya fedha kama mchango wake kwa ujenzi wa chama. Inahitajiwa fikra mpya ili ukombozi tunaoendelea nao uweze kufanikiwa. Lakini kutegemea fedha tu hakutatufikisha mahali.
Hivyo, Tafsiri sahihi ya Kauli ya Mheshimiwa Mwenyekiti wa Chadema, inaweza kuhojiwa katika misingi hii. Nimeona nieleze hili kwa misingi ya uwazi kwa vile Chadema hatuna cha kuficha, chama ni cha wote wenye nia njema, na hata wasiokitakia mema kama wapo ni vema wakajua Chadema inaendeshaje shughuli zake ili wasiohoji kwa nadharia na kwa hisia. Mwenye kuhitaji Taarifa zaidi, Dr. Slaa, anapatikana kwa Simu na +255 784 666995 au +255 754 366 995 au kupitia E mail zangu
slaa@chadema.net,
wslaa@hotmail.com. Nafurahi kwa wote waliochangia kwa angle yeyote ile kwani licha ya kuwa kila mmoja ana uhuru wa kutoa maoni yake, pia kila mwanademokrasia halisi hutambua mchango wa kila mmoja na pia anaweza kuokoteza mawazo mazuri katika michango hiyo. Hakuna mchango uko mbovu tu, hata uliombovu sana unajambo zuri, japo dogo la kuweza kujifunzia. Naomba radhi si nia yangu kutoa mhadhara, lakini kila inapohitajika katika mada yeyote ile nitafanya hivyo kwa maslahi ya nchi yetu, wanachama wetu na wote wenye mapenzi mema.