Watasahihisha makosa baada ya kupata ushauri wa zito, aliutoa akiainisha kifungu cha tatiba 37(2) kitumike kuweka mambo sawa kabla nchi haijasambaratikaKwanza naomba nikiri kuwa binafsi sikumchagua rais John Pombe Magufuli ingawa nilijua atashinda, sababu ni moja tu hakuwa mgombea bora.
Baada ya jina la Magufuli kupitishwa na mkutano mkuu wa CCM kuwa mgombea, wazo la kwanza lililonijia kichwani ni kuwa wajumbe wa CCM walijali maslahi ya chama zaidi kuliko nchi, kuwa walichoangalia wao ni chama kwanza kibaki salama lkn si kuteua mgombea bora ili aje kuwa kiongozi wa watanzania wote na sio kiongozi wa CCM.
Nikajiuliza, Usalama wa Taifa ulikuwa wapi kuzuia hili lisitokee, najua wasingeweza kupinga hadharani kutokana na maadili ya kazi lkn walikuwa na uwezo wa kuzuia kwa vile walijua fika udhaifu wa Magufuli.
Nilitaraji CCM watuletee watu kama Balozi Mahiga, Asha Migiro au Membe wazoefu wa diplomasia za kimataifa. Nilitegemea watuletee watu waadilifu wasio na doa kama kina Agustino Ramadhan, Mizengo Pinda, mama Samia au Shein, angalau basi wangetuletea jasusi la kimataifa kama Kitine kupambana na hujuma za majirani zetu kwenye soko huria la uchumi.
Hivi kweli CCM walishindwa vipi kuteua angalau mmoja bora kati ya hawa wagombea 38 waliojitokeza?
1. Bernard Membe
2. Balozi Mstaafu Agustine Mahiga,
3. Mizengo Pinda,
4. January Makamba,
5. Balozi Amina Said Alli,
6. Profesa Mark Mwandosya
7. Mama Samia Suluhu
8. Jaji Mstaafu Agustino Ramadhan,
9. Asha Rose Migiro.
10.Dk. Ali Mohamed Shein,
11.Dk. Hassy Kitine.
TUJISAHIHISHE, muda bado upo tusirudie makosa tena hapo 2020 tutajuta.
Mawazo huru kutoka kwa mwanaJF mzoefu Quinine.