Kwanini CCM Iko Matatani?

Mkuu wangu Mwanakijiji majibu ulopewa nadhani viongozi wa CCM wanatakiwa kuyatazama kwa makini na kutafakari kwa sababu Ukweli upo kati yake..CCM wamekuwa wakipuuzia sana maswala muhimu ya Kichama badala yake wakafikiria kutumia fedha la ulaghai wakati wakitumikia Azimio la Zanzibar. Nakumbuka wakati wa Mwalimu wananchi wengi hawakujali umaskini wao, waliendelea kuulinda pamoja na machungu yote lakini leo wanapoona baadhi yao wakitajirika kwa jasho la wananchi na maisha na hakuna mwelekeo kabisa tumepoteza dira hapo ndipo wingu linapotanda juu ya CCM.

Tazama jinsi JK alivyoweza kuzoia kura mwaka 2005 kwa kuudangany Umma tu ya kwamba atakuwa tofauti na waliomtangulia na kuweka ule upinzani wake dhidi ya uongozi mzima wa CCM kwa kutoa ahadi zinazokabiri matatizo yao kisiasa ndipo alipowabiga bao kina Mbowe na Lipumba na wengine hata kusema ule utabiri wa Mwalimu kuwa ushindani utatoka CCM umetimia..

Leo hii wananchi hawadanganyiki tena na pengine niseme Ahsante Kikwete kwa kutuonyesha kwamba CCM haiwezi kuaminika tena lakini tukumbuke tu ya kwamba CCM bado ni maarufu sana. Tatizo la CCM ni kichwa, ni kukosa kiongozi ambaye ni MTU wa watu WATU mwenye kutukuza UTU..

Na amini maneno yangu akitokea mtu mwenye utashi na maarufu sana akaunda chama ama kujiunga na chama chochote cha Upinzani basi nina hakika kabisa CCM wataondolewa madarakani. Leo hii bado nina mashaka makubwa na viongozi waliojipanga kugombea Urais kmwaka 2015 na nachelea kusema kwamba CCM wanaweza kuitumia nafasi hiyo kumweka mtu ambaye atakuja na ahadi kama za JK na kwa sababu Wadanganyika ni wepesi wa kusahau, hawajifunzi kutokana na makosa na kuna uwezekano mkubwa sana wakarudia yale ya mwaka 2005.
 




umechambua vizuri sana........bravo
 

"But for how long? There is a new official opposition in the country; it is urban and has youthful support, even in the high schools. It is called Chadema (Chama Cha Demokrasia na Maendeleo). It baits the government in parliament, asking awkward questions, and is brazen enough to be distasteful to many people. It is always in the news, especially in Swahili. Some even call it “activist.” And the word is that the official party, the CCM (Chama Cha Mapinduzi), which has ruled the country since independence, is nervous but cautious" - M.G. Vassanji onTanzania: land of constant complaints
at Tanzania: land of constant complaints - World - Macleans.ca
 
1.Ukosefu wa ubunifu
2.Kutokidhi mabadiliko ya nyakati
3.Kuacha misingi yake mfano ahadi za mwana TANU/CCM
4.Kuua fikra mbadala,aliye na fikra tofauti ndiye adui wao eg H. Kolimba
5.Kuendekeza matabaka,huyu mwenzetu,yule siyo mwenzetu
6.Kuruhusu hela kuwa utambulisho wa heshima,
7.Kutekwa na matajiri
8.Ahadi zisizotekelezeka
9.Kushindwa kusimamia rasilimali na kuruhusu uporaji kwa jina la uwekezaji
10.Kushindwa kupambana na ufisadi

Hizi ni baadhi ya sababu
 
Jibu la hilo swali liko kwenye statement maarufu ya Kolimba (RIP); CCM imepoteza mwelekeo.
Tanu kilikuwa na mambo ya msingi ambayo kilisimamia; kupigania uhuru, kuwatetea wanyonge (wakulima na wafanyakazi), kusimamia haki, kujenga taifa kwenye misingi ya ujamaa na kujitegemea nk.

Ebu waulize CCM leo ni nini wanasimamia, majibu utakayopata, kama siyo tu kwamba yatatofautiana kutoka kiongozi mmoja hadi mwingine, lakini pia yatakuwa tofauti kabisa na hali halisi ya ukweli wa mambo.
Ukiuliza maswali mepesi kama ndo utajua jinsi ccm ilivyo hopeless:
Hivi CCM inafuata siasa ya ujamaa au ubepari?
Hivi ccm ni mtetezi wa wanyonge au mtetezi wa matajiri?
Hivi ccm inaunga mkono au inapinga hujuma, dhuruma, za aina yoyote kwenye jamii?
Majibu watakayokupa yote yatakuwa tofauti kabisa na uhalisi wa utendaji wao. Kimekuwa chama kisicho na dira wala mwelekeo.

Pamoja na hilo, suala la uongozi dhaifu nalo linachangia kwa kiasi kikubwa.

 
Ningekuwa miye kiongozi wa CCM wa ngazi yoyote ile ningefanya haraka na kuprint majibu haya ya Watanzania. Haya ni majibu ya wazi zaidi na ambayo kama siyo ya kweli kabisa basi yanakaribiana na ukweli kama vile mdomo wa simba unavyokaribia shingo ya swala akinywa maji. Ni maneno ambayo yanatokana na nostalgia ya aina fulani. Watu wanaikumbuka "CCM" na sasa hawaioni. Wanaona chama kinaitwa CCM, wanaona viongozi wanaitwa "Viongozi wa CCM" na wanakutana na wanachama wanaitwa "Wanachama wa CCM". Lakini "CCM" yenyewe hawaioni.

Kuna kitu ambacho kwa macho ya kawaida kinaonekana katika fikra za watu kimekosekana. Kwamba CCM hii siyo ile ile. Kuna vitu viliitofautisha CCM ile na hii ya sasa na hapa ndio kiini cha mawazo ya watu wengi. Swali ambalo litaendana na hilo ni kuwa je CCM yaweza kujirudi na kurudia baadhi ya misingi yake bila kujikuta inavunjika? Kwa mfano, ikianza kutetea tena wakulima na wafanyakazi at the expense of the rich and businessmen haiwezi kujikuta kwenye matatizo yale yale? Wafanyabiashara wakikimbia na kujiunga na upinzani na kuanza kuunga mkono CCM itafanya nini? Je yawezekana hoja ya "kutenganisha biashara na siasa" ina lengo zaidi la kuzuia upinzani kuliko kuiokoa CCM? Sasa hivi wafanyabiashara wakubwa na wadogo wanaunga CDM kwa mfano, je wanafanya hivyo at the expense of CCM?

Lakini muda haurudi nyuma. Hatuwezi kurudi wakati wa TAA, TANU au wakati wa CCM ya Nyerere. Lakini haiwezekani kurudia misingi? Kama mtu umejenga nyumba imefika hadi unapaua na ukakuta kuwa kumbe msingi ni mbovu utaendelea kukaa kwenye hiyo nyumba tu? Je utaendelea kuipamba na kukaribisha wageni? Je utaendelea kuombea tu kuwa isije kupigwa na kimbunga au ardhi yake kulowa ikatetereka? Misingi ikidhoofika ni jengo gani laweza kusimama? Unakumbuka hotuba ya Nyerere juu ya "misingi imetikisika?".
 
Mwanakijiji, posti yako ya mwisho hapo juu inaongelea TANU sio CCM!
 
Tatizo la ccm ni wizi wanaoufanya ndio umesabisha tusikipende hiki chama,wala hamna mtu anayekichukia eti chadema wamepanda chuki, dawa ni kuacha wizi na wezi wote wawajibishwa na kurudisha walivyotuibia.
 
Tatizo ni kwamba ndani ya CCM sasa hivi meritocracy ina kufa. Watu hawapewi au kupata vyeo kutokana na sifa kwa hiyo wale wenye sifa wanachoka na kuihama CCM. Watu hao wakihama CCM na kujiunga na upinzani ina maana wana wapa option wananchi. Zamani vichwa vyote vikubwa vilikua CCM, siyo hivyo tena.

Ngoja nitoe mfano wa kifo cha meritocracy ndani ya CCM na hili ni tatizo la kimfumo:
Kwenye kutafuta wagombea wa ubunge wa CCM kuna kura za maoni. Kushinda kura za maoni hai maanishi huyo mtu atakua mgombea moja kwa moja. Wanaweza kwenda na 2nd choice au 3rd choice. Sasa ikiwa hivi mawili yana weza tokea

1. Mtu aliyeshinda kura za maoni na kutoswa ana amua kuhama chama na kugombea jimbo hilo kupitia chama kingine. Kwa vile tayari ana umaarufu jimboni hapo inakua rahisi kushinda.

2. Watu wamempa mtu ushindi kwenye kura za maoni halafu mnamtosa ina maanisha mna pandisha hasira wananchi na wanaishia kutafuta mtu mbadala. Wao wamempigia kura wakitegemea ndiye atakae peperusha bendera ya chama. Sasa mkimtosa mna tegemea nini?

Pia sasa hivi CCM kuna mtindo wa kugawa vyeo vya upendeleo haswa kwa watu ambao hawatakiwi na wananchi. Hii yote ina haribu mvuto wa chama. Unakuta mtu kakataliwa na wananchi lakini anapewa ubunge wa viti maalumu? Au unakuta mtu ana bebwa kwa vile tu ana undugu na fulani.

Kama CCM inataka kuendelea kubaki madarakani inabidi waweke mfumo ambao wale watu wenye sifa na wanao takiwa na wananchi ndiyo wanapewa nafasi. Waache kulazimisha watu kumkubali mtu kwa vile tu ni kipenzi cha mtu fulani ndani ya chama. We need MERITOCRACY.
 
Tatizo la ccm ni kiongozi wake mkuu, haya mengine yote ni matokeo ya kiongozi dhaifu, ccm itakapopata kiongozi mkuu imara itaimarika kwani tayari chama hiki kiliasisiwa katika misingi imara. Udhaifu wa uongozi wa juu ndio unadhoofisha mpaka misingi ya chama. so dawa hapa bila kumungunya maneno ni kumbadilisha kiongozi wa juu na kumpata kiongozi imara. Ukiniuliza nikuambie kiongozi imara kwa sasa ccm ni nani hilo tuwaachie wana ccm wenyewe. lakini siwezi sema el, huyu ni fisadi tu na mwenye taama ya mali na wala hana utu na huruma kwa waTZ hata chembe. By the way yeye ni mmoja wa matatizo ya waTz ya sasa.
 
Ni vigumu sana kulinganisha CCM ya wakati ule tunalipia kadi zetu za uanachama na hii ya sasa ambayo wanachama wakihudhuria mikutano wanadai/wanalipwa posho!
Mie naona wamejitahidi sana kung'ang'ania madaraka kwa miaka 20 tangia vyama vingi viruhusiwe kisheria. Wako wapi akina KANU na UNIP?
 
Kuanzisha mitandao ya kifisadi hasa kwenye uchaguzi wa 2005, kukumbatia wafadhili wa chama(CCM) ambao lengo lao ni kukwepa kodi, Mwenyekiti wake wa taifa kutokujua kwanini yeye ni mwenyekiti na majukumu yake nini, kutokujua kwa viongozi wake tangu shina mpaka taifa kwamba Tanzania sio maskini bali wao ni maskini wa akili na fikra na kwa hiyo kuendelea kutegemea wezi wa kimataifa. Tamaa, uchu, ulafi ukatili na kutowjibika kwa viongozi wake.....................................
 
mimi nafikiri tatizo kubwa ni makundi yaliyopo ndani ya chama, mambo mengine yalikuwapo hata enzi za tanu mfano mafisadi walikuwepo ndio maana likapitishwa azimio la arusha enzi ile walikuwa wanaitwa wanyonyaji au wahujumu uchumi. makundi hasa ndio kinakitafuna chama chetu na serikali yake, na ndio chanzo cha kuvuja siri nyingi za chama na serikali na hii ni hatari kwa ustawi wa chama
 
Viongozi wa ccm wanashiriki direct and indirect kuua chama aidha kwa kujua au kutokujua. Ukiwasikiliza mara nyingi wanasema serikali amefanya mambo makubwa kuwaletea maendeleo watanzania kitu ambacho wahusika yaani watanzania wa kawaida hawa kioni. Nita toa mifano michache.
1. Hivi karibuni Mkapa ameenda Igunga alipofika huko, akasema anajisikia vizuri kwa sasa anaweza kusafiri kutoka Dar mpaka Mwanza kwenye barabara ya lami ambayo imejegwa na serikali ya ccm. Kikubwa hapa Mkapa alitaka kuwaaminisha wana Igunga kwamba serikali ya ccm imejitahidi kujenga barabara hiyo, hapo alitaka wanaigunga waipe ccm ili iwafanyie makubwa zaidi. Sasa nani asiye jua udhalimu alioufanya huyu Mkapa. Hivi pesa alizoshiriki kupora zingewekwa kwenye maendeleo tungekuwa wapi sasa hivi? Kwa mwenye akili akisikia kiongozi mkubwa kama huyu kwenye chama anafuka hivyo anazidi kuichukia ccm hata kama hajasoma atajua Mkapa anadanganya wajinga.
2. Juzi juzi tulimsikia Wasira anasema Mungu ameumba dunia kwa siku sita, lakini angependa ingeiumba kwa siku moja. Manake hapa ccm haiwezi kuwaletea maendeleo watanzania kwa muda mfupi kwa hiyo waendelee kusubili itawaletea tu. Kwa hakika hii ni kauli ya kejeli mbele ya waliokuwa wanamsikiliza.
3. Kila mtu ni shahidi ccm inatoa ahadi inashindwa kutimiza. mfano maisha bora kwa kila mtanzania yamekuwa maisha magumu, mara "tatizo la umeme litakuwa historia" limekuwa janga la kitaifa.
4. Wizi na ufisadi uliokithiri wakati viongozi wa ccm na serikali wakikomaa serikali inawajali watanzania na itawaletea maendelo. kauli kama hizi na nyingine nyingine kama hizi zinaharibu na kupoteza hadhi ya ccm. Mie nashindwa kujua kama viongozi wanajua matendo yao na maneno ndo vinaua chama, haya yakiendelea ccm inajizika kwa kujua au kuto kujua.
 
Mkuu wangu nitakujibu swali lako ktk paraghraph ya mwisho..
Usitegemee CCM wanaweza kurudi kule walikotoka, haiwezekani CCM kurudisha misingi ya ujenzi wa taifa letu kwa sababu tumeisha ondoa imani hiyo kichwani sii rahisi kuirudisha..Nyerere aliweza kukataa katakata kufungamana na siasa hizi iwe ya kushoto ama kulia kwa weledi wa hizi siasa zao ktk maswala la ukoloni mamboleo tofauti ambayo hayana tofauti kabisa na Ukoloni wa kutawaliwa.

Maadam tumepokea na kuweka mikataba ya kimataifa na kuukubali ubepari kiasi kwamba tumekubali kuuza ardhi na rasilimali zetu kwa wawekezaji na mataifa ya nje hatuwezi kamwe kurudisha misingi ile kwa sababu mikataba yenyewe imewatazama Wafanyabiashara na sii Wakulima na Wafanyakazi. Na hata kama Chadema wataingia madarakani hawawezi kubadilisha lolote zaidi ya kubana sheria pale tulipoziacha uchi lakini nao hawawezi kueteta Wakulima na Wafanyakazi ktk uchumi ambao tayari umekwisha uzwa..

Kama umemsoma Pinda akipiga kelele na Barrick utagundua kwamba mambo mengi yamefanywa na vioongozi wetu bila kujua ama kuwa na weledi wa hii mikataba kwani Barrick ni wafanyabiashara na huongozwa na fikra za kibiashara zaidi ya hudruma au kutoa huduma. They are for profit! hivyo kuwataka Barrick watoe huduma kwa wananchi iwe maji, shule au umeme inaondoa malengo yaliyowaleta nchini na zaidi ya hapo kwa nini wagawe umeme bure kwa wananchi wa vijijini wakati viongozi wetu wenyewe hawagawi umeme au maji toka nyumba zao kuwasaidia jirani zao? - It doesn't make sense at all. Na zaidi ya hapo Barrick wanatudai zaidi ya billini 120 (overpaid taxes) hizi serikali yetu walizifanyia kitu gani na kwa nini wasipige mahesabu ya matumizi ya kodi wanazopokea kutoa huduma hizo kwa wananchi wa sehemu zenye madini?..

Hakuna sababu nyingine zaidi ya UFISADI...CCM wanaweza kurudisha imani ya wananchi kama wataweza kupiga vita Ufisadi lakini tatizo ni kwamba Ufisadi ndio dini ya viongozi wengi wa CCM. How do you go around that ndio swali gumu sana kulipatia ufumbuzi...I think the only solution ni Chadema ambao vita yao kubwa ni Ufisadi na kaa wataweza kupambana na Ufisadi nina hakika yapo mazuri yatajitokeza.
 
<br />
<br />
we vipi? Mada umeielewa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…